Nisaidieni hizi hesabu za Temeke! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni hizi hesabu za Temeke!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 9, 2006.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 9, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimesoma habari hii kwenye ippmedia.. na nikajaribu kuziangalia hesabu zao jumla na asilimia n.k haziingii akilini!! Sijui ni tatizo la kuripoti au yeyote aliyetumwa kutoa habari za Bajeti ya Temeke hajua asubuhi vizuri au kufafanua takwimu? Au kwa makusudi wanajaribu kuwachanganya watu? Hili ni Jukwaa la Uchumi... nisaidieni!!

  Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Jijini,imepanga kutumia mabilioni ya fedha katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka 2006/07.

  Manispaa hiyo katika bajeti yake ya mwaka huu imepanga kutumia kiasi cha bilioni 8.2 kwa miradi ya maendeleo.

  Taarifa hizo za kutia matumaini zimetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Bwana Idd Nyundo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoketi kwa lengo la kutangaza bajeti ya mwaka 2006/07.

  Amesema fedha hizo zitatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo michango kwa Halmashauri hiyo ambayo ni shilingi 2,129,150,000.00 sawa na asilimia 26.00, ruzuku ya maendeleo Sh.105,00,000.00 sawa na 1.28 pamoja na tuzuku ya MMEM ambayo ni Sh. 1,297,000,000 sawa na asilimia 15.83.

  Ametaja vyanzo vingine kuwa ni ruzuku ya kujenga uwezo ambayo ni Sh. 1,745,000,000 sawa na asilimia 21.30 na wahisani shilingi 2,737,873,800 sawa na asilimia 33.54.

  Pia amesema kiasi cha shilingi 168,000,00 kitatokana na michango ya wananchi.

  Amesema mpango huo umezingatia sera ya serikali katika Dira ya maendeleo ya Taifa (Vision 2025) na mwongozo wa bajeti wa mwaka 2006/07 kama ulivyotolewa na wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa pamoja na Hazina.

  Aidha Mkurugenzi huyo ametaja vyanzo vya nje kuwa ni ruzuku kwa ajili ya mishahara ambayo ni zaidi ya Sh. Bil. 8.7, kiasi ambacho ni asilimia 34.59.

  Alisema ruzuku kwa ajili ya mambo mengineyo ni zaidi ya Sh. Bil.1.4 sawa na asilimia 5.70 wakati ruzuku ya mfuko wa pamoja ni zaidi ya Sh. Bil. 3.7 sawa na asilimia 14.75.

  Alisema ruzuku ya miradi ya maendeleo ni zaidi ya Sh. Bil. 3.1 sawa na asilimia 12.49.

  Amesema vyanzo vingine vya nje ni michango ya wananchi Sh. Mil.168 sawa na asilimia 0.67 na wafadhili Bil.1.9 sawa na asilimia 7.74 ambapo jumla ya vyanzo hivyo ni zaidi ya Sh. 25,195,126,228.00 sawa na asilimia 100.

  Akifafanua jinsi Halmashauri hiyo ilivyopanga kutumia fedha hizo,

  Bw. Nyundo alisema mishahara ya wafanyakazi itatumia kiasi cha zaidi ya Sh.Bil. 9.9 ambacho ni sawa na asilimia 39.26 na matumizi mengineyo yatatumia kiasi cha zaidi ya Sh. Bil. 7.9 sawa na asilimia 31.38


  SOURCE: Alasiri
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2014
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa waliobahatika kusoma ripoti ya CAG, kwa ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2006/07 wa fedha alisema nini kuhusu Temeke?
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2014
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280
  Please kwa wale wanaopenda kurukia mada bila kuchunguza vizuri hii mada ni ya mwaka 2006! :focus:
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2014
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  MTAZAMO, we waache watajishitukia namna wasivyojua kusoma na kuelewa yaani sawa na ile signature ya Invisible

  Karibu kwenye mjadala japo alianzisha MM.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...