Nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MalaikaMweupe, Jul 30, 2009.

 1. M

  MalaikaMweupe Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jana ilitangazwa kuwa 'taasisi ya madawa na chakula' iliiifanya shtukizo la ukaguzi wa vipodozi vya kuongeza na kupunguza maungo ya mwili kariakoo... 'Kazi nzuri! cha ajabu walikwenda na waandishi wa habari na dunia nzima....Tanzania nzima tukajua kulichotendeka.. woga wangu ni kwamba, je maduka yaliyo nje ya Kariakoo, huko Temeke,Tabata,Kijito, Mwenge ,Ilala na upajupo...hawataficha hivyo vipodozi? sasa kweli hii taasisi imesaidia au wanatuziba midomo?:confused:
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Maduka ya huko ulikotaja yatatembelewa kwa wakati wake!

  Kama umeona Operesheni za TRA, huwa zinakuwa hivyohivyo! Wanapita mtaani, na jamaa wote wa eneo hilo huwa wanafunga maduka kuwakwepa, lakini ipo siku wanawatime!, na hakuna njia rahisi sana ya kutumia kwa wateja zaidi ya hiyo.

  Lakini Udhibiti mkubwa ungefanywa kwenye importation ya hizi bdidhaa!
  Pana shida kubwa sana hapo.
   
 3. B

  Bw.Ukoko Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndiyo utendaji wa kazi kwa mashirika ya serikali ya tanzania.Rai hapa ni kwa vyombo vya habari kwani mimi naona shida kuamini kuwa ni lazima vyombo vya habari vipate habari kama hizo baada ya msako hivi wao hawezi kufanya uchunguzi na kutupatia news?afadhari umeongea dar,je kule Kyaka,Ngara,mpanda,srengeti nk nako watabeba lundo la waandishi ni utendaji usio na mashiko.nafikiri tatizo ni kwenye kuagiza,wadhibiti hukohata na wale wanaozityumia na upungufu wa akili,elimu nk
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe hujui mikwara ya kiTz? unajua hali itukuaje? wacha nikupashe ;vipodozi hivyo vitapanda bei ile mbaya na waliozoea na wenye uwezo watanunua na wale wenzangu wataingia mikenge ya machemist uchwara na kununua huko [madhara kesho]. Mifano ipo mingi mbona dawa za kujichubua ambazo zimepigwa marufuku zipo mitaani?
  Hivi tunajiuliza hizi dawa zimeingiaje nchini? jibu ni kuwa kama imezekana pembe za tembo bila TRA kujua rasmi itashindikana vipodozi? Hawa jamaa wanatuzingua tu. Umesahau JK alisema ana majina ya walarushwa TRA? Wa Tz tunafunga geti wakati mwizi kesha ondoka.
   
Loading...