Nisaidieni swali hili kuhusu Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi

Huyu ndie rais alieliingiza gari la maendeleo na nidhamu ya maadili ya watanzania porini. Huyu anaharibu misingi yt bora. Nashangaa watanzania hta hatukumbuki.
mwehu kweli wewe..nidham mkose wenyewe usingizie MTU!..hebu thibitisha madai yako
 
Naombeni mnisaide swali lifuatalo.
J.K.Nyerere anatoka Butiama, Mara.
B.W.Mkapa anatoka Mtwara.
J.M.Kikwete anatoka Msoga, Pwani.
J.P. Magufuli anatoka Chato, Geita.

Je Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ndugu Ali Hassan Mwinyi ni mwenyeji wa mkoa gani?
Kijiji cha Sotele Wilaya ya Mkuranga/Pwani, wakati huo ilikuwa Wilaya ya Kisarawe
 


By Idd Hamis ,Mwananchi
Huwezi kusikiliza lolote kuhusu kampeni za uchaguzi Tanzania bila kulisikia jina la Mwalimu Julius Nyerere likitajwa kwa kunukuliwa alichokisema. Kila upande, uwe ni upinzani au Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea akitaka kutia uzito maneno yake, atamnukuu Mwalimu Nyerere.


CCM kinampinga mgombea wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa kwa kusema; “hata Mwalimu alimkataa Lowassa mwaka 1985”. Lowassa naye anajibu mapigo kwa kusema; “Hata Mwalimu alisema wananchi wakiyakosa mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM”.
Kwa maneno mengine, Mwalimu Nyerere haepukiki katika siasa za Tanzania hasa wakati wa uchaguzi. Kauli zake ni mtaji mzuri wa kisiasa kwa yeyote yule awe chama cha upinzani au chama tawala. Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuangalia uhusiano wa Mwalimu Nyerere na uchaguzi Tanzania.

Mwalimu katajwa kwa mengi lakini kuna moja ambalo Mwalimu Nyerere halitajwi ni lile la kutaka kuwaamulia Watanzania nani awe rais wa Tanzania. Hili ndilo linaloipa tabu wanaCCM kuona haiwezekani chama kingine kushika madaraka badala yao.
Katika makala iitwayo: “Great leaders groom heirs and relinquish power,” mtunzi, Peter Mutua anasema kwamba viongozi wakubwa huandaa warithi wao kisha huachia madaraka.

Mwalimu na kuachiana madaraka

Mwaka 1985 wakati Mwalimu anang’atuka, kama alivyosema Peter Mutua kuwa watu mashuhuri huandaa warithi wao kabla ya kuachia madaraka, na yeye alijaribu kumrithisha uongozi wa Tanzania mtu wake ambaye alikuwa ni balozi Salim Ahmed Salim.

Kwa bahati mbaya ingawa Mwalimu alikuwa na nguvu kubwa katika CCM, mtu wake huyo hakukubaliwa hasa na Wazanzibari. Baada ya Mwalimu kuona hali hiyo, Balozi Getrude Mongella akatoa wazo kwa kumwambia: ‘‘Mwalimu kwa nini usimjaribu Makamu Ali Hassan Mwinyi?”.

Mwalimu hakuwa kama viongozi wa sasa wa CCM ambao hawasikilizi watu wanasema nini. Zaidi ya mara moja aliwaambia CCM katika kutafuta kiongozi chama lazima kisikilize watu wanasema nini. Mwalimu alisikiliza maoni hayo na kilichotokea hivi sasa ni historia.

Mzee Mwinyi akawa Rais wa Tanzania kumrithi Mwalimu ingawa hakuwa chaguo lake. Kwa kufanya hivyo, Mwalimu Nyerere akaweka utaratibu wa kiongozi aliye madarakani kutaka kurithisha mtu anayemtaka yeye badala ya kuwaachia wananchi kumchagua wamtakaye.

Mwalimu na uchaguzi 1995

Miaka 10 baada ya Mwalimu kung’atuka madarakani, muda wa urais wa Mzee Mwinyi ukawa umemalizika kikatiba.

Katika kutafuta nani atamrithi Mzee Mwinyi, wanaCCM kadhaa wakajitokeza wakiwamo John Samuel Malecela, Jakaya Mrisho Kikwete na hata Edward Lowassa anayegombea urais kupitia tiketi ya Chadema mwaka huu.

Mwalimu aliwapinga wote hao na kwa John Malecela alifikia kusema; “Kama jina la John lipo basi mimi narudisha kadi ya chama”. Si mahali pake kueleza sababu kwa nini hakumtaka Malecela lakini jambo la muhimu ni kwamba kwa mara nyingine tunamuona tena mwalimu akitaka kumrithisha mtu aliyeona yeye anafaa.

Walipobaki Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, Mwalimu alimwambia Kikwete kuwa wakati wake bado. Hapa Mwalimu alipuuza mawazo ya watu kwani aligundua kwa kusikiliza watu asingeweza kumpata yule anayeona anafaa kuiongoza Tanzania baada ya Mzee Mwinyi.

Mwalimu alimuona Benjamin Mkapa kuwa ndiye anayefaa kuwa rais baada ya Mwinyi. Kwa kuwa alitaka kumuweka ‘mtu wake’, ilibidi Mwalimu ainuke mwenyewe kumnadi Mkapa nchi nzima. Mkapa akashinda na CCM ikabaki madarakani.

