Nisaidieni: Wa-tanganyika/tanzania bara wanafaidika nini na muungano??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni: Wa-tanganyika/tanzania bara wanafaidika nini na muungano???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kuti kavu, May 3, 2012.

 1. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Samahani kama nitawakwaza baadhi ya watu. Lakini kutokana na kelele nyiingi ambazo nimekuwa nikizisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu wa-zanzibari kuto utaka muungano kati yao na Tanzania bara nimeguswa kutaka kujua FAIDA AMBAZO WATU WA BARA WANAPATA KWA KUUNGANA NA ZANZIBAR.

  Nimeuliza hivi kwa sababu kelele toka Zanzibar zinaonekana zina picha ya kuwa Zanzibar inanyonywa na WATANGANYIKA kima-slahi. Na ni kama vile wa Zanzibar wanaamini kwa kujitenga na WA TANGANYIKA watakuwa na maisha bora zaidiKwa staili ya kuwa wamejitenga na KUPE MNYONYAJI i.e. TAnzania BARA. lakini kila nikijaribu kuangalia ni namna GANI TANGANYIKA/ Tanzania Bara inafaidika zaidi na huu MUUNGano nakosa JIBU LA MSINGI.

  HIvyo naomba msaada wa kujuzwa ni nini ambacho TANGANyika inafaidika toka Zanzibar ambacho huu muungano ukifa LABDA TANGANYIKA itayumba kwa kukosa HIZO FAIDA husika...
   
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu jibu liko wazi, ni kwamba hakuna cha kupoteza, zaidi sana watanganyika ndiyo tungenufaika kwa kiasi kikubwa kwa kufanya biashara ya uhakika ya mazao, mbogamboga n.k.

  Ushuru wa forodha utakaopatikana kutoka kwa wananchi wa zanzibar watakaokuja kufanya biashara huku utakuwa mkubwa na utaongeza pato la Tanganyika.

  Nyumba za kupanga zitashuka bei sana maeneo ya Tandika, magomeni, temeke tuseme maeneo ya Uswazi kwani wapemba wengi watalazimika kurudi unguja na pemba ili wajipange vizuri kutafuta vibali na viza za kuingia na kuishi nchi ya Tanzania bara(Tanganyika).

  Wageni kutoka Unguja na Pemba waliojenga maghorofa yote yatachukuliwa na shirika la nyumba hivyo kuongeza idadi ya nyumba ambazo serikali inazimiliki.

  Hatari kubwa na hasara nionayo mimi ni kuwa soko la ajira kana kwamba lipo Tanganyika sidhani kuwa kwa udogo wa visiwani na muamumko wa elimu uliopo kwa sasa matokeo yake yataweza kukosha nyoyo za wazanzibar

  Yote ni yote kama wanataka waachwe wachape lapa!!!!:wave:
   
 3. M

  Maliki Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanzia 26/4/1964 zanzibar ilianza kua koloni la TANGANYIKA mpaka leo hii. Kila ifikapo 26/4 kila mwaka ni siku ya HUZUNI KWA WAZANZIBAR kutokana na zanzibar kuwa koloni la TANGANYIKA. Pia, kila ifikapo tarehe 26/4 kila mwaka ni siku ya FURAHA KWA WATANGANYIKA kutokana na kumiliki KOLONI LA ZANZIBAR. Mzanzibar shiriki katika harakati za kudai uhuru wa zanzibar 2012 kutoka mikononi mwa utawala wa kikoloni wa TANGANYIKA. WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO NA TANGANYIKA.
   
 4. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,257
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  mmhh! okkkeey nilikuwa thijui
   
 5. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nionavyo mimi ni kwamba Watanganyika hatutapoteza kitu zaidi zaidi serikali itaongeza mapato hawa jamaa wakirudi kwao Zenji na watakuwa wanalipa kodi wakileta biashara zao huku Tanganyika tofauti na ss hv. Pia tutapunguza mzigo mkubwa wa wakimbizi(Wapemba) waliojazana kila kona huku Tanganyika.

  Muungano ufe tu hata leo hii.
   
 6. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  mh! naogopa tunapoelekea kama tunaanza kuitana wakimbizi ndani ya jamuhuri ya muungano. ni busara kusubiri muungano uondoke ndo tuitane majina tunayoitana
  kwa upande wa faida na hasara sina uhakika lakini najua kuna upande utaumia muungano ukivunjika. kumbuka thamani ya kitu huonekana kinapoondaka
   
 7. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata sisi watanganyika hatuna haja na huo muungano na wazanzibar. Kama kweli ninyi hamtaki muungano mnangoja nini kumwambia Shein awatoe kwenye ukoloni? Uzuri mna bunge lenu ambalo linaweza kuamua mkajitoa kiulani badala ya kukaa mkilalamika kila siku. Kwa kweli na sisi tumeshawachoka sasa!
   
 8. k

  karafuu Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanganyika itaumia sana kuliacha koloni lake la miaka 48,kwani kinachofanyika zanzibar sasa ni hasara kubwa kwa Tanganyika iwapo muungano utavunjika kwasababu mapato yote ya zanzibar ni ya muungano hivyo mabilioni hayo kuyakosa hamuoni kuwa ndio hasara yenyewe? ZANZIBAR KWANZA!
   
