Nisaidieni kimawazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni kimawazo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by msasa, Oct 30, 2009.

 1. m

  msasa Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina ex-wife ambaye kwa mda mrefu mawasiliano yetu tunafanya kwa ajili ya mtoto wetu mpendwa ambaye anaishi nae yeye. Zaidi ya hapo akinipijia labda kwa shari tu ila hatuna mawasiliano zaidi ya hapo. Sasa jana kanipijia simu tena alikuwa mpole hadi nikashangaa alichoniambia kuwa alitaka kunisalimia tu nikamshukuru nikakata sim, nikawa nawaza manake haijawahi kutokea mara akapijia tena akanambia this week anaomba tuonane nikamwambia ntachek kama nitapata nafasi. Kwa sasa nina wife wangu mwingine mpendwa naishi nae. Sasa ushauri kutoka kwenu maanake ninajiuliza sana hasa nini anachoniitia ni heri au shari nisaidieni
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sisi hatuwezijua kama anakuitia shari au heri la msingi kubali wito but nenda na wifi na usisitize uwepo wake kwatika mazungumzo kwani hakuna siri kati yako na mkeo.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Du hapo mkuu usitie maguu kama unampenda huyu mkeo ulie nae sasa, anaweza akakutega mwishoe mkasau yaliyopita na kuganga yajayo.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Unajuaje pengine hata hamwitii hayo anayojiwazisha. Wanasema kataa neno usikatae wito. Aende tu BUT aende na my wife wake wa sasa.
   
 5. mbuvu

  mbuvu Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hakuna ubaya wowote kuonana nae kwani ni mzazi mwenzako na vilevile katika uhusiano wenu kuna mambo mengi mliyofanyiana ambayo kila mmoja wapo kwa wakati wake huyakumbuka na hasa yale mazuri na yalioyokuwa yakiwafanya mfurahie mapenzi yenu.Nadhani amekumbuka ndio maana kwa upole kakubigia simu na kutaka muonane.
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yes,,nenda lakini na mkeo. nyie ni wazazi na tena yawezekana amekumbana na magumu kwenye malezi ya mwanenu anahitaji mtu wa kushare naye, kuwa wazi kwa wife wako in every step, mshirikishe na awepo.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kusitasita kwako tayari nishaona kwamba wewe una hali fulani ya natakasitaki!...Lakini
  ukitaka kuishi vizuri na huyo bibie ndugu, simamakiume mwambie machoni jambo la ukweli bila kumwogopa. Kama ni mambo ya mtoto ni bora muelewane jinsi ya kulikabili, lakini si vyema kuitana konakona
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu msasa wewe si mwanaume? nenda onana naye, ni mzazi mwenzio. nenda ukiwa na nia thabiti kuwa hakuna kukumbushia. zaidi zaidi ulizia kwa nini ameamua kukuita sasa na sio wakati uliopita.

  Nisingeshauri uende na mkeo, kwa sababu naye hatakuwa huru kusema anachotaka kusema. atajisikia kidogo embarrased. Mkabili kiume ukishatoka hapo utapata jibu.
   
 9. herrypeter1

  herrypeter1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 17, 2009
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni pesa ndo inafanya akuite na wala si jingine
   
 10. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kwani mliachana katika mazingira gani? Ni wewe ulimwacha sababu ya uliyenaye au...,

  Wito wake unategemea zaidi na jinsi mlivyoachana, kama bado anamapenzi nawe hapo ni majaribu sana ya kukutana naye kona. Wanawake wana kasumba sana.

  Anaweza kuja kwako na kuwa mwingine kabisa ukasahau yaliyopita,atakubembeleza sana, ili tu akishakuweka kwenye line, maumivu yatabaki kwa mkeo na familia yako.

  She is already a loser, nothing to worry, sasa kilichobaki huenda anataka kukuharibia na wewe. UENENDE KWA AKILI MAANA NI MJANJA KAMA NYOKA, ikibidi msikutane usiku, na wala mafichoni kama kweli unaipenda ndoa yako.

  Kila la heri mkuu, we ndo kidume sasa angalia usiangushwe.


   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Mzee, kilichowaachanisha hakiwezi kuwaunganisha kamwe, mawasiliano ya kawaida na ya wazi na mzazi mwenzio kuhusu mtoto/watoto ni kitu cha kawaida,lakini epuka sana kurudia mwanamke au mume mlieachana labda kama mazingira ya kuachana kwenu ni ya kawaida na wewe huna mke au mume mwingine.

  Binadamu tumeumbwa wapole wa midomo, muonekano na mienendo yetu lakini roho zetu zinaficha siri kuu!.....hujui kwa nini anakutafuta na kwa ushauri tafadhali sana epuka kuwasiliana nae kwa sms au simu katika mazingira tata (unaelewa) kama mtoto anaishi nae ni bora ongea na mkeo wa sasa umchukue uishi nae wewe akue katika makuzi mazuri vinginevyo atakuvuruga ukose na huyo mke wa sasa........Kina mama wana mambo mzee,
   
 12. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wewe nenda kamsikilize ndio uje hapa utuambie kuwa amekwambia nini. Saasa unasita kama anataka mimba nyingine je?
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani nyie wote mliomshauri aende na mkewe kwa huyo ex-wife wake mnaijua tabia au reaction ya mkewe au m,namsahuri na yeye anamwaga asante hapa tu? Wake wengine vichefu chefu nyie!! Haya nenda naye Bwana wewe ndio unajua
   
 14. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mhhh sidhani kama itakuwa vizuri kwenda na mke wako wa sasa hivi...Hivi mfano umeenda nae hivi kweli ataweza kuongea kama jinsi inavyotakiwa??Mkubwa wewe mwanaume nenda na kamsikilize nini anasema ila ninachokushauri kwamba mchukue rafiki yako wa karibu usiende mwenyewe na ukifika pale usinywe kinywaji chochote kile......
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,771
  Trophy Points: 280
  MJO1, sidhani katika huu mwaliko mke wa sasa alikuwa included. Kwenda naye itakuwa ni kutafuta shari, lakini labda mama ana shida ambayo haihusiani na mtoto na anataka mwenzake amsaidie. Kwa maoni yangu nenda lakini kama unaitiwa nanihii...kazi kwako, Utajiju!
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wewe nenda kamcheki:
  nenda na mkeo wa sasa kama mkeo umemwambia na anajua kama una mtoto nje ya ndoa:
  ukifika usiendekeze masihara na kumsikiliza anyoosh maelezo kwakile alokuitia:
  fanya utaratibu wa kumchukua mtoto mara moja:
  we nenda kaka wala usohofu, kama kawaida kaka si unajua halua haina kipolo??!!!!
   
Loading...