nisaidieni nini maana ya mazingira ya uwekezaji? labda tanzania ni tofauti na dunia?

Arsene Dom

Member
Nov 21, 2010
10
0
kila mara nazikia hili neno "mzingira mazuri kwa uwekezaji" kutoka midomoni mwa vio-ngozi "wetu" watanzania.. mimi kwa kuangalia jinsi mambo yanavyokwenda hili neno kwa "vio-ngozi" (viongozi) wa nchi hii ya wadanganyika (tz) linamaanisha kama nitakavyoainisha hapo chini
1. kufukuza wazawa kama vile ni wanyama hii ikihusisha kuchomewa nyumba zao hebu angalia kesi ya loliondo eti kwa kisingizio cha "mazingira mazuri ya uwekezaji"
2. misamaha ya kodi siyoeleweka
3. faida kubwa kwa wageni na pato dogo kwa serikali .hebu angalia sekta ya madini asilima 3 tanzania na asilimia 97 "wawekezaji" ,swali je huu ni uwekezaji au uporaji?
4. kutojali sheria za utunzaji mazingira eti kuwafurahisha hawa waporaji (wawekezaji)
hebu angalia yaliyotokea north mara utapata majibu
5. kuwapa ruhusa ya kutoheshimu mikataba na kufanya wanavyotaka mfano angalia swala la shirika la reli yaani TRL yaliyotokea
6. kuwaruhusu hawa waporaji (wao huwaita wawekezaji+) kuajiri wageni katika nafasi muhimu na watanzania kubaki walinzi na wafagizi
7. ili uwe mwekezaji Tanzania uwe na ngozi nyeupe
kwa mambo kama haya husimama majukwaani bila aibu na kuisifia tanzania kuwa ina mazingira bora ya uwekezaji.. nahisi hata wao wanatushangaa sana kwa "wema" huu tunao watendea na wanatutukana kimoyomoyo kwa upumbavu wetu na wanaomba tuendelee kusinzia, tukiamka watakuwa wamemaliza kila kitu na hatutakuwa na la kufanya......
lakini hawa ndo vio-ngozi tuliowachagua kwa kura zetu na kuendelea kuwang'ang'ania
maokeo yake tunazidiwa na nchi zilizokuwa kwenye mapigano muda mrefu kama rwanda
najua yapo "mazingira mazuri ya uwekezaji" ambayo sijayataja un a weza kuogezea
 
Back
Top Bottom