miss_mbeya
JF-Expert Member
- Mar 24, 2015
- 1,073
- 1,021
Wapendwa poleni na majukumu ya kujenga taifa.Niende kwenye hoja yangu ,Mimi ni mdada/mama mwenye mtoto 1,nimeolewa na ndoa ya kanisani
Mume wangu alifiwa na wazazi wote wawili kitambo sana,sasa upendo kwangu haupo najitahidi sana nimletee vizawadi nikitoka kazini,amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa yeye upendo wake ulishaondoka na wazazi wake ,kiujumla anasema wazazi wake wangekuwepo angeishi maisha ya furaha sana,eti anaona maisha yote ni ubatili.
Kuna siku moja alinambia anashangaa wanaume wanaowanunulia wake zao nguo au kuwasomesha watakuwa wapumbafu na wajinga,anajali zaidi mtoto wake ,kwakweli ni mtu wa hasira nikikosea kidogo ni kipigo na akiongea kugomba nanyamaza kimya,but yeye anafanya makosa makubwa namsamehe ,kwasababu ukimwambia kwa kumshauri anakuja juu.
Pili ni mbinafsi sana kiasi inapelekea uchoyo wa hali ya juu.Nasema hivi nilivoolewa mimi nilikuwa nawasaidia ndugu zake,niliwachukulia km ndugu zangu but nikaona mwenzangu kwetu hajali babaangu mzazi alilazwa wiki mbili nilikuwa natuma hela,yeye hata senti tano kwamba anisupport hata kupiga cm kumjulia hali mgonjwa hakuweza ,nilivolalamika akanambia nichukulie jinsi nilivo univumilie ndivo nilivo.
Ila nami nachoka ,yeye ni mwajiriwa ana kipato kikubwa zaidi yang.Nisaidieni kwa mawazo naona maisha ya ndoa magumu sana.