Nisaidien nifanye nn ili aniache na maisha yangu

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,905
Huyu jamaa alikuwa mpnz wangu kwa miaka 2, mwaka jana mwezi wa pili akawa amebadilika analewa sn tukawa tunagombana hatimae tukaachana mwezi wa 4 kila mtu akawa na maisha yake, yeye akapata mchumba akaoa, na mie nikawa nadate na mtu kumbe ananifatilia akafuta yule mtu wangu sikujua alimwambia nn,ila mtu wangu akaomba tuachane kwa amani na nisimtafute tena,kwa vile tulikuahatujanza kupeana nikamwacha aende zake na sikujua sababu, ni wiki mbili sasa yule x wangu alieoa ananifuatilia akiniona na mtu ananitumia msg kali na kuniambia atamfanyizia huyo mtu anaetaka kumuibia penzi lake km alivyomfanyia yule niliadate nae baada ya kuachana ndio nikajua yeye alikuwa sababu,sasa jana usiku kampigia dada yangu anamwambia anikanye nisiwe na mpnz yoyote kwan yeye ndie mpanz wangu wa maisha na mimi akanitumia msg hivyohivyo ya kunionya,naomben msaidie nimfanye nn huyu mtu aniache na maisha yangu, nawasilisha.
 
mpigie simu umweleze hupendezwi na hiyo tabia kwani kila mtu ana maisha yake
 
mimi nakushauri na wewe uwe kauzu mtafute mke wake umpe mkanda mzima na umwambie amfikishie mumewe ujumbe kwamba ahache kukufuatafuata dawa ya mume wa mtu akikuzingua wakilisha kwa mkewe lazima ashike adabu

Well said mama kigogo, nenda kamweleze mkewe huo upuuzi wake na hakikisha kila msg anazokutumia unampelekea mkewe aone
 
Hii ndio suluhisho...
 
mimi nakushauri na wewe uwe kauzu mtafute mke wake umpe mkanda mzima na umwambie amfikishie mumewe ujumbe kwamba ahache kukufuatafuata dawa ya mume wa mtu akikuzingua wakilisha kwa mkewe lazima ashike adabu
Hilo nalo neno!hiyo kweli inahusika kabisa, asante mamaa kigogo!
 
sitaki nyie mmetengana tu kwa hiyo inawezekana mkarudia suala lenu "watu hawaachani hasa waliokaa muda mrefu wanatengana tu"
tafutanene mzungumze ikishindikana mhusishe wife wake...........
 
Well said mama kigogo, nenda kamweleze mkewe huo upuuzi wake na hakikisha kila msg anazokutumia unampelekea mkewe aone
Hii imekaa vizuri, je ikitokea mkewe hakuniamin na akalishwa sumu nn mumewe kwamba mie ndio namtaka mmewe na akanigeuka na kuniona mwizi wake itakuwaje?
 
Nikimpigia hapokei,nikatumia namba tofauti aliposikia sauti yangu akakata simu.

hakuna jinsi ambayo unaweza kurahisiha kuwasiliana nae ??? au tafuta watu wake wa karibu wawakutanishe umweke wazi kwani tabia hizi zinaweza kukusumbua zaidi siku za usoni kwani yeye ana lengo la kukuharibia
 
Well said mama kigogo, nenda kamweleze mkewe huo upuuzi wake na hakikisha kila msg anazokutumia unampelekea mkewe aone

sidhani kama hii imekaa vizuri kwani matatizo ni yao wawili anaweza kumhusisha mke wa jamaa nae akawa kauzu zaidi mwisho wa siku atakuwa mbaya au akawa tatizo
 
sitaki nyie mmetengana tu kwa hiyo inawezekana mkarudia suala lenu "watu hawaachani hasa waliokaa muda mrefu wanatengana tu"
tafutanene mzungumze ikishindikana mhusishe wife wake...........
Sie tumeachana na ndio maana aliweza kuoa, anachofanya ni kuniharibia na kunikosesha amani na uhuru wa maisha yangu,na huyu hahitaji maongezi ndio maana ananipa vitisho other wise angenitafuta kistarabu tukaongea,sina uhakika km nikimwambia mkewe atakuwa upande wangu au mmewe anaweza mwambia mie ndio namtaka then na yeye akaniona mwizi kumbuka wale wanapendana ni mke namume!
 
endelea tu kuwakera na ww. kila msg hakikisha unamtumia mkewe (baada ya kupata namba yake). halafu, kwa nini usi-block namba yake ama ww kubadili namba ya simu? akiendelea mchukulie rb, tafuta mshkaji mmoja mbabe afu mumtafute ajitambulishe. ila ukimpotezea tu ataona ujinga aachane na ww. kama uliwajua wazazi wake nenda kamwage mboga,waambie wakalipe mahari kwenu akuoe mke wa pili kama wanataka!
Hii imekaa vizuri, je ikitokea mkewe hakuniamin na akalishwa sumu nn mumewe kwamba mie ndio namtaka mmewe na akanigeuka na kuniona mwizi wake itakuwaje?
 
hakuna jinsi ambayo unaweza kurahisiha kuwasiliana nae ??? au tafuta watu wake wa karibu wawakutanishe umweke wazi kwani tabia hizi zinaweza kukusumbua zaidi siku za usoni kwani yeye ana lengo la kukuharibia
Kuwasiliana nae ndio hivyo ni ngumu, nitajaribu kuwashirikisha watu wake wa karibu.
 
endelea tu kuwakera na ww. kila msg hakikisha unamtumia mkewe (baada ya kupata namba yake). halafu, kwa nini usi-block namba yake ama ww kubadili namba ya simu? akiendelea mchukulie rb, tafuta mshkaji mmoja mbabe afu mumtafute ajitambulishe. ila ukimpotezea tu ataona ujinga aachane na ww. kama uliwajua wazazi wake nenda kamwage mboga,waambie wakalipe mahari kwenu akuoe mke wa pili kama wanataka!
Wala hata cmpendi tena so sitaweza kuolewa nae,asante kwa ushauri king'asti.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom