Nisaidieni kazi yoyote jamani nateseka!

EveningStar

JF-Expert Member
Nov 14, 2018
262
162
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Nimeangaika kutafuta kazi kwa muda mrefu sana pasipo kupata mafanikio yoyote yale na muda unazidi kwenda, yaani hapa nilipo sina mahali pakuishi nimehifadhiwa tu kwa ndugu na ninalala ukumbini, kula yangu imekuwa ya tabu sana. Nimepeleka nyaraka zangu sehemu mbalimbali hasa viwandani hapa DSM lakini hawajanibu chochote na muda unaenda.

Hapa kwa ndugu nilipo wameshanichoka japokuwa nalala ukumbini lakini wanataka kunifukuza yaani nina hali mbaya sana jamani. Kwahiyo naomba kwa yeyote yule mwenye kazi au mwenye kuweza kuniunganisha nq kazi usisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, mimi sichagui kazi na nipo tayari kufanya kazi yoyote ili mradi iwe halali tu mimi nitaifanya. Nisaidieni jamani maana niko kwenye hali mbaya sana jamani. Mimi nipo Dar es salaam.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki!
 
mkuu pole sana. sana
sisi ndo mana tunauza Bangi mkuu japo tunajua kuna magogoni central ila hakuna namna
cha msingi hapo weka makabrasha chini ingia mtaani tu pambana piga hatadebe mkuu
Ushauri wako ni mzuri sana binafsi nimekuwa nikiwaambia hata vijana wenzangu kwamba kwa hali ilivyo sasa inabidi mtu upige kote kote
 
ila mkuu wengi wao hawa ndugu zetu wasomi
wanamentality ya kuwa msomi sijui ndo nani yani ,kama bhakhresa au ukisoma ww ni wa kuajiriwa tu.
yani unafuta ujinga mmoja unaongeza ujinga mwingine wa kuwa ww ni wa kuajiriwa tu
kusoma ni kutoa ujinga,kusoma ni kuongeza maarifa na ufunuo wa kukupeleka huko kwenye mafanikio.
kwahiyo ukimaliza pale Udsm ,huku umetuma email NMB huku unabeba lumbesa mahakama ya ndizi kwani nani atakuuliza? Heshima pesa haijalishi unakozitoa ,hata kama unafaulisha vyoo hio ni pesa haijawekwa lebo ya mpiga debe hapo mkuu
 
Upo dar sehem gani jaribu kuomba hata kufundisha private schools unaweza kupata relief
 
ila mkuu wengi wao hawa ndugu zetu wasomi
wanamentality ya kuwa msomi sijui ndo nani yani ,kama bhakhresa au ukisoma ww ni wa kuajiriwa tu.
yani unafuta ujinga mmoja unaongeza ujinga mwingine wa kuwa ww ni wa kuajiriwa tu
kusoma ni kutoa ujinga,kusoma ni kuongeza maarifa na ufunuo wa kukupeleka huko kwenye mafanikio.
kwahiyo ukimaliza pale Udsm ,huku umetuma email NMB huku unabeba lumbesa mahakama ya ndizi kwani nani atakuuliza? Heshima pesa haijalishi unakozitoa ,hata kama unafaulisha vyoo hio ni pesa haijawekwa lebo ya mpiga debe hapo mkuu
nafikiri wewe unaweza saidia vijana wengi sana
 
Unaishi sebuleni kwa ndugu.. Nyumbani kwenu ni wapi na kwanini usirudi nyumbani?

Nadhani nikijua hilo ntakushauri cha kufanya
 
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Nimeangaika kutafuta kazi kwa muda mrefu sana pasipo kupata mafanikio yoyote yale na muda unazidi kwenda, yaani hapa nilipo sina mahali pakuishi nimehifadhiwa tu kwa ndugu na ninalala ukumbini, kula yangu imekuwa ya tabu sana. Nimepeleka nyaraka zangu sehemu mbalimbali hasa viwandani hapa DSM lakini hawajanibu chochote na muda unaenda.

Hapa kwa ndugu nilipo wameshanichoka japokuwa nalala ukumbini lakini wanataka kunifukuza yaani nina hali mbaya sana jamani. Kwahiyo naomba kwa yeyote yule mwenye kazi au mwenye kuweza kuniunganisha nq kazi usisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, mimi sichagui kazi na nipo tayari kufanya kazi yoyote ili mradi iwe halali tu mimi nitaifanya. Nisaidieni jamani maana niko kwenye hali mbaya sana jamani. Mimi nipo Dar es salaam.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki!
Iyoo kofia ya shahada uliyovaa ivue kuna wenzio waliishia darasa la 7,ndo wanakimbiza maisha,fanya kazi yoyote tafuta hata genge uchome chips one day itakuuuua big yes kinachokutesa ni huna xpirience ya mtaa ambacho ndio kinachochea wewe kuwa dependent psychological kuajiriwa
 
Jiwe kaivuruga sana hii nchi. Vijana wasio na ajira mtaani ni maelfu kwa mamia sijui watakwenda wapi masikini. Poleni sana
HaTa system yetu ya elimu ni chanzo kikubwa,na mfumo wa maisha wa kila mtu mmojammoja pia,ila Tz opportunities zipo nyingi sana ni mtu kuamua tuu
 
Hii fani soko lake la ajira ni dogo mno., ni nadra saana kupata kiwanda kinachohitaji fani hiyo.,Ila usikate tamaa.., ukiona kazi za extension we omba., utakwenda kufit huko huko ndani., unaweza kuajiliwa as extension ndani kupata field ya food science.,
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Nimeangaika kutafuta kazi kwa muda mrefu sana pasipo kupata mafanikio yoyote yale na muda unazidi kwenda, yaani hapa nilipo sina mahali pakuishi nimehifadhiwa tu kwa ndugu na ninalala ukumbini, kula yangu imekuwa ya tabu sana. Nimepeleka nyaraka zangu sehemu mbalimbali hasa viwandani hapa DSM lakini hawajanibu chochote na muda unaenda.

