Nisaidieni niokoe maisha ya kijana huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni niokoe maisha ya kijana huyu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by elimumali, Jan 20, 2010.

 1. elimumali

  elimumali Senior Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nina mtoto wa jamaa yangu wa karibu anatumia madawa ya kulevya muda mrefu – miaka kumi sasa. Katika kipindi chote hicho, Mzazi wake (Mama) kamsumbukia sana kupata suluhu ya kumfanya aache madawa mpaka sasa hajafanikiwa. Kusumbuka huko ni pamoja na matibabu (detoxification), Maombi mbali mbali, Ushauri nasaha (councilling), nk. Athari zake zimekuwa kubwa, anajidunga sindano na mishipa yake sasa imekuwa tabu kupatikana. Alishapelekwa Lutindi (Korogwe) ambako ndiko panaaminika kuwasaidia vijana hawa mara tatu, lakini bado. Yeye mwenyewe anaonyesha nia ya kuacha, lakini anasema mwili unamuuma sana anapojaribu kuacha. Wanafamilia walimshauri kuwa suluhu ni kumpeleka Rehabilitation Centre inayoaminika kwa muda mrefu akae huko. Hapa Tanzania Rehabilitation Centre inayoweza kuwadhibiti na kuwatibu vatu hawa iko papi? Naomba ndugu wapendwa anayejua anielekeze nimsaidie ndugu yangu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Be patient, kuna watu humu kibao watakusaidia...Thats all i can say.
  Jaribu kueleza vizuri wewe uko wapi.
   
 3. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Muhimbili
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  pole sana
   
 5. M

  Mzee wa Kale Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Tanzania Rehab ya uhakika sijui iko wapi, najua Kenya ipo Rehabilitation Centre, Malindi inaitwa The Omari Project hawa jamaa ni wajuzi sana wa mambo haya, kwa Tanzania utapelekwa kwenye jela za Vichaa tu, hatuna Rehabitation ya uhakika kwa watumiaji wa madawa ya kulevya, si kushauri umpeleke mental hospital kwa kuwa hizo ni kesi tofauti.

  Maumivu ni lazima, cha msingi anatakiwa apate ushauri ili yeye muhusika mwenyewe ajione kama analo tatizo linalomsumbua, na nyinyi wengine muweze kusaidia tu, mara nyingi matatizo kama hayo jamii inayomzunguka mteja wao ndio wanaliona tatizo na wakataka walitatue badala ya mteja mwenyewe kujiona analo tatizo hivyo nawapa pole lakini pia naomba muwe makini sana, kwa hatua za kwnza ni lazima mjitahidi mteja mumsaidie alione tatizo lake.
   
 6. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilishawahi kusikia hiyo ya Mombasa, kwa pamoja tufanye utafiti kuhusu hicho kituo maana hilo sio tatizo lako peke yako,,ni letu sote kama jamii..
  Pole sana
   
 7. elimumali

  elimumali Senior Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mzee wa kale asante sana kwa ushauri. Hii ni issue inayohitaji sana ushauri na matibabu kwani hata anayemlea huyu kijana (mama yake) anaathirika kiakili na kiafya kutokana na sononeko alilo nalo la kumuona mwanae anaangamia bila kujua afanye nini, na ni mwanae wa kiume wa pekee. Kweli anatia huruma, hatujui tusaidieje. Mfuko ungekuwa unaruhusu angeweza kupelekwa Rehabilitation Centre za nje, lakini hela itoke wapi, kila mtu kafulia.
   
 8. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu elimumali I can understand the pain maana pia mimi nina rafiki yangu ana experience the same kwa mdogo wake, Huyu kashapelekwa Rehab mara kadhaa akirudi anakaa mwezi tu anarudi kulekule kiasi kwamba familia imemtengea bajeti yake ya siku kwa ajili ya kumnunulia hizo kete maana asipopata anapata hali mbaya ya kukaribia mauti.

  Kituo cha Mombasa kinasifika kwa kutoa hayo matibabu lakini pia kiko kingine Nairobi ( Hope and Freedom Treatment Centre) jaribu hapo kunaweza kumtoa ndugu huyu kwenye hili tatizo.. Yote haya yanaanza wakati vijana wakianza kujifunza kuvuta bangi wakizoea wanahamia kwenye cocktail (Bangi na mchanganyiko wa unga) baada ya hapo ni kujidunga ndio kunakobakia.
   
