Nishati kutoka kwenye jua, isiyotumika huwa inakwenda wapi??

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
"Energy can neither be created nor destroyed, but it can be transformed from one form to another" ~ Newton’s Law of energy Conservation.

Kwamba nishati haiwezi kuundwa wala kuharibiwa, lakini inaweza kubadilishwa kutoka form moja kwenda nyingine, sasa Solar energy kutoka kwenye jua isiyotumika na mimea kujitengenezea chakula huwa inakwenda wapi?.

Unaweza kudai kuwa inatumika ku support photosynthesis na kutoa joto(heat energy) kwa ajili ya dunia, lakini kiukweli si yote inayotumika ku support photosynthesis.

Majangwa hayana mimea, bahari hazina mimea, lakini kila siku zinafyonza solar energy ya kutosha nani tangu dunia inaumbwa mpaka leo.

Na ikumbukwe pia asilimia kama 98 ya viumbe vya baharini na nchi kavu miili yao hujizalishia energy lake yenyewe kwa mifumo yake ya ndani, kwa hiyo havihitaji solar enegry kama direct source ya nishati kwa ajili ya miili yao.

Sasa swali ni je hii energy isiyotumika kwa mimea kujizalishia chakula chake kwa huwa inakwenda wapi??

Inarudi kwenye jua??, Kivipi??
Au ndio hio inayohifadhiwa kwenye kiini cha dunia(earth core)??

Lakini pia tukumbuke kitaalamu binadamu wote ni black-bodies maana yake tunatema nishati ya kutosha hususani joto(heat energy) kutoka kwenye miili yetu.

Nishati ya joto kutoka kwenye mwili wa mwanaume inayotemwa kwa siku ni wastani wa 10.5MJ/siku au 120Watts na kwa mwanamke ni kama 97Watts, hii ina maana kuwa solar energy kamwe haitumiki kutupashia sisi joto miili yetu maana kama ingekuwa inapasha joto kanuni za sayansi zisingeruhusu miili yetu kutoa joto pia.

Simply ni kwamba miili yetu inazalisha joto la kujitosheleza na joto la ziada linalobaki hutupwa nje ya mwili kila siku, kwa kuwa kamwe haiwezekani kuiharibu nishati.

Kama solar enegry haifonzwi na miili yetu, je ile ziada inayobaki baada ya mimea kufyonza huwa inapelekwa wapi, maana energy can neither be destroyed .??

Umeanza well katika argument yako.
Nitoe mfano katik hiyo dhana ya Energ cn neither created not destroyed bt can me transformd from one to another.

Kama unakubali dhana hii ilitakiw pia usisem kuwa Our bodies zina zalisha energy nop ila zina transform energy katika form ambayo itaenda katika surounding.

So ile energy iliyo kuwa absorbd na mimea kutoka katika jua ili hiweze kutumika lazim ipitiea process kadhaa ikiweo hyo photosynthis then respiration.

Na hiil hii emegry ambayo mimea imechukua itachukuliwa kama food kutoka kwa mimea then digestion then respiration.

Kiujumla kuna process kadhaaa hapa tunapata food chain katika kusambaa kwa energy hiii.

Ila kumbuka hakun device au chochote chenye eficieny ya 100% lazima kuwa kuna loss.

Enegry inayobak kutoka kwenye jua inakuwa transformd katika other forms of energy na hapa hata human akachukua fursa na kuipeleka kwenye mechanical , electrical, heat energy. Etc au nyingine nying inapotea bure
 
asigwa said:
Energy can neither be created nor destroyed, but it can be transformed from one form to another" ~ Newton’s Law of energy Conservation

I bound to fail to correct your scientific misconceptions,

Hakuna 'Newton law of Energy conservation',hiyo ni First law of thermodynamics na kama ulitaka kui-attribute,ulitakiwa ui attribute kwa Michael Faraday

Tuje kwenye swali lako,Ulimwengu sio Jua na Dunia tu,sisi tupo ndani ya solar system na kwenye solar system kuna sayari nane nyingine zinazopokea solar energy

Pia solar system ipo ndani ya Milky way galaxy,na Milky way galaxy nayo inaunda clusters of galaxies

So hapo tunaona kuwa,hata kama Dunia inatumia 0.1% ya solar energy,Energy iliyobaki inatumika sehemu nyingine

Yet,first law of thermodynamics haijawa violated kwasababu ulimwengu ni closed system!
 
Mkuu unaposema earth ni closed system una maana gan???
 
Closed system sio earth ni solar system. Ambapo ndio nyumbani kwao na dunia pamoja na sayari nyingine. Use mwepesi kuelewa usilete vichekesho humu
 
Mkuu unaposema earth ni closed system una maana gan???
Closed is simply a system which does not interact with its sorroundings in any way

That is,it is neither exothermic nor endothermic,it's absolutely isolated

Hakuna sehemu niliyosema Earth ni closed system,ingekuwa closed system isingetoa wala kupokea solar energy

But universe by definition is perfect closed system,for it is totality of existence
 
Closed system sio earth ni solar system. Ambapo ndio nyumbani kwao na dunia pamoja na sayari nyingine. Use mwepesi kuelewa usilete vichekesho humu
If you delve more deeply,hata na wewe utajiona unachekesha tu

Solar system bado hai qualify kuwa closed system,to the contrary,solar system ni open thermodynamic system

Sio closed system,kwasababu even solar system itself takes one cosmic year to orbit around the milky way's galactic center
 
Je hiyo energy iliyobaki yawezekana inakuwa absorbed na dark matter,Nyingine kubadilishwa ikawa dark energy na nyingine ikiingia ndani ya black holes kupeleka Kwenye parallel universe.?kama kuna parallel universe Je yawezekana universe yetu sio closed system?just thinking.
 
Naomba kuwauliza wataalam wa physics.kati ya classical physics na Quantum physics ipi inaelezea Uhalisia wa mfumo wa ulimwengu kwa ufasaha zaidi.ie Absolute Reality.kama swali limeeleweka
 
Kwa hapa duniani, electromagnetic energy from sun huwa inakuwa either absorbed, transfered or reflected back by earth particles, be it solid, liquid or gaseous.

Nishati inayokwenda kwenye sayari zingine za solar system yetu, i have no idea vile zina interact.
 
Back
Top Bottom