Mwalimu alifariki mwaka 1999 akiwa amewaachia Watanzania utamaduni wa rais aliyeko madarakani kuona ni haki yake kumrithisha ‘mtu wake’ madaraka. Utamaduni ambao ukifuatwa unaonekana kuwa na madhara kwa CCM na hata Taifa .
Mwaka 2005, Benjamin Mkapa alijaribu kufanya kile alichokifanya Mwalimu, kumrithisha ‘mtu wake’ madaraka. Mkapa hakuwa na nguvu na ushawishi kama Mwalimu Nyerere hivyo ilibidi asalimu amri kwa kundi lililojulikana kama wanamtandao, kundi ambalo lilikuwa na Jakaya Kikwete na Edward Lowassa.
Tukumbuke kuwa mwaka 1995, Mwalimu Nyerere alimwambia Kikwete muda wako bado. Kauli hiyo ilikuwa na maana Kikwete anafaa kuwa rais lakini zamu yake ilikuwa tu haijafika.

Kwa maneno mengine, mwaka 2005 hata akiwa kaburini Mwalimu Nyerere aliamua nani awe mgombea wa CCM kwani kwa kumkubali Kikwete wakati wa uhai wake, ilikuwa ni sawa na kumkubali akiwa kaburini.

Mwaka huu, athari ya Mwalimu Nyerere katika uchaguzi huu imebakia katika nukuu ya maneno yake. Mwalimu amesababisha Lowassa kukataliwa na CCM kwa madai kuwa “hata Mwalimu alimkataa”.

Kwa vyovyote vile, Watanzania wanapokumbuka miaka 16 ya kifo cha Mwalimu Nyerere athari yake katika uchaguzi haiepukiki iwe ni kwa wema au ubaya, kwa CCM au vyama vya upinzani. Lililo baya ni ule utamaduni wa rais aliyeko madarakani kutaka kumrithisha madaraka anayemtaka.

Hili iwapo halitoachwa, litasababisha nchi kuja kuingia katika machafuko. Kama watu wananukuu Mwalimu Nyerere alisema “katika kutafuta wagombea chama lazima kisikilize watu”, tujiulize ni chama gani cha siasa Tanzania kinasikiliza watu katika kuwapata wagombea wake?

Fikiria kile kilichotokea CCM mwaka huu; je, mgombea aliyepo alitokana na sauti ya watu? Matokeo yake ni huu mpasuko tunaoushuhudia katika CCM kwa kuhamwa na makada wake waandamizi akiwamo mmoja wa waasisi wake, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru. Hatujui ni nani atafuatia lakini haya ni madhara ya jaribio la Mwalimu kutaka kumrithisha mtu wake uongozi.

Muda mfupi kabla ya uteuzi wa mgombea wa CCM, rais Mstaafu Benjamin Mkapa alinukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akisema kuwa chama hakiwezi kwenda kinyume na matarajio ya watu kuhusu uteuzi wa wagombea kwa ajili ya urais. Kauli hiyo ni kamba Mkapa anakumbuka wosia wa Mwalimu usemao: “Katika kuwapata wagombea, lazima chama kisikilize watu wanasema nini”.

Lowassa aliijua kauli hiyo ya mwalimu kwa hiyo akapiga kampeni na kujipanga ili chama kisikie watu wanasema nini. Kitu ambacho alikisahau ni ile kanuni kwamba kiongozi hupenda kuachia madaraka kwa mtu ambaye alimwandaa. Bahati mbaya mtu huyo hakuwa yeye Edward Lowassa.

dinyampuntaz@yahoo.com
Umejibu kitu ambacho hujaulizwa!
 
Naombeni mnisaide swali lifuatalo.
J.K.Nyerere anatoka Butiama, Mara.
B.W.Mkapa anatoka Mtwara.
J.M.Kikwete anatoka Msoga, Pwani.
J.P. Magufuli anatoka Chato, Geita.

Je Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ndugu Ali Hassan Mwinyi ni mwenyeji wa mkoa gani?
Kama anapotoka mtu ni alipozaliwa/ kwenye asili ya wazazi wake, Alhaji Ali Hassan Mwinyi ni mwenyeji wa Wilaya ya Kisarawe (sasa Mkuranga).

Ali Hassan Mwinyi - Wikipedia
 
Naombeni mnisaide swali lifuatalo.
J.K.Nyerere anatoka Butiama, Mara.
B.W.Mkapa anatoka Mtwara.
J.M.Kikwete anatoka Msoga, Pwani.
J.P. Magufuli anatoka Chato, Geita.

Je Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ndugu Ali Hassan Mwinyi ni mwenyeji wa mkoa gani?
Ukijua anakotoka itakusaidia nini?

Pambana na hali yako
 
Huyu ndie rais alieliingiza gari la maendeleo na nidhamu ya maadili ya watanzania porini. Huyu anaharibu misingi yt bora. Nashangaa watanzania hta hatukumbuki.

unaonekana umezaliwa mwaka kuanzia 2000, unayajua maisha tuliyokuwa tuishi enzi za nyerere, hakuna tv ukiwa na tv wewe ni jela moja kwa moja hakuna sabuni za kuoga hakuna sabuni ya kufulia hakuna sukari hakuna kununua redio bila kibali viatu raba tulikuwa tunawaona wakenya tu wakivaa unga wa yanga mchungu resheni ya chakula kununua mweyekiti ndio anawapeni kwa wiki mnajipanga foleni trc kila kaya kilo ya sukari na dawa moja ya meno magari peugeut tu za kizamani kitaifishwa mali za watu majumba za watu kupewa NHC alipoingia mwinyi siku hiyo hiyo akasema Ruhsa kuleta kila kitu nunueni tv na magari naleteni chochote kutoka RUHSA ndio akaitwa mzee ruhsa hapo ndio watanzania wakazaliwa upya na kuona maisha mazuri,kenge wewe una sema mzee mwinyi sijui kafanyaje hujui chochote
 
Back
Top Bottom