Nisaidieni JF GTs: JK aagiza wizara ianzishe Idara ya kushughulikia Watanzania walioko nchi za nje.

Proud Patriot

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
224
10
Salaam wana-JF! Katika hali ya kunishangaza mpaka moyo kushtuka kijoti, wakati napitia hotuba ya Rais JK ya sept 2011 nilishtushwa na hili,nanukuu: ".....Ndiyo maana katika Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
tumeunda Idara ya kushughulikia
Watanzania walioko nchi za nje.
"
Sasa nikajiuliza wizara ya mambo ya NJE imeagizwa kuanzisha idara ya kushughulikia watanzania walioko nchi za NJE. Hivyo kunifanya nihoji kwani waTZ walioko nje walikuwa (huwa) wanashughuliwa na wizara/chombo kipi cha Serikali kabla. Kwa uelewa wangu nilidhani kuwa ni wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ndo inahusika na waTZ waishio nchi za nje. Naomba mwongozo kwa yafuatayo:
Je kundi hilo la waTZ lilikuwa likishughulikiwa na wizara/chombo kipi?
If you ask me, sioni sababu ya kuanzishwa idara ya "A" katika wizara ya "A & B". Hii kwa kweli ni unnecessary expenditure
 
Aseeee..
idara A kwenye wizara ya A&B.

msamehe yule jamaa, sidhani kama alikuwa anajua anachosema, usually he dont...
 
Sijui siye choka mbaya hapa ndani tz nani anashughulikia matatizo yetu,maana hao kawaahidi taasisi ziwasaidie viwanja,majumba wakati sisi wanagongo la mboto tuko mahemani, anafikiria kuwawezesha jamaa zetu dual citizenship wakati wabongo original-mababu-babu-baba-mtoto tumezaliwa hapa kupata kadi ya uraia vumbi haswa kama huna magamba, any ilikuwa lazima aongee chochote !
 
Sijui siye choka mbaya hapa ndani tz nani anashughulikia matatizo yetu,maana hao kawaahidi taasisi ziwasaidie viwanja,majumba wakati sisi wanagongo la mboto tuko mahemani, anafikiria kuwawezesha jamaa zetu dual citizenship wakati wabongo original-mababu-babu-baba-mtoto tumezaliwa hapa kupata kadi ya uraia vumbi haswa kama huna magamba, any ilikuwa lazima aongee chochote !

Mkuu usiwe na shaka Jeshi la Polisi lipo bega kwa bega kukuhudumia
 
Hilo nalo swali!!. Ngoja wataalamu wa International Relationship waje kutujuza.
 
Hilo nalo swali!!. Ngoja wataalamu wa International Relationship waje kutujuza.

Neno haswaa, manake mi kanichanganya... Au ndo ili mradi tu kahutubia? Yip-Yaping his mouth bila kufikirisha ubongo
 
Tatizo tulilonalo ni mfumo wa uongozi unaompa madaraka rais kuanzisha nafasi yeyote ile hata kama haiko kwenye hekama. Hivi sasa rais wetu anakabiliwa na tatizo la ukame mkubwa wa uungwaji mkono na watanzania; huko Marekani amekuta wakina Maajar katika kupalilia kula yao wamemwandalia kundi la wadiaspora lililompokea kama shujaa. Kwasababu katiba inamruhusu anajaribu kulipa fadhila.
 
Kushugulikia mambo yapi? na hiyo wizara ilikuwa haina kazi kama hizo awali? alikuwa anaongea live au recorded labda aliongea Rwehemamu alikuwa anaigiza sauti ya Kikwete!

Je hiyo ilikuwa katika list za kazi za Serikali mwaka huu, kwa maana ya kuwa ni utekelezaji wa jambo ambalo lilifanyiwa utafiti wa kutosha na kuchambuliwa bayana au ndio kila tukiamka tusubiri kusikia lolote? 'Ad hoc Govering system'
 
Back
Top Bottom