 9. elimumali

  elimumali Senior Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu wa kwetu ametengewa bajeti ya 10,000 kwa siku, asipopewa anachukua chochote kinachoweza kuuzika hapo nyumbani. Inabidi kila kitu kiwe kinafungiwa makabatini, sitting room imekaa kama watu wamehama, vyombo vinafichwa vyumbani. Maisha haya maisha gani. Jamani tumlilie nani Tanzania ili tupate Rehabilitation itakayowasaidia vijana hawa kwa bei nafuu? Ukitoka tu nje ya Tz ni gharama tusiyoweza kuimudu. Vijana ndio Taifa la kesho, tumwambie nani aanzishe kitu cha kuwaokoe vijana hawa waliokwisha athirika? Ambao bado hawajaathirika nina imani wanapata mafunzo tosha, yapo sehemu mbali mbali. Lakini tiba ya uhakika ndio bado.
   
 10. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  pole sana ndg
  naamini atapata tu matibabu samuwhere
   
 11. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,746
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  njia bora zaidi ni kumuweka mbali na mazingira yanayochochea madawa... hata akitibiwa wapi anaweza akarudia kama vishawishi bado vitakuwepo
   
 12. elimumali

  elimumali Senior Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Inshallah!
   
 13. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu huyo keshafikia hatua ya kwamba si vishawishi ndio vinamlazimisha kutafuta hayo madawa bali ni addiction ambayo iko controlled na ubongo zaidi ya vitu halisi. Huyo hata ukimfungia ndani anaweza vunja mlango ilimradi tu akapate dozi.. Anatakiwa kupewa tiba ya kisaikolojia zaidi kuliko ile ya mazingira.
   
 14. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Inauma sana pale unapoju akuwa yale mazungu ya unga yenyewe yako vizuri yanakula maisha na kuendesha ma-vogue!! wakati watoto wa masikini wanateketea. Hivi kwa nini hii sheria ya madawa ya kulevya isiongezewe makali mtu akikamatwa na dawa za kulevya anyongwe pale jangwani kwenye viwanja vya wazi vile..huenda amani itakuwepo. I can understand tabu mnayokumbana nayo mazee. Pole bana... Nadhani china wananyonga sijui kama hata kuna mateja kule!!
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  pole sana ila sumu ya teja jela mjaribuni hiyo kama zote zimeshindikana
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni vyema akaonyeshwa mapenzi na acceptance na all family members au watu wake wa karibu ili aweze jisaidia na kupata imani ya kuwa yuko na watu wenye nia ya kumuokoa kama ni tatizo la miaka michache ni rahisi. lakini kama ni la muda kama mna family member else where outside ya mazingira ni bora ahamishiwe huko its much to do with coping and facing reality ndio sababu wateja wengi hu-relapse after detox, having to face life and obligations is hard kwao psychologically any problem kwake ujue suluhisho ni hilo tu litakua.
   
 17. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivyo vitu huko jela vinaingizwa!!!
   
 18. elimumali

  elimumali Senior Member

  #18
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  My dear, huyu kijana alipelekwa Arabuni kwa jamaa yetu ili akatulie huko na kufundishwa dini, tena baada ya kupata VISA ukoo wote tulifurahi kuwa sasa amepona. Siku hiyo hiyo aliyofika, usiku akatoweka baada ya arosto kumshika akaenda chemist kutafuta cha kumsaidia, wenyeji walipoona haonekani hadi saa 4 usiku na ni mgeni wakatoa ripoti polisi. Aliporudi nyumbani usiku akazolewa na polisi hadi Airport na kurudishwa alikotoka, TZ - yaani ana stori nderu ndio maana mnaniona nasumbuka humu kutafuta ushauri. Taabu kweli kweli cha muhimu hatutakata tamaa. Naamini iko siku.
   
 19. elimumali

  elimumali Senior Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Leo nimeikumbuka hii comment, na nakubaliana nayo 100% kwani addiction ya kijana huyu jana imesababisha mama yake auze TV yake na DVD ili apate pesa za kumtoa kijana wake mikononi mwa Polisi. Wabaya zaidi ni WAUZAJI! Watumiaji ni waathirika, na hawapati tiba ya moja kwa moja (long time rehabilitation). Jamani ajitokeze basi Amina Chifupa mwingine, tutamtetea kwa kila hali ili WAUAJI hawa watiwe nguvuni! WANYONGWE! NINA HASIRA SANA nifanyeje mie.
   
 20. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Alikaa kwa muda gani hapo milimani Lutindi?
   
Loading...