 9. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Faida ni za mmoja mmoja,mi mdogo wangu anafanyia kazi hotel ya bwawani so hiyo ndo faida
   
 10. n

  ngaranumbe Senior Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tanzanganyika ndio koloni la zanzibar, kwanza tanganyika haipo duniani, ipo tanzania, tanganyika haina bendera yake wala katiba. Raisi wa zanzibar anapigiwa mizinga kuonesha ni kiongozi wa dola kamili. Tanganyika ilidumu kwa miaka 2 tu baada ya uhuru wake na baada ya hapo ikawa koloni la zanzibar. Tanganyika iko wapi kwenye ramani ya dunia? Wazanzibari wakijitoa kwenye ndoa ya muda hawatahitaji kupeperusha bendera yao tena umoja wa mataifa kwani ipo na ya tanganyia iko makumbusho
   
 11. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pia kwa upande wa michezo TFF ilikuwa inapata mgao wote wa fifa bila kuhusisha zenji. Vilevile TFF itakosa mshiko unaopatikana baada ya wachezaji wa zenji kuuzwa kwenye timu za nje ya nchi.
   
 12. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo falsafa ya umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu haina maana yoyote kwetu wana JF?
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ng'ombe hajui faida ya mkia wake mpaka ukikatika! Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977 sasa hivi Wakenya wanaililia Jumuiya hiyo wakati walikuwa machampioni wa kuivunja! Muungano nao utakapovunjika ndio tutajua tulikuwa tunapata nini na tulikosa nini! Endeleeni na kampeni za kuvunja Muungano!
   
 14. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Hakuna faida yoyote watanganyika wanapata kutokana na muungano. Gharama ya kuendesha serikali mbili ni kubwa mno. Umbumbumbu wa wazenji unawafanya wasitambue kuwa mapato halisi yatokayo upande wao wa muungano hayawezi kugharimia ofisi ya makamu wa raia Zanzibar, achilia mbali ofisi ya rais, wizara zote, watumishi wa umma na huduma za kijamii. EBU NA SISI WA BARA TULIKATAE HILI DUDU TUONE NANI ATAKOMA! TUNABEBA MAJITU HAYABEBEKI KWA NINI TUSIYATOSE? TUNA FAIDA GANI WATANGANYIKA NA MUUNGANO WA NAMNA HII?
   
 15. k

  kichole Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sioni faida yoyote ya muungano, uvunjwe tu.
   
 16. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Kwa kweli naomba kuwa wazi kuwa NAKERWA sana na hizi kelele za WAZANZIBARI kuhusu muungano; na kwa kuwa wa Tanganyika tumekuwa kimya kuhusu hili naona kama tumezidi kuwapa sababu wenzetu wa visiwani kuwamini kuwa LABDA TUNAFAIDIKA SANA NA HUU MUUNGANO!!! nadhani mmeona wenyewe tayari kuna mdau kasema TUNAPATA MABILIONI KUTOKANA NA MUUNGANO HUU!.

  Naona ifikie mahali na sisi waTANGANYIKA tuwaambie kuwa MUUNGANO huu ulikuwa wa hiari na kama wanataka kuuvunja WAUVUNJE!!!...sidhani kama ZANZIBAR wna BIDHAA yeyote adimu ambayo TANGANYIKA HAIWEZI KUISHI BILA KWAYO. SIo kwamba napigania muungano uvunjike lakini KAMA TULIO UNGANA NAO HAWATAKI TENA KUWA NA SISI NINI SABABU YA KUWALAZIMISHA???...kama vipi WAENDE ILI ITUPE MUDA WA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO NYINGINE ZA MSINGI KULIKO KUPOTEZA MUDA KUFANYA VIKAO NA MIDAHALO NA WATU WASIOTUPENDA WALA WASIOTHAMINI MCHANGO WETU KATIKA UWEPO WAO!!!
   
 17. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Utalii wa Luxury Beach Resorts walizojenga wawekezaji ndio jueri ya Zanzibar, Dar bado wamelala kwa hilo, Mainland ina nafasi kubwa na nzuri zaidi kwa hilo kama wataruhusu ujenzi katika viziwa kama Mbudya au Bongoyo (inviromentaly friendly) Dar ina Airport kubwa na ni muhimu kwani midege ya Private Charter companies ingejaza mafuta hapahapa badala ya kwenda Mombasa kama kwa case ya Zanzibar
   
 18. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Zanzibar ni koloni la nchi gani? Hiyo Tanganyika inayowamiliki iko wapi? Nani raisi wake? Uko wapi wimbo wake wa taifa? Liko wapi bunge lake? Iko wapi bendera yake?
  Tumia na akili kidogo unapoandika mambo yako. Watanganyika tumewachoka Wapemba na kelele zenu za kibaguzi. Endelezeni harakati zenu ili Tanganyika yetu ifufuke.
   
 19. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba wazanzibari wangeacha kulalamikia wananchi wa Tanganyika maana hatuhusiki na matatizo yanayotokea ila wangelalamikia viongozi na wapelekeeni hizo lawama wao ndio wahusika:help:.

  Bring back New Tanganyika with big change!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. M

  Musia Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  strange!
   
Loading...