Nisaidieni, upendo unapungua kwa mume wangu

Huyo mumeo nahisi anatumia swala LA kufiwa na wazazi wake kama excuse tu..ila nahis kuna mambo kati ya haya
1) Ana asili ya uchoyo/ ni tabia yake
2)Alishawahi kumpenda mdada, lakini akaishiwa kuchunwa pesa nyingi na papuchi hakupata..so maumivu ya kupendewa pesa na kuchunwa bado anayo miss_mbeya
Uchoyo nimeona hata dada zake wako hivo nafikiri ni trait ya kuridhi
 
Hyo hata kama n utoto umezid utadhan ndo wa kwanza kufiwa na vip akiwa na kisiran ndo watchful
Ashanti
1.anza kumpotezea,akiwa na kisiran jifanye kama vile hujal,akae na kisiran chake kiishe kisiishe Altamont
2.kuwa mwanamke sasa mahitaj ambayo hayakuhusu mfano umeme,kodi au ada na hata chakula usiyafanye kama umeme ukiisha mlale giza,hajaacha hela ya chakula pika chako kula lala kiufup asikute Chaka
Kataa kupigwa kisiran chake apeleke kwa boss wake kama n mzur wa ngum akapigane na wenzake mpe warning kwamba siku akikupiga hata kofi ataenda kujieleza polish
4 punguza ikiwezekana acha kabisa kumletea zawad hzo ambazo huwa unamletea instead jinunulie zawad unayoipenda,ukiweza siku za weekend toka out na mwanao ye hata usimuulze kiufup mpotezee utaona mabadiliko anaeza akahis unachepuka narudia yaan jifanye kama husikii anayoyaongea
Amen dear nashukuru kwa ushauri
 
Mamiii unajua huduma ya anointed room??? Em ngoja nikushirikishe hili.... Hakuna linalomshinda Mungu.... Ingia insta au fb search anointed room au nenda u tube search uone masomo yao naamini yatakujenga... Na Kama utaweza jiunge na prayer marathon ukienda hizo pages nilizokuelekeza utapata maelekezo..... Kama hujaelewa Ni pm ntakuelewesha zaidi.... Sio kitu Cha kulipia hela kwamba utatapeliwa noo dear ingie huko then thank me latet
Ahsante dear
 
Wapendwa poleni na majukumu ya kujenga taifa.Niende kwenye hoja yangu ,Mimi ni mdada/mama mwenye mtoto 1,nimeolewa na ndoa ya kanisani .Mume wangu alifiwa na wazazi wote wawili kitambo sana,sasa upendo kwangu haupo najitahidi sana nimletee vizawadi nikitoka kazini,amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa yeye upendo wake ulishaondoka na wazazi wake ,kiujumla anasema wazazi wake wangekuwepo angeishi maisha ya furaha sana,eti anaona maisha yote ni ubatili.kuna siku moja alinambia anashangaa wanaume wanaowanunulia wake zao nguo au kuwasomesha watakuwa wapumbafu na wajinga,anajali zaidi mtoto wake ,kwakweli ni mtu wa hasira nikikosea kidogo ni kipigo na akiongea kugomba nanyamaza kimya,but yeye anafanya makosa makubwa namsamehe ,kwasababu ukimwambia kwa kumshauri anakuja juu.Pili ni mbinafsi sana kiasi inapelekea uchoyo wa hali ya juu.Nasema hivi nilivoolewa mimi nilikuwa nawasaidia ndugu zake,niliwachukulia km ndugu zangu but nikaona mwenzangu kwetu hajali babaangu mzazi alilazwa wiki mbili nilikuwa natuma hela,yeye hata senti tano kwamba anisupport hata kupiga cm kumjulia hali mgonjwa hakuweza ,nilivolalamika akanambia nichukulie jinsi nilivo univumilie ndivo nilivo.Ila nami nachoka ,yeye ni mwajiriwa ana kipato kikubwa zaidi yang.Nisaidieni kwa mawazo naona maisha ya ndoa magumu sana
Angalia usiwe kama MAMA DAVIS wa cocochanel na Naipenda Jumatano Yangu yake. Nakuhurumia maana Mama Karisa anakaribia kukutafutia Fadhili akufadhili. Ndiyo akufadhili Ub.oo, Mahaba na Fwedha.

Nimesema!
Bazazi
 
Angalia kuna uwezekano amekosa imani na wewe labda ulimsaliti au kuna viashiria vya usaliti au labda wewe ni kiburi ama ulionesha dharau na kutomuheshimu. Kama kipo kimojawapo wanaume tunapoteza upendo kwa mwanamke
Hapana kiufupi hata baadhi ya baba zake wakubwa kwa wadogo wana hizo tabia,watatu walishaachana na wake zao wa mwanzo ,mmoja nilimkuta wakati naolewa alinisimulia mengi sana akasema ukoo wao yaani wa mume wake ( ambae mimi ni baba mkwe wangu mdogo) akasema wana roho ya kikatili baba yake alishamuuaga mke wake wa kwanza kwa kumpiga na kamche ka kutwangia karanga yaani yaani babu
 
Angalia usiwe kama MAMA DAVIS wa cocochanel na Naipenda Jumatano Yangu yake. Nakuhurumia maana Mama Karisa anakaribia kukutafutia Fadhili akufadhili. Ndiyo akufadhili Ub.oo, Mahaba na Fwedha.

