Nisaidieni dawa ya kutibu Kisonono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni dawa ya kutibu Kisonono

Discussion in 'JF Doctor' started by KIBURUDISHO, Jul 2, 2012.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 45
  Wakubwa habari za kazi natumai mu wazima.Naombe msaada wenu kwa wanaoijua dawa ya kutibu ugonjwa huu.
   
 2. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  pole kisonono kitakuua,mzizimkavu kagoma hamumlipi na vitendea kazi hakuna
   
 3. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 688
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  weka picha mzee tuone iko stage gani hiyo kitu.
   
 4. Fasouls

  Fasouls JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 916
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hakuna dawa,mkiambiwa tumien kondom hamsikii,
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Kisonono (gonorrhea) ni nini?

  Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15-19 wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 -wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.

  Ugonjwa huu huambukizwa vipi?

  Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum). Ugonjwa wa gono huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya kulevya.Dalili za ugonjwa wa kisonono
  Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7 baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili ni kama zifuatazo;

  Kwa wanaume:


  • Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation)
  • Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana
  • Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
  • Maambukizi yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.

  Kwa wanawake:  • Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote
  • Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
  • Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu
  • Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika.
  • Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa
  • Kichefuchefu
  • Homa (fever)
  • Kutapika

  Vipimo vya ugonjwa wa kisonono  • Swab for culture Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono.
  • Polymerase Chain Reaction (PCR) Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.

  Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?


  Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na

  puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano. Fuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito (mfano doxycyclin). Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za ugonjwa huu.Madhara ya ugonjwa wa kisonono


  • Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
  • Huweza kuathiri moyo (heart valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
  • Madhara kwenye sehemu za maungio au jointi (joint inflammation)
  • Kwa wanawake wale ambao hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
  • Wale wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor).
  • Kwa wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu (blindness), homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).

  Kinga ya kisonono  • Kutumia kondomu wakati wa kujamiana
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
  • Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
  • Kwa wanawake wajawazito Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwengine wowote.
  • Wanawake wajawazito wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha kuwa kipofu.
  • Epuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono.

  "Kumbuka ya kwamba hakuna kitu kama ngono salama kwani huwezi kujua kama wewe au mwenzako wakati wa kujamiana ameathirika au la, au una michibuko au umekatika kwenye ngozi au la kwani michibuko mengine inaweza isionekane au kugundulika kwa urahisi. Njia pekee na nzuri ni kuacha au kujikinga na vitendo vya ngono". Mtu aliyepata gono awali anaweza kupata tena.
  ummu kulthum Aende hospitali kupiga Sindano haraka iwezekanavyo.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,201
  Likes Received: 1,600
  Trophy Points: 280
  Dr bora umemtibu kaka wa watu,lol!

  Hivi hakuna tiba m'badala ya magonjwa haya?
  Usisahau kumuambia asione soo, kwani kuugua kisonono ni dalili kuwa ukimwi hauchezi mbali naye.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Kienyeji ya Kisonono ya Tiba Mbadala Apate Mizizi ya Mvule na Mizizi ya Mbono uchemshe kwenye maji unywe kutwa mara 3 kwa muda wa wiki 3 inshallah atapona.@KIBURUDISH Mkuu.@King'asti
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Gonorrhea Pictures and Images

  Here are a few gonorrhea pictures in order to make a clearer image of this disease. They are somewhat shocking so take care.
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Baadhi ya maradhi ya kisonono hizo picha dalili zake.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,201
  Likes Received: 1,600
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu hukosi maarifa. Asante boss. Manake na mgomo huu, mweeh! Ataishia kuzodolewa na dr kwa ngono nzembe kuliko kusaidiwa.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Akikosa mizizi ya Mvule na mbono basi anaweza kutafuta mizizi ya Mkorosho akachemsha na maji anywe siku 7 kutwa mara 3 atapona tu inshallah ninamsaidia ingawa Ma Daktari Wamegoma . Mkuu King'asti
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,201
  Likes Received: 1,600
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Na hizi picha, wallah atabadilika tabia tu! Kha!
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Basi mkuu hata kubonyeza neno (Like) unashindwa?Mkuu King'asti acha uchoyo wako huo lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 1,489
  Trophy Points: 280
  Dah.. mkuu si tuliosoma na. Practice nje haya magonjwa kwa kiswahili ni mtihani.. sikujua kisonono no gonorrhea.. nambie kaswande .. kisambusa ..etcl kwa kiingereza yanaitwaje..? Je syphilis kwa kiswahili inaitwaje.?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,597
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Aende hospital akachome Ceftriaxone 2g od for 4days + Doxycycline caps 100mg bd 7/7. Wahi mapema coz siku hizi wamedevelop resistance hasa kwa dawa za kumeza tu, lazima uchome hii sindano na dawa za kumeza. Good luck
   
 15. i

  imani ernest Senior Member

  #15
  Jul 11, 2013
  Joined: Jan 16, 2013
  Messages: 105
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sija elewa nikwamba. dawa ni hakunaga?
   
 16. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2013
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,092
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  dawa ipo ssoma mchangiaji aliyepita utaona
   
 17. M

  Marnah JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2013
  Joined: May 3, 2013
  Messages: 1,128
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Allah atuepushe kwa maradhi mazito kama haya,,...@ Mzizi mkavu,,...jazaka llah kheiry
   
 18. Kiba

  Kiba JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2013
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 453
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hili janga limeninyemelea.
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,265
  Likes Received: 3,174
  Trophy Points: 280
  paka mafuta ya ubuyu kila baada ya masaa matatu
  kwa mawasailiano zaidi ni pm
  nte
  MAFUTA YA UBUYU AYANYEWI
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,265
  Likes Received: 3,174
  Trophy Points: 280
  big up kamanda usiogope utapona mwanaume jasiri bila kisonono ujaitwa mwanaume
   
Loading...