Hapa kwa ndugu nilipo wameshanichoka japokuwa nalala ukumbini lakini wanataka kunifukuza yaani nina hali mbaya sana jamani. Kwahiyo naomba kwa yeyote yule mwenye kazi au mwenye kuweza kuniunganisha nq kazi usisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, mimi sichagui kazi na nipo tayari kufanya kazi yoyote ili mradi iwe halali tu mimi nitaifanya. Nisaidieni jamani maana niko kwenye hali mbaya sana jamani. Mimi nipo Dar es salaam.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki!
 
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Nimeangaika kutafuta kazi kwa muda mrefu sana pasipo kupata mafanikio yoyote yale na muda unazidi kwenda, yaani hapa nilipo sina mahali pakuishi nimehifadhiwa tu kwa ndugu na ninalala ukumbini, kula yangu imekuwa ya tabu sana. Nimepeleka nyaraka zangu sehemu mbalimbali hasa viwandani hapa DSM lakini hawajanibu chochote na muda unaenda.

Hapa kwa ndugu nilipo wameshanichoka japokuwa nalala ukumbini lakini wanataka kunifukuza yaani nina hali mbaya sana jamani. Kwahiyo naomba kwa yeyote yule mwenye kazi au mwenye kuweza kuniunganisha nq kazi usisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, mimi sichagui kazi na nipo tayari kufanya kazi yoyote ili mradi iwe halali tu mimi nitaifanya. Nisaidieni jamani maana niko kwenye hali mbaya sana jamani. Mimi nipo Dar es salaam.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki!
Kwanza pole sana aisee. Pili ajira ni shida kila kona. Ujanja wa sasa hivi ni kujiajiri.

Tatizo la kujiajiri ni mtaji na wateja. Ila kuna site mpya ya freelancing Tanzania inaitwa www.ajiras.com.

Hii site unaweza kujiunga bure na kupost kazi unayoweza kufanya na gharama zako.

Mfano, una degree ya chakula, na uwakika unaweza kufanya kazi kama consultant. Kuna kampuni nyingi au watu binafsi ambao hawana uwezo wa kukujiajiri full time lakini wanahitaji ujuzi wako.

Kwa hiyo, wataweza kukuita ukapiga kazi, unachukua chako unaondoka. Mambo jinsi yanavyoenda, kampuni nyingi Tanzania zita prefer njia hii badala ya full time ajira.

Unaweza pata kazi za Consultant nyingi na zikalipa kuliko mshahara na one day ukafungua kampuni yako.

Raha ya www.ajiras.com ni kuwa kujiunga ni bure, uhitaji ofisi, ni simu au computer yako na ujuzi wako basi.

Cheki uone baadhi ya kazi zilizopo.
 
Mkuu upo tayari kuja wilayani upige kazi ya 170000 kwa mwezi?
Mimi nipo tayari mkuu kwa malipo yoyote yale ilimradi tu iwe kazi halali, mimi sitanii nina shida kweli na wala sitanii nimeshachoka kulala ukumbini yaani wewe acha tu mkuu, kama upo tayari kunisaidia nitafute 0758 106 501 sichaguhi kazi. Nisaidieni jamani nagalagala ukumbini kama Paka vile nimeshachoka. MUNGU akubariki na nitakushukuru sana kwa yeyote atakaenisaidia.
 
Kwanza pole sana aisee. Pili ajira ni shida kila kona. Ujanja wa sasa hivi ni kujiajiri.

Tatizo la kujiajiri ni mtaji na wateja. Ila kuna site mpya ya freelancing Tanzania inaitwa www.ajiras.com.

Hii site unaweza kujiunga bure na kupost kazi unayoweza kufanya na gharama zako.

Mfano, una degree ya chakula, na uwakika unaweza kufanya kazi kama consultant. Kuna kampuni nyingi au watu binafsi ambao hawana uwezo wa kukujiajiri full time lakini wanahitaji ujuzi wako.

Kwa hiyo, wataweza kukuita ukapiga kazi, unachukua chako unaondoka. Mambo jinsi yanavyoenda, kampuni nyingi Tanzania zita prefer njia hii badala ya full time ajira.

Unaweza pata kazi za Consultant nyingi na zikalipa kuliko mshahara na one day ukafungua kampuni yako.

Raha ya www.ajiras.com ni kuwa kujiunga ni bure, uhitaji ofisi, ni simu au computer yako na ujuzi wako basi.

Cheki uone baadhi ya kazi zilizopo.
Ahasante mkuu kwa ushauri wako.
 
Mimi baada ya kumaliza shahada yangu ya kwanza sikusumbuka kutembea na bahasha kama wewe,
Nilijiunga kwa mafundi ujenzi (wengi wao ni std 7) kama kibarua wao na baada ya muda nilipata mtaji wa kufanya biashara ya mazao na kilimo.

Kifupi,sijawahi tamani kuajiliwa kwani mapato yangu kwa mwezi ni mara dufu ya mameneja wengi wa bank,ujasiriamali unalipa sana.

Fuga kuku n.k,lima mazao ya chakula ,fanya biashara ya mazao,uza mitumba n.k.
 
Back
Top Bottom