Nisaidieni ushauri wa kumpa huyu rafiki yangu

clefting

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
222
389
Salaam,

Kuna rafiki yangu tangu wa toka utotoni lakin tulikuja kutengengana katika harakati za kutafuta maisha na hatujawasiliana kama mwaka hivi umepita.

Sasa jana kanicheki WhatsApp akanitumia picha ya kidonge akaniambia amevikuta kwenye mkoba wa demu wake, kutokana wasiwasi wa hivyo vidonge akaamua ku-google ARV akaona vinafanana, akaamua kunicheki maana mimi ni mtaalamu wa hayo mambo.

Mimi kukicheki ni ARVs (TLD) yenyewe. Akanipigia simu nikaongea naye ikabidi nimdanganye kwamba sio zenyewe hii imekuja baada ya kuwa kapanic sana, ananiambia hajalala usiku anawaza tu. Na kwa hali aliyokuwa nayo counseling kwenye simu isingeleta matokeo chanya.

Sasa apa nawaza nimwambie tu ukweli au niache.

Samahani, positive comments zitafaa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa we ukaona kumdanganya kuwa sio zenyewe ndio counceling nzuri au?

Nadhani ka we uko mbali naye mwambie atoe hapo kimoja apeleke kwa daktari ili amsaidie. Kumuacha aendelee kungonoka kizembe sidhani ni kumsaidia.
 
Huyo demu kimeo kaishaungua! Mwambie ukweli rafiki yako! Hila kuna wale wa kuwahi kabla ya Masaa 72 tangu unapohisi umeambukizwa! Anaweza anajihami kuambukizwa! Lakini pia uenda abafubaza! Mwambie mshikaji amuulize huyo demu kati hizo hali mbili
 
Ongea nae mshkaji wako vzr,
lakini mkumbushe kuwa kwa mtumiaji mzuri wa ARV hawezi kuambukiza kirusi kwa mwenzie (because of low viral load), hivyo asiwe na shaka ila aongee na mpenzie vzr ili ajue matumizi yake ya dawa kama anatumia kwa usahihi na maendeleo yake ya clinic.

Kisha aende kituo cha afya kuchek afya yake, nina uhakika kuwa, kama mpenzi wake anatumia dawa kwa usahihi, basi mwana hatakua na virusi vya ukimwi,

Mshauri vzr ili hata akijikuta ameshaathirika aweze kukubaliana na hali na maisha yakaendelea, muunganishe na washauri wengine wazuri kama unaona hutaweza kutoa counceling nzuri. clefting

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ongea nae mshkaji wako vzr,
lakini mkumbushe kuwa kwa mtumiaji mzuri wa ARV hawezi kuambukiza kirusi kwa mwenzie (because of low viral load), hivyo asiwe na shaka ila aongee na mpenzie vzr ili ajue matumizi yake ya dawa kama anatumia kwa usahihi na maendeleo yake ya clinic.

kisha aende kituo cha afya kuchek afya yake, nina uhakika kuwa, kama mpenzi wake anatumia dawa kwa usahihi, basi mwana hatakua na virusi vya ukimwi,

mshauri vzr ili hata akijikuta ameshaathirika aweze kukubaliana na hali na maisha yakaendelea, muunganishe na washauri wengine wazuri kama unaona hutaweza kutoa counceling nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie tu ukweli, km upo nae mkoa mmoja bs mfuate kbs ili umuambie kwa usahihi zaidi....ila dah awa watu wasiowaambia wapenz wao kwamba hali gani wanazo , wanakatisha tamaa sn.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam,

Kuna rafiki yangu tangu wa toka utotoni lakin tulikuja kutengengana katika harakati za kutafuta maisha na hatujawasiliana kama mwaka hivi umepita.

Sasa jana kanicheki WhatsApp akanitumia picha ya kidonge akaniambia amevikuta kwenye mkoba wa demu wake, kutokana wasiwasi wa hivyo vidonge akaamua ku-google ARV akaona vinafanana, akaamua kunicheki maana mimi ni mtaalamu wa hayo mambo.

Mimi kukicheki ni ARVs (TLD) yenyewe. Akanipigia simu nikaongea naye ikabidi nimdanganye kwamba sio zenyewe hii imekuja baada ya kuwa kapanic sana, ananiambia hajalala usiku anawaza tu. Na kwa hali aliyokuwa nayo counseling kwenye simu isingeleta matokeo chanya.

Sasa apa nawaza nimwambie tu ukweli au niache.

Samahani, positive comments zitafaa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwambie ukwel mkalishe chini kwa ustadi mkubwa wa afya ulio nao mueleze ukimficha badae akijua atakuchukia sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom