Nisamehe kama nakufuru, nahitaji kufahamishwa

Ukiamua kuchukuwa kisu na kumchoma mtu, huenda anaekuamulia ni Mungu (Shetani tunamsingizia bure) kwa kuwa Mungu alishakuumba ni mtu wa motoni anakuamuru ufanye kazi yako. Kamwe binadamu hana free will!!

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Kosa lililopo hapa ni kuwa simulizi hili linasomwa kama historia.

Simulizi hilo sio historia. Kuna mambo ya kuangalia katika simulizi hilo.

Hayo ni mazingira au tamaduni za wakati huo, mwandishi wa hilo simulizi aliwaandikia kina nani, lengo la mwandishi lilikuwa ni nini. Simulizi hili lina ujumbe gani kwetu; sisi tunaoishi baada ya hao walioandikiwa?

Je, hayo umeyazingatia? Tunaposoma biblia tuache kufikiri kuwa ni matukio ya kila siku yaliyotokea.

Biblia ni neno la Mungu sio matukio ya kila siku ya watu; kazi za kiakili sio matukio ya kila siku ya watu.
Wewe unaonekana hujaelewa hoja yangu

Hoja yangu mimi sio kufanya comparison ya mazingira ya zamani na ya sasa, hoja yangu imejikita katika maandiko ambayo yamesema Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu.

Na wewe umepinga kwamba Mungu hawezi kufanya hivyo (sijajua kwa mantiki gani ila nahisi ulitumia mawazo yako na sio hoja kibiblia) nimekupa reference ya biblia inayo support hayo madai halafu we unakuja kuniambia habari za simulizi (kitu ambacho ni irrelevant na hoja niliyoisimamisha)

Hoja hapa ni kwamba je ni kweli Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu?

Kama jibu ni ndio basi iwekwe reference ya mstari kutoka kwenye biblia inayo support hayo madai

Kama jibu ni hapana basi iwekwe kifungu kutoka kwenye biblia kinachopinga kuwa mungu hakufanya moyo wa farao uwe mgumu

Sio mmoja anaweka references kutoka kwenye biblia halafu mwingine anakuja kupinga hoja hizo kupitia mawazo yake na mtizamo wake ambao haupo kibiblia.
 
Mi naona farao alionewa tu Mungu ndio mwenye dhambi alafu kama iko mbingu basi farao lazima tumkute sababu yeye ndio aliwafanya waisraeli wamuamini Mungu kwaio asilaumiwe

By the way hivi vitabu walioviandika walijichanganya sana
 
Kuwa na moyo mgumu au moyo laini ni katika free well ya mwanadamu, uhuru wa kuchaguwa na kufanya maamuzi, alicho kifanya
 
Alicho kifanya Farao ni katika Uhuru wa kuchaguwa na kufanya maamuzi free well, maana kukubali au kukataa jambo ni katika uhuru wako wa maamuzi.

Kuwa na moyo mgumu au moyo laini katika kukubali au kupinga jambo flani, yote hayo ni katika maamuzi yako wewe mwenyewe, Mungu hakuishia tu kutupa free well ila akatupa na akili ili tuwe ni wenye kutafakari si (kukariri) ili kwenye maamuzi tuamuwe yaliyokuwa sahihi.
 
hakunaga kitu kinaitwa free will, mimi sikupenda kuzaliwa mweusi tena Tanzania. Free Will iko wapi apo?
Hili sio swala nani wa kumlaumu,Unawajibika na machaguo unayofanya ndio maana ya FREE WILL.You can take or do anything,But once taken it is taken.Ugumu uko wapi?Au hupendi kuwa na Free will?Je ni bora kwako usingekuwepo kabisa?
 
Mkuu haya mambo yana two options,, Either uamini au usiamini..

Ili usipoteze muda inabidi uchague hayo tu
Tatizo ni kwamba, imani haitoagi majibu sahihi.

Wapo waliwaamini wenza wao kuwa hawatasalitiwa ila wakasaritiwa.

wapo walioamini watasaritiwa ila hawakusaritiwa.

imani ni upuuzi.
 
unaweza kuthibitisha mungu yupo? Let alone kumpa vidole vyenye uwezo kutype.
Angalia sana unachoandika, hata hivyo vidole vilivyotumika kutype ujumbe wako ni Mungu amekupa uwezo. Kama huna mchango wa kuchangia nyamaza au pita bila comment. Usije ukapitia magumu zaidi kwa kuamini yaliyoandikwa katika historia ya Mungu na watu wake ni mauzauza. Be humble hata pumzi unayoitumia na mapigo ya moyo wako siyo mauza uza ni uumbaji ambao yupo aliyeumba na huyo ndiye Mungu. Umepata wapi ujasiri wa kusema ni mauzauza mambo yahusuyo Mungu?
 
Back
Top Bottom