Nisaidieni, Waliokuwa wanaishi katika 1st class za ndege wanaendeleaje

Feb 27, 2016
7
2
Ni miezi zaidi ya mitano sasa tangu maamuzi magumu yaanze kufanyika. Kuna ma-CEO walikuwa wanaishi katika 1st class za ndege na 5 stars hotels kwa pesa za umma. Kila ukipanda ndege, wakati unaelekea kwenye daraja la economy, unawakuta wamekaa wako busy na I-Pad, Laptop, I-Phone na kadhalika, na wala hawakuangalii.

Jamani, nani kakutana nao tena huko angani aeleze kama wanasalimia sasa au hapana.Lakini pamoja na hilo kuna ambao walikuwa wanatumia simu mpaka shilingi milioni 100 kwa mwaka, kisa wameachia simu zao masaa 24 zina-search internet wakiwa nje ya nchi...nao wanaendeleaje?

Na wale mawaziri na makatibu wakuu waliokuwa wanaomba pesa kwa kila shirika lililo chini yao nao wanaendelea au wameacha?
Nipeni update wana-mtandao....
 
Haha aisee Muhongo mwenyewe aligoma kupanda ndege kwenda hapo Egypt kisa sio first class sasa sijui angekua anaenda Australia angeweka mgomo wa kula kwa mwezi mzima ,na hivi wahisani wanazidi kukaba achana na ndege hizo V8 zitabadilishwa watumie Maruti
 
Tunaendelea vizuri...kumbuka tembo hata akikonda vipi hawezi kufikia size ya mbwa
 
Haha aisee Muhongo mwenyewe aligoma kupanda ndege kwenda hapo Egypt kisa sio first class sasa sijui angekua anaenda Australia angeweka mgomo wa kula kwa mwezi mzima ,na hivi wahisani wanazidi kukaba achana na ndege hizo V8 zitabadilishwa watumie Maruti[/QUOTE

Vigogo wa TCRA, EWURA, SUMATRA, TPA, TRA, BOT, NAOT wote sasa naona wanaona safari zanje ni adhabu. Nadhani bado utumiaji kwa fujo simu za mkononi na kutumia magari ya umma kwenda sokoni, shambani, misikitini na makanisani. Kuna mmojawao anatumia mpaka milioni 100 kwa mwaka simu ya mkononi.
 
Back
Top Bottom