Nisaidieni kijana wangu wamempa pesa fekio kwenye account ya mpesa, nianzie wapi?

Mbwambo

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
625
93
Jamani mimi ni mama ambaye nimempatia kijana wangu anifanyie biashara ya mpesa tangu july mwaka huu sijakutana na shida leo hii ninapigiwa simu kutoka nyumbani wananiambia wamepeleka kuweka hela (float) happy mvungi asubuhi ya leo. Cashier alipoweka hela kwenye machine akakuta laki nne na nusu ni feki. Transaction ilifanyika jana tu mchana mtu alikuja kuweka binti akaja akaniambia nimepokea hela na float sasa imekwisha. Swali la kwanza nilimuuliza ume zi check hela vizuri?
Akasema ndio kumbe zile hela alipewa feki
hatua gani nimechukuwa?
1. Watu kuile nyumbani walipiga simu vodacom na wakaelezea kisha vodacom wakasema huyo mtu ameishakuwa hizo hela ila wakasema wameisha block namba yake. Je hiyo kweli inasadia?
Mimi nikawaambia kum block haisadii kitu maana si atafungua namba nyingine?

Sasa naomba ushauri nifanyeje kwa sasa?

Kwa sasa nimejifunza kwamba natakiwa kuwa na machine ya ku chek hela kama ni halali au la
asanteni
 
mimi crdb mbezi beach walinipa laki 1 fake ktk bundle la 10million!yani kila note 1 fake ktk milioni 1.pole
 
Mkuu ni rahisi kum-trace huyo mwenye namba hiyo na kumpata unless namba hiyo aliotumia hajawahi kuongea na mtu mwingine yeyote na hiyo simu aliotumia haijawahi kuingizwa simcard nyingine yeyote.. Tatizo kubwa ni jinci ya kupata hizo huduma zote.. Polisi ni wazembe na waracimu kwenye hilo unless uwe na
god father huko juu.. Anyway jaribu kufungua jalada polisi ucikikie watakuambia nini.. Ucikate tamaa ndugu yangu..
 
Kama umesha mjua aliyefanya hilo tukio toa taarifa polisi japo ushahidi ni mgumu hapo kwasababu tukio limegunduliwa baadae sana,mmaweza kumkamata huyo mhusika lakini je akikana unauthibitisho gani kama ni mtu mwingine aliyeleta hiyo fedha?kijana anatakiwa awe makini zaidi kukaagua noti vizuri kabla ya kurusha float na pia kukagua hesabu zake mara kwa mara ili kama kunatatizo inakua rahisi kuligundua.
 
Mkuu ni rahisi kum-trace huyo mwenye namba hiyo na kumpata unless namba hiyo aliotumia hajawahi kuongea na mtu mwingine yeyote na hiyo simu aliotumia haijawahi kuingizwa simcard nyingine yeyote.. Tatizo kubwa ni jinci ya kupata hizo huduma zote.. Polisi ni wazembe na waracimu kwenye hilo unless uwe na
god father huko juu.. Anyway jaribu kufungua jalada polisi ucikikie watakuambia nini.. Ucikate tamaa ndugu yangu..

Kwa kweli ninashukuru sana kunijali nakusoma shida yangu kisha kunipa pole. Mimi ninawafahamu Polisi kwamba ni wazembe ila kama siyo uzembe wao kweli nina imani watampata tu huyo mtu unless kama hiyo simcard hajaongea na mtu yeyote.
Maana VODA wanasema kaishatoa hiyo hela tayari
Ninasema sina mtu yeyote Polisi na mimi alimradi nimefungua jalada tayari basi ninamwamchia Mungu
Kuna mtu anasema atakataa kwamba hajaitoa hiyo hela kwa muuzaji wangu. Nikamwambuia FLOAT ilikuwa na laki 5 na yeye ndiye alikuja kuomba aweke laki nne na nusu akaweklewa kwenye line yake na sisi tumepokea cash yake kiasi hicho hicho ambacho ni feki sasa atakataaje wakati amaefanya transaction yeye?
Anyway nitajaribu kuongewa na mwanasheria wa hapa kazini atasema lakini mimi sikuwa na hela zaidi ya hizo kwenye cash yangu
 
Pole sana ndugu yangu, ila nasikitika kuwa huna ushahidi usioacha shaka wa kumtia hatiani mtuhumiwa hata kama utamshika. Kumbuka huna namna ya kuithibitishia mahakama kuwa kijana wako hakuwa na hela nyingine feki au hajabadilisha fedha feki na kuzitoa za fedha halali ambazo mtuhumiwa anaweza kudai kuzitoa kwa kijana wako na kijana wako kuzihakiki na ndio maana akamwekea salio kwenye MPesa account yake.

Kwa msaada tu wa kisheria siku za usoni ...utaweza tu kumtia hatiani ikiwa aidha:
(i)umefunga kamera ambayo imenasa tukio zima ikiwamo kuonesha walau namba ya noti bandia mojawapo/....au

(ii) Umemshika right on the spot na fedha bandia na kumpeleka ready handed to Police post au kuita polisi ukiwa naye ndani bado...

Vinginevyo ndugu yangu ni vyema umuachie tu Mungu kwa kuwa utajisumbua tu bure na pengine kutoa hongo polisi (ambayo ni kuongeza gharama kwako) wakati ukijua fika kuwa kwa mkono wa sheria huna uwezo wa ku-recover chochote wala kumweka ndani kwa tuhuma hizo.

Somo hapo kwetu sote ni " kutokumwamini mtu yoyote katika swala la fedha na kuhakikisha fedha yoyote tuipokeayo iwe kwa mikono au kwa mashine kutegemeana na wingi wa noti tupokeazo"

Naomba kuwasilisha !
 
Back
Top Bottom