Nisamehe kama nakufuru, nahitaji kufahamishwa

Huwa napata shida sana kufanya mijadala na watu ambao hawapendi/hawawezi kujibu hoja moja kwa moja. Hebu mkuu, eleza biblia inaposema Mungu aliufanya moyo wa farao uwe mgumu inamaanisha nini?
Hawa jamaa huwa wanajitoa ufahamu
 
Hapo juu umesema kuwa Mungu hujua mwisho wa mtu. Hii inamaanisha kuwa binadamu hatuna free will. Kwa sababu kama mwisho wangu ni kuwa gaidi, inamaana huo mwisho ulipangwa kabla hata mjmi sijazaliwa na ndiyo maana Mungu akaujua. Kwa hiyo si mimi ninayetenda makosa bali aliyeniweka ndiye anapanga nitende makosa.
 
Basi huyu Mungu atakuwa mkatili sana. Fikiria ananifanya mimi nimbake bibi kizee, mimi nikiwa naamini ni tamaa zangu kumbe ni yeye ameshinikiza nifanye hivyo kwa sababu zake.
Halafu ikifika siku ya mwisho ananichoma milele kwa kosa la kubaka ilhali yeye ndiye aliyefanya nibake.
Huyo Mungu atakuwa Ni zaidi ya Adolf Hitler
 
Angalia sana unachoandika, hata hivyo vidole vilivyotumika kutype ujumbe wako ni Mungu amekupa uwezo. Kama huna mchango wa kuchangia nyamaza au pita bila comment. Usije ukapitia magumu zaidi kwa kuamini yaliyoandikwa katika historia ya Mungu na watu wake ni mauzauza. Be humble hata pumzi unayoitumia na mapigo ya moyo wako siyo mauza uza ni uumbaji ambao yupo aliyeumba na huyo ndiye Mungu. Umepata wapi ujasiri wa kusema ni mauzauza mambo yahusuyo Mungu?
Yaani tatizo lenu ndio hilo mkiishiwaga hoja mnaanza vitisho vya kipumbavu ,
 
Huwezi kuona msitu ukiwa ndani ya msitu...toka nje ya msitu uone msitu.....
 
Alitaka kujidhihirisha kwa Pharaoh kuwa yeye ni Mungu.

Huyo Pharaoh umemsoma vizuri ukatili wake?
Ukatili wake siumetokana na Mungu kuufanya moyo wake kuwa mgumu so inakuwaje huyo Mungu ana muhukumu tena , if tukisema Mungu hajielewi tutakuwa tunakosea !?
 
Ninavyofahamu mimi ni kwamba farao alikua kiongozi mbishi na jeuri,kiongozi asiyekubali jambo au ushauri wowote,kiongozi asiyekubali kushindwa lolote.ni kama tu ilivyo kwa baadhi ya viongozi wa dunia ya leo walivyowabishi.Sasa swala la binadamu kuzaliwa hivyo niswala la maumbile jinsi mtu alivyozaliwa na tunaamini ndivyo Mungu alivyomuumba na ndivyo pia mwandishi alivyomaanisha.
 
daahh ukiwa Muumini wa hizi dini yakupasa uache kutumia logic kabisa , Kwa hiyo Mungu alikuwa anataka atukuzwe na kupokea utukufu wake , kwa kutumia njia ya kum-monitor farao na kumfanya afanye maovu bila ya Matakwa ya farao , halafu hapo hapo ana mtuhumu kuwa Ni mdhambi '' Hivi huo sio uonevu !?
Logic gani unayotaka kuitumia wakati mambo mengine yanaeleweka kwa akili za kawaida tu.
 
Mkuu,Swali zuri sana?Je nini maana ya FREE WILL?Je Unafikiri Free will inakupa uhuru wakwenda nje ya Mpango wa Mungu au kumzidi Mungu Ujanja?Je unafikiri Free will inakupa uwezo zaidi ya MUNGU?Tumtazame Farao na Musa sasa.Je unafikiri Musa na Farao walikuwa ndani au nje ya Mpango wa Mungu?Je unafikiri Matukio yaliyotokea wakati wa Musa na Farao yalisimuliwa kabla au baada?

Napenda ufahamu kwamba katika maandiko ya Biblia unayoyaona yalisimuliwa baada ya kutokea na sio kabla ya kutokea na kuna uwezekano kabisa kwamba mwandishi hakuwa Musa bali ni mtu mwingine kabisa.Kwa mantiki hio basi unaposoma maandiko haya lazima uongozwe na Roho wa Mungu ili uelewa hasa mantiki ya andiko.

Waisrael walikuwa watumwa Misri kama ambavyo Waafrika walitawaliwa na Wakoloni.Katika hali ya kawaida unajua kwamba katika harakati za kutafuta ukombozi wakoloni hawakukubali kirahisi vivyo hivyo Pharao hakukubali kirahisi.So ni kweli Mungu alimfanya awe na Moyo Mgumu ashindwe kuelewa kwamba anatakiwa awape hawa watu uhuru wao kwa sababu ya kupenda kuwanyonya.SO kwa ufupi kabisa NDIO MUNGU HURUHUSU TUWE NA MIOYO MIGUMU ILI TUONE UKUU WAKE NA HIO NI SEHEMU YA FREE WILL NA SIO INTERFERENCE YA MUNGU.

MAISHA NI MACHAGUO.

Ubarikiwe
Vipi wewe roho mtakatufu unaye?
 
Mkuu mungu ana upendeleo sana tu. Wewe ona status anayowapa waisrael kwenye biblia.
Kwani Biblia kaandika nani?Hata historia ya wachaga,Wamasai na hata Wajalua ikiandikwa na wajaluo lazima itawapandisha wajaluo.Umenielewa?Hata mm nikikupa historia yangu itanipendelea mimi?
 
Back
Top Bottom