Nisaidieni ndugu zangu. Nahitaji Mganga wa kweli wa kienyeji amponye mama yangu.

katuni

Senior Member
Dec 8, 2012
151
77
Nina mama yangu mdogo yu mgonjwa kwa muda mrefu sana.

Matatizo yake yanahusiana na haya mambo ya kiswahili. Ameshakaa sana hospital bila mafanikio. Amekwenda huku na kule lakini wapi. Kinachomtesa ni JINI. Ana jini kubwa sana ambalo lilimkumba tangu akiwa bado mdogo. Baadhi ya wataalam walikili kwamba ni ngumu kulitoa hilo jini.

Wengine wakasema likitolewa na yeye mama anaweza akafariki. Linamtesa sana mama yangu. Sasa ivi hadi amepalalaizi mkono ila mdomo haujampinda. Nisaidieni japo kunielekeza kwa mtu ambaye unadhani ataweza kumsaidia huyu mama maana waganga wengi ni siyo kweli. Ukiona aibu kunielekeza hapa, we nitumie hata PM unielekeze.

Nisaidieni jamani.
 
Mimi naomba uende hospital, kama hutajali nitumie pm dalili zake, tuone. Na ametibiwa hospital zipi
 
Mkuu mbona unakimbilia Uganga, mganga hatoi jini ila anaweka pandikiza la jini lingine.
Mathayo 15:13 'Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa'. Mkimbilieni Mungu.
 
mkuu kama mna hela ya nauli mpekeni tu kwa tb joshua nakuhakikishia atarudi mzima wa afya
 
Ni pm ili tuanze huduma ya maombi na maombezi hapo uweke namba yako ya simu tuanze. Hakuna haja ya kwenda NIGERIA. YESU ni yuleyule atosha.
 
Nina mama yangu mdogo yu mgonjwa kwa muda mrefu sana. Matatizo yake yanahusiana na haya mambo ya kiswahili. Ameshakaa sana hospital bila mafanikio. Amekwenda huku na kule lakini wapi. Kinachomtesa ni JINI. Ana jini kubwa sana ambalo lilimkumba tangu akiwa bado mdogo. Baadhi ya wataalam walikili kwamba ni ngumu kulitoa hilo jini. Wengine wakasema likitolewa na yeye mama anaweza akafariki. Linamtesa sana mama yangu. Sasa ivi hadi amepalalaizi mkono ila mdomo haujampinda. Nisaidieni japo kunielekeza kwa mtu ambaye unadhani ataweza kumsaidia huyu mama maana waganga wengi ni siyo kweli. Ukiona aibu kunielekeza hapa, we nitumie hata PM unielekeze. Nisaidieni jamani.
Pole sana kwa kuumwa na mama mdogo ana jini Mkubwa kabisa Akipenda

Mungu nitaweza kulitoa inshallah. Jaribu kuwasiliana na mimi kwa njia ya Email yangu address hii fewgoodman@hotmail.com inaonyesha

mumechelewa mpaka hilo jini limempozesha mkono mama mdogo? Ulikuwa wapi wewe kuleta haya malalamiko hapa Jamii forums?

Mama yako mdogo ana umri wa miaka mingapi? na ameanza kuumwa tangu lini? alipima vipimo vyote hospitali? yaani vipimo vya Damu

na Mkojo na X-ray? na haikuonekana maradhi yoyote yale? wasiliana na mimi nitaweza kumsaidia na akapona kabisa .

Subiri aje dokta MziziMkavu atakusaidia tu. Pia usikate tamaa Mungu yupo.
Vipi mkuu* habari

yako? unaendelea na tiba yetu ya faida ya Maajabu ya Maji?
 
Pole ndugu yetu.. naomba kuuliza je mama mdogo alishafanyiwa ct scan?? Nakumbukuka nilimpoteza mjomba ktk mazingira kama hayo.
 
Nina mama yangu mdogo yu mgonjwa kwa muda mrefu sana. Matatizo yake yanahusiana na haya mambo ya kiswahili. Ameshakaa sana hospital bila mafanikio. Amekwenda huku na kule lakini wapi. Kinachomtesa ni JINI. Ana jini kubwa sana ambalo lilimkumba tangu akiwa bado mdogo. Baadhi ya wataalam walikili kwamba ni ngumu kulitoa hilo jini. Wengine wakasema likitolewa na yeye mama anaweza akafariki. Linamtesa sana mama yangu. Sasa ivi hadi amepalalaizi mkono ila mdomo haujampinda. Nisaidieni japo kunielekeza kwa mtu ambaye unadhani ataweza kumsaidia huyu mama maana waganga wengi ni siyo kweli. Ukiona aibu kunielekeza hapa, we nitumie hata PM unielekeze. Nisaidieni jamani.

Kwanza nenda hospitali hakikisha kuwa sio tatizo la kitabibu. Kama hospitali watasema hakuna tatizo, nenda tanganyika packers kwa Askofu Gwajima, nenda BCIC mbezi kwa askofu Gamanywa....kama ni Jini au nini basi hilo ni tatizo dogo sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom