Nisave nikusave kwa ajili ya status view nakerwaga na hawa watu nakosa cha kufanya

Kwenye status jaribu kuweka mambo ya busara kwani mwenye namba yako popote duniani anaku- view.
 
Of course inakela Sana,juzi Kuna mdada kaniibukia na swaga Kama hizi ,sikumjibu chochote Ila niliishia kumblock tu.

Kitu kingine kinachonisikitisha Ni pale unapomuona mtu mzima na unaamini Yuko siriazi na maisha lakini kutwa kupandisha status za WhatsApp utadhani Kuna malipo.

Kuna jamaa fulani nafanya naye kazi siku za karibuni amekuwa siriazi Sana kila baada ya dakika tatu anaweka status ,nimeamua kum-Mute maana naona Kama Ni upuuzi Flani kwa mwanamme kukaa unaweka status za kilofa kila dakika.

Wanaume tuwe siriazi na maisha mambo ya status tuwaachie wanawake.
Dah wewe una shida mkuu Yani status za mtu zikuumize na u judge mtu negative something fish oooh
 
Back
Top Bottom