Nisaidieni, MUHIMBILI wamesema figo, hindu mandal wamesema moyo, Mwili unavimba

Kaka mwisho

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
402
166
Ndugu yangu anaumwa sana alipoenda hospital muhimbili wamesema figo imejaa maji wakati hindu mandal wamesema moyo ndio tatizo haufanyi kazi vizuri.

Mwili mzima umevimba na upumuaji umekuwa wa shida sana hatembei miguu yote inauma na uongeaji umekuwa wa shida sana. Ushauri na maombi yako ni muhimu sana.
 
Ndugu yangu anaumwa sana alipoenda hospital muhimbili wamesema figo imejaa maji wakati hindu mandal wamesema moyo ndio tatizo haufanyi kazi vizuri. Mwili mzima umevimba na upumuaji umekuwa wa shida sana hatembei miguu yote inauma na uongeaji umekuwa wa shida sana. Ushauri na maombi yako ni muhimu sana.

Pole sana Kaka mwisho ... Mgonjwa si lazima awe na tatizo moja tu, yaani Figo au Moyo. Mgonjwa anaweza akawa na tatizo zaidi ya moja, yaani akaugua Figo na Moyo vyote, na hata zaidi ya hayo. Matatizo ya Moyo yanaweza yakasababisha Figo zishindwe kufanya kazi (Renal Failure), na matatizo ya Figo yanaweza sababisha Moyo ushindwe kufanya kazi (Cardiac Failure).

Kuna uwezekano mgonjwa wako ana vyote, Cardiac na Renal failure...sasa inategemea Daktari kabobea wapi na kugundua kipi. Inawezekana mgonjwa wako ana matatizo ya moyo ya muda mrefu (labda mnajua au hamjui) yakapelekea maFigo kushindwa kufanya kazi, nayo yamapelekea tatizo la moyo kuwa kubwa zaidi..ndio maana mgonjwa wako amevimba mwili mzima (Renal Failure), na anapumua kwa shida (shortness of breath - Cardiac Failure).

Kuwa makini na majibu ya vipimo, naamini amefanya vipimo vingi...uliza Daktari maswali juu ya majibu ya vipimo, pia ulizia uwezekano wa kuwa na magonjwa yote mawili..ili ueleweshwe na ujue kwa uhakia nini matatizo ya mgonjwa wako na matibabu yake yatakuwaje.

Jitahidi (hata kwa gharama) mgonjwa wako amuone 'Physician' (Specialist Internal Medicine), hata ikibidi Cardiologist (Dr Hery Mwondolela - Heameda Clinic) na Nephrologist (Dr Pascal Rugajo - Muhimbili/Heameda Clinic). Okoa maisha ya nduguyo!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu anaumwa sana alipoenda hospital muhimbili wamesema figo imejaa maji wakati hindu mandal wamesema moyo ndio tatizo haufanyi kazi vizuri. Mwili mzima umevimba na upumuaji umekuwa wa shida sana hatembei miguu yote inauma na uongeaji umekuwa wa shida sana. Ushauri na maombi yako ni muhimu sana.
Ndugu pole sana kwa hayo matatizo ya ndugu Fuatilia maelezo ya Dr Riwa yeye amemaliza kila kitu Muwahishe kwa wahusika Ma-Daktari Mabingwa ili upate kuyaokowa maisha ya ndugu yako pole sana Kaka mwisho Mwenyeezi Mungu atamponyesha kwa jitihada za Ma-Dakatari ameen.
 
Pole sana Kaka Mwisho Kwa kuuguliwa na ndugu yako.,,,Zingatia sana ushauri Wa Riwa ni wa muhimu sana,waone hao specialists Kwa ushauri na matibabu ya ndugu yako.Namuombea M/Mungu amsaidie katika kuugua kwake akaweze kupona.Amina!
 
pole sana,usiogope amini mungu yupo pamoja nawe,muhimbili kuna madaktari wazuri fanya kama wasemavyo,utapona
 
Pole sana kwa tatizo LA nduguyo

watafute hao specialist haraka, Dr Rugajo alikuwa nje kimasomo in case utahitaji mawasiliano yake ni-PM nitakupatia.
 
Back
Top Bottom