Nisaidie ushauri wenu muhim sana kwangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidie ushauri wenu muhim sana kwangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nasra82, May 18, 2010.

 1. N

  Nasra82 Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana HY! mimi kwa mara ya kwanza naomba msaada wa mawazo yenu, mnisaidie kwa tatizo kubwa nililonalo!
  Mie ni msichana wa umri wa 28 na nimebahatika kupata mume ninaempenda sana, mwenyezi mungu ametujaalia pia kuwa tutapata mtoto karibuni akipenda yeye Inshaalah, tatizo linakuja hivi " Nilipoanza clinic kw mara ya kwanza kabisa nilienda na mr. na ktk kupima VVU tulipata majibu tofauti! mme amekutwa + na mimi nimekutwa -, wapendwa wa HY hii si mara ya kwanza kwetu kupima tulipima siku za nyuma na majibu yalikuwa mazuri kw wote! tangia nimeanza clinic 3 months tayari sshivi lakn jamani cna amani kabisa naogopa kurudi kuchek tena, japo sina dalili yoyote ile na wala siumwi namshukuru mungu, Najipa moyo kuwa wikiendi hii niende kituo chochote kucheck tena, jamani ukweli ni kwamba cna amani ya moyo kabisa, nawaza, namuomba mungu anihepushe ata cjui nifanye nn tu lakn ndio limeshanifika, naomba mnisaidie hivi ukikutana na situation km hii unawezaje kuikubali? na unakabiliananayo vp? mi sina ugomvi na mme wangu wala hakuna tofauti yeyote tangia limetokea hili ila tu mawazo kichwani kwangu hayaishi, nisaidieni jamani sijui ata nianzie wapi lakn hili tatizo linanikosesha amani! Naomba mniombee wapendwa mwenyezi mungu aninusuru, pia naombeni mnijuze jinsi ya kuishi ktk hali hii!
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pole sana!.

  Unacho hofia ni nini? kuikubali hali halisi ndio suluhisho la yoote.vile itakavyotokea ni hivyo hivyo kwani hata mtu akikushauri vipi wewe ndie mwenye mwili na uamuzi wa mwisho.

  Wakati yawezekana huna VVU, waweza kuathirika kwa msongo wa mawazo ukapata magonjwa mengine mengi kwa hofu ambazo hazina msingi.

  wakati wote unashauriwa kuwa tayari kuiikubali hali yoyote, iwe kwa kujitakia au kusababishiwa.. Zaidi ni kuomba Mwenyezi Mungu akunusuru kwa yote.

  CHUKUA HATUA ILIYO SAHIHII, EPUKA HOFU AMBAZO HAZIKUSAIDII KWA AFYA YAKO NA KIUMBE UNACHOKITARAJIA!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  pole sana dearest na umenikumbusha mbali sana, nakushauri kuwa mvumilivu ukapime na ukikuta tofauti kaza roho dear, cku hizi kuna kinga za kumkinga mama na mtoto, wahi haraka ku check kwa mara nyingine, ni ngumu lakini inabidi....naku pm kukuelezea kitu.
   
 4. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nasra kwanza pole kwa mawazo na hongera kwani majibu yameonyesha uko salama.
  Kwanza rudi tena clinic pima uwe na uhakika hii ni kwa usalama wako na wa mtoto. kwa kujua status yako itasaidia wauguzi kukupa ushauri unaofaa na dawa kama ikibidi kwa ajili ya kumkinga mtoto wako asipate maambukizi, na pia wakati wa kujifungua watafanya extra care kumkinga mtoto na atapewa dawa. lakini uwezekano wa wewe kutoambukizwa upo kwani mbona kuna watu wanaishi mmoja akiwa positive na wameweza kuwa na mtoto negative?
  Baada ya kujua status yako nivyema kutumia kinga wakati wote utakapokutana na mumeo, na ucje mnyanyapaa mumeo kwani ndoa ni kuvumiliana katika raha na shida. japo umri wako bado mdogo sana kukabiliano na hali hii lakini kadri siku zinavyosonga utaikubali . mjali sana mumeo bse imagine we huna ulivyochanganyikiwa yy ni zaidi anauhitaji upendo wako sana na assuarence from you kwamba maisha bado yapo. bado mnaweza furahia maisha pamoja na ukimwi. Punguza mawazo si mazuri kwa kiumbe huyo uliembeba.
   
 5. N

  Nasra82 Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mpendwa nasubiri hiyo pm! Nawashukuru na wengine wote kwa mawazo yenu
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,056
  Trophy Points: 280
  Pole sana. Tafuta ushauri kwa Wataalam jinsi ya kukabiliana na hali hii. Pia uliza maswali kuhusu kujamiina ndani ya ndoa yako maana mpaka sasa wewe inaelekea uko salama lakini ni lazima uhakikishe unajikinga kwa kila hali ili nawe usiathirike kama mwenzio. Pole sana.
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Pole sana dada. Hakuna tatizo lisilo na njia ya kutokea,Kwa imani yeyote ile ya dini uliyoko nayo au hata kama huamini katika Mungu tafadhali chukua biblia yako soma huu mstari Isaya 45:2
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  HY ndio nini naombeni ufafanuzi mwenzenu kabala sijaanza kuchangia....Kuuliza si uijnga ila nikujifunza..
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mhh na mie nimechanganyikiwa na thread walaaa ckuliona hilo...ka copy mahali.
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  dear hiyo HY ni ki2 gani?
   
 11. N

  Nasra82 Member

  #11
  May 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo HY ni blog inaitwa Harusi yangu, nimeizoea sana ata ukiangalia huku mie ni mgeni sana sasa nimekosea baada ya kuandika JF nimeandika HY poleni kwa usumbufu, sijacopy mahali ni tatizo lililonifika kwaiyo nisaidieni wana JF
   
 12. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  HY = Habari ndio Hiyo!!
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  holalalaaa, sweetheart ningepaliwa ungekiona cha moto, lol
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  eeehh.....
   
 15. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  100% kadesa
   
 16. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Usikonde sweetie, ningekueletea tu kile kinywaji chako ukipendacho!
   
 17. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hahahahaha!!! Utamu wa kudesa unanoga zaidi pale unapojikuta umedesa mpaka jina au namba ya mtihani ya mshkaji.
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kanikatisha tamaa mwenzio....ngoja niishilie hapa.
   
 19. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pole Mama Nasra. Hongera kwa kukuta -ve. MUNGU akujalie na ukipima tena utakuta hivyohivyo. Jipe moyo kwani MUNGU ni mweza wa yote.
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nyamayao ........hakuna atakaedesa na kuja hapa kusema mumewe ana VVU na yeye ana hofu. huyu tatizo analo kweli

  ushauri wangu kwako nasra ni: nendeni nyote wawili mkapime tena (katika hospitali nyengine.........kuna watu ambao wamewahi kupima Aga Khan ikakutikana kumbe ilikosewa, pia namjua mtu alipima muhimbili akaambiwa anao akenda hospitali nyengine kama tatu akaambiwa hana)

  ukishakujua kama mume wako anao na wewe huna ..........hapo kaa chini omba mungu akupe nguvu za kuweza jambo hilo kwanza.

  kisha onana na wataalamu watakupa namna ya kukabiliana na suala hilo
   
Loading...