Nimesema!
Bazazi

Ngoja nimpatie link akasome ushauri wa Tilda anaompa mama Davis


Nimesoma post yake moja miss_mbeya anajitetea hadi kutumia mifano ya ndugu ambao yao ni yao na yake yaweza kuwa tofauti nao kabisa. Aibu sana mwanamke kuishi kukaribisha au kusala udaku kwa kukaribisha nguvu za giza mwenyewe.. huyu hajitambui kwa sasa.. anaweka watu mbele na labda mchepuko kuliko yeye na mwenza na mtoto na furaha yao..
 
Ngoja nimpatie link akasome ushauri wa Tilda anaompa mama Davis


Nimesoma post yake moja miss_mbeya anajitetea hadi kutumia mifano ya ndugu ambao yao ni yao na yake yaweza kuwa tofauti nao kabisa. Aibu sana mwanamke kuishi kukaribisha au kusala udaku kwa kukaribisha nguvu za giza mwenyewe.. huyu hajitambui kwa sasa.. anaweka watu mbele na labda mchepuko kuliko yeye na mwenza na mtoto na furaha yao..
Ahsante mpenzi nitaifuatilia uweenda inaweza nisaidia kwa kiasi fulani
 
Ahsante mpenzi nitaifuatilia uweenda inaweza nisaidia kwa kiasi fulani

Tutag kutupa mrejesho.
Kila la kheri.. muhimu hapo ulipo acha kufikiria hao hao wasio wewe na mumeo.. anza kutulia na kuongea na kuomba na Mwenyezi Mungu.
Usikimbilie kwa watu.. tulia endelea n.k.
 
Kwa hatua ya kwanza mshirikishe ndugu yake wa karibu ajaribu kumuelimisha kuhusu anayofanya lkn pia yaweza kuwa ana mchepuko ambao akili nyingi amewekeza kwake kitu kinachomfanya akuone ww si kitu zaidi ya mwanaye,ikishindikana km ndio na kipigo juu asije akakudhuru mwisho ukashindwa hata kulea wanao chukua hatua mapema

Issue nyingine umesema ww ni mama kijacho huenda hiyo hali yako pia imesababisha msipendane subiri kwanza ujifungue maana ujauzito muda mwingine unakuja na changamoto zake
 
Nashukuru dear kwa ushauri ingawa ni mama kijacho ,yaani kazini walikataa kunilipia masomo ya master ,ada ilikuwa milioni kama milioni kumi na tano hivi pamoja na research nililipa kama milioni 13,000,000 hivi sasa ikabaki milioni 3 nikamwomba akakataa kunipa ikabidi nikamkopa coz bank nilikuwa najua ana sh.ngapi akanipa baada ya miezi 3 alikuwa ananidai mpaka nikitoka kazini nakosa raha ya kurudi Nyumbani ,ikabidi niingie bank nikope nimrudishie ndo tukawa na amani but roho inaniuma coz kaenda kuweka bank,
Daah mumeo mbinafsi sana miss, lakini haya yote hukuyajua kipindi cha uchumba?
 
No kipindi tupo uchumba hakuwa anaonyesha hizo tabia,tulipofunga ndoa baada ya miezi kadhaa ndo nikawa nashangaa baadhi ya tabia ,mfano anaweza kufunga samaki mzima sato kama kulikuwa na kifunction kazini ,but akija nampashia kwa oven anakula pekee yake anamaliza namwangalia ,
 
mama kwani umepigiliwa misumali hapo.?
ndoa ya mateso sio ndoa. Usisikilize Yale maneno wazee wamevumilia mengi.
Atakuua huyo
 
No kipindi tupo uchumba hakuwa anaonyesha hizo tabia,tulipofunga ndoa baada ya miezi kadhaa ndo nikawa nashangaa baadhi ya tabia ,mfano anaweza kufunga samaki mzima sato kama kulikuwa na kifunction kazini ,but akija nampashia kwa oven anakula pekee yake anamaliza namwangalia ,
Aisee sina nia mbaya ila tu kwa ustawi wako wa akili na afya ningependa tu ikibidi umteme tu huyo jamaa kama unajimudu.
Kwa stage iliofikia huyo jamaa hashindwi kukacha kulipia drip au dawa when you reach a state of emergency.
 
Pole kwa mkasa unaokusibu katika maisha always kuna pande mbili kama ilivyoshilingi. Na kama ni mumeo na mlifunga ndoa kanisani kuna haja ya kumlilia bwana, jaribu kuomba ushauri hata kene mabaraza ya watu wazma, ikiwemo hata watamushi wa kiroho, hyo grieving period ya kuhusu wazaz wake yawezekana ni kifungo alichonacho na inahitaji msaada wa kiroho au wakisaikolojia kwamana sio normal situation as it is. Wana JF weng wanasema either uondoke that is not a solution ulishajenga mji huwez kuukimbia kisa umeona panya ndani ya nyumba yamkini utaondoka hapo utaenda kwingine ambako mwanaume harud hata nyumban. Hio ndo mitihani ya ndoa na changamoto zake eb ona umekutana na kashkash lakin still umebeba mimba nyingine that means there is a happy hour too. Uvumilivu, sala, ibada, utii ndo mkombozi wako n never the less.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom