Nishani ya Ndege: Magufuli kampa Mzee Mapunda, Kikwete alimtunuku Tony Makinda

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
IMG_20190103_223955.jpg
 
Wanabodi...

Napenda kujua mwenye ufahamu wa hili.Baada ya shirika la ndege la Africa Mashariki kuvunjika tumeambiwa kuna rubani alirejesha ndege nyumbani Tanzania kutoka Kenya.

Juzi mhe Rais alimtambua Rubani Mapunda kama ndie rubani alirejesha ndege hiyo lakini kupitia hii document hapa chini inaonekana Rais Mstaafu Kikwete nae alishawahi kutoa tuzo (nishani) ya mwenge kwa rubani mwingine.

Je, kuna ndege mbili zilirejeshwa na marubani wawili?

Tusaidiane watanzania.
IMG-20190103-WA0038.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi sijaelewa tatizo lipo wapi! zaid ya kukuza mambo tu

1. kwanza ieleweke waliosaidia ATCL kuwepo sio mtu mmoja ni watu wengi sana, wanaweza fika kumi kila mmoja kwa namna yake so kunauwezekano huyo nae alikuwepo

2, pia hizo nishani naona zinamadaraja, hii inamaanisha wapo wengi na wanatofutiana madaraja.
 
Tukipiga kura kwa kuzingatia viashiria vya historia ya uongo, takwimu feki, maamuzi yenye kuishia njiani, ukurupukaji, mbwembwe, usanii, kutaka kushindana, kutakuwa na urazini(irrationality).

Haraka sana tutampata mchawi wetu!
 

Wakati mwingine tuwe tunajikumbusha ya zamani:

Nakumbuka,taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi wa wakati huo Ndugu Phillemon Luhanjo ilisema yafuatayo:
"tunuku hizo zilikuwa sehemu ya sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo zilifikia kilele chake Desemba 9, 2011, na zimetolewa katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Nishani alizotunuku Mheshimiwa Rais Kikwete ziko katika makundi matatu ambayo ni:

  1. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo hutolewa kwa Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao waliingia madarakani kwa njia za kikatiba na wameendelea kuonyesha maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
  2. Nishati ya pili ni Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili inayotolewa kwa Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu Wastaafu walio hai ama marehemu na walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka katika madaraka wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya Ofisi yao.
  3. Nishati ya tatu iliyotolewa ni Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne ambayo hutolewa kwa raia ambao walishiriki katika harakati za kupata uhuru na walionyesha vitendo thabiti vya kizalendo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru na wameendelea kuonyesha maadili mema ya kusifika na kuigwa. Nishani hiyo pia hutolewa kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuendelee kuwa wazalendo.
 
Back
Top Bottom