Nisaidie Maneno haya kwa Kiswahili

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,270
8,032
Wakuu naomba tafsiri (kwa kiswahili) ya maneno/titles hizi:

1- Receptionist
2- Desktop Publisher
3- Programs Intern
 
kiswahili bado hakijakuwa na hakiendani na halihalisi ya utandawazi maneno hayo Desktop publisher na program .... yanatumika kama ya livyo
kiswahili bado hakijajitosheleza misamiati hivyo bado kinakopa/kinaazima maneno kutoka lugha nyingine
 
Si kwamba kiswahili hakijajitosheleza kimsamiati hapana! Na kwa mfano tu ni jambo gani ambalo huwezi kuelezea kwa kukosa msamiati wa kiswahili?

Lugha yeyote duniani iwe na wazungumzaji wengi au wachache ni lazima tu itakopa baadhi ya maneno au misamiati kutoka katika lugha nyingine na hiyo ndiyo desturi ya lugha zote.

Lugha yetu adhimu inayo maneno na msamiati wa kutosha na kujitosheleza na ukiona baadhi ya maneno yanakosa maana usirukie kusema ni ukosefu, neno moja au mawili tu hayafanyi msamiati kutokamilika vivyo hivyo neno moja au mawili hufanya lugha kujiongezea msamiati.

Kumbuka hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya jina na kitu halisi. Mfano. Kikombe kama jina lina uhusiano upi na umbo lake au mwonekano wake? Hivyo tunaweza kugundua kuwa hakuna kitu ambacho kinaweza kukosa jina katika lugha yeyote bali jambo ambalo husubiriwa na wanajamii ni makubaliano na hivyo baadaye neno au jina hilo husanifishwa na kuingizwa katika msamiati wa Lugha husika.

Nimalizia kwa kusisitiza kwamba, lugha zote huwa na tabia ya kukopa toka lugha nyingine na hii ni moja ya njia ya kujiongezea msamiati na sio udhaifu kama wengi wanavyodhani.

Hali kadhalika lazima kuwepo na vikao maalumu ambavyo hupitia maneno kutoka lugha moja kwenda nyingine na kusanifishwa.
 
Mfano rahisi tu ni kwa nini katika Lugha ya kiingereza wameshindwa kutoa tafsiri nzuri ya maneno yafuatayo ya kiswahili?
1. Ugali
2. Makande
3. Mjomba
4. Baba Mdogo
5. Mama Mdogo
6. Kining'ina
7. Mpwa
8. Kilembwe

Maneno au majina hapo juu ukiyasoma katika fasiri ya kiingereza utagundua kwamba lugha yeyote lazima ikope baadhi ya maneno kutoka lugha nyingine na hasa ni kutokana na baadhi ya maneno kutohusiana na lugha husika kiasili au mwenendo, mfano mzuri. Aunt- aweza kuwa ni Shangazi au Mama mdogo katika kiingera, hali ni tofauti ktk Lugha yetu ambapo tuna majina mawili ya kuwatofautisha.

Na ninaweza kukuthibitishia hivi, ukutanapo na mtumizi wa kiingereza akakwambia 'oh! Meet my Aunt' je? Unaweza kutambua huyo ni Shangaziye au Mama yake Mdogo? Hapo ni kazi ''it needs more clarification'' kwa hapa nafkiri tumeelewana kidogo na huo ni mfano wa maneno ya kawaida tu, je tungeingia katika maneno tata/yenye maana zaidi ya moja nafikiri hapo kusingekucha leo.

Nadhani kwa hapo kiasi tunaelewana wandugu au mnasemaje? Penye makosa nisahihisheni.

Eid- Mubarak.
 
ASANTE, upo sahihi, hata hicho kiingereza kimekopa maneno mengi ya kirumi, kiratini na nk.
 
Swahilian nakubaliana nawe kwa uliyoyaandika ila kwenye rangi nyekundu hiyo inaweza kuwa namna moja wapo ya kuchelewesha upanukaji wa lugha. Sina uhakika maneno kama Bongo Fleva, chombeza, powa na mengine yalifanyiwa vikao vya kuridhiwa matumizi yake.

Kwa upande mwingine nionavyo mimi ni kwamba kutokuwepo na waandishi wengi wa vitabu vya lugha ya kiswahili vinavyoelezea mambo mapya yanayojitokeza, mathalan, yanayohusiana na sekta ya TEKNOHAMA kunafanya kiswahili kionekane kuwa na upungufu wa misamiati jambao ambalo siyo kweli. Ukiangalia kwa mfano neno "Desktop" siyo jipwa ila ni muunganisho wa maneno mawili, na kitu ambacho huwa kinafanyika kwenye uandishi ni kwamba ukishatumia neno fulani ambalo ni jipya lina ugumu fulani wewe Mwandishi unalitolea maana ili msomaji aelewe. Kitu ambacho kinaweza kufanyika kwenye kiswahili pia. Mfano wakati Marehemu Nyerere alipoacha uongozi alitumia neno la Kizanaki "Kung'atuka" akimaanisha kuachia ngazi. Neno hili halijkuwepo kwenye misamiati ya kiswahili hapo kabla lakini baada ya hapo linaendelea kutumika. Vivyo hivyo kwa neno "Kihiyo"
 
UOGA WAKO NDO UMASIKINI WAKO !

sidhani kama hii signature iko sahihi kwa matumizi ya hapa bongo labda Ulaya
 
Wakuu naomba tafsiri (kwa kiswahili) ya maneno/titles hizi:

1- Receptionist
2- Desktop Publisher
3- Programs Intern - hii imeandikwa vizuri??

1. mpokea wageni, mpokeaji, mpokezi
2. uchapishaji wa eneokazi
3. ??
 
Mfano rahisi tu ni kwa nini katika Lugha ya kiingereza wameshindwa kutoa tafsiri nzuri ya maneno yafuatayo ya kiswahili?
1. Ugali
2. Makande
....
Nadhani kwa hapo kiasi tunaelewana wandugu au mnasemaje? Penye makosa nisahihisheni.
......

Marhaba Mkuu!
Kwani ndo kiswahili kinalidwa hivyo, na ndivyo kikuavyo pia!
 
Mpwa = N
Mfano rahisi tu ni kwa nini katika Lugha ya kiingereza wameshindwa kutoa tafsiri nzuri ya maneno yafuatayo ya kiswahili?
1. Ugali
2. Makande
3. Mjomba
4. Baba Mdogo
5. Mama Mdogo
6. Kining'ina
7. Mpwa
8. Kilembwe

Maneno au majina hapo juu ukiyasoma katika fasiri ya kiingereza utagundua kwamba lugha yeyote lazima ikope baadhi ya maneno kutoka lugha nyingine na hasa ni kutokana na baadhi ya maneno kutohusiana na lugha husika kiasili au mwenendo, mfano mzuri. Aunt- aweza kuwa ni Shangazi au Mama mdogo katika kiingera, hali ni tofauti ktk Lugha yetu ambapo tuna majina mawili ya kuwatofautisha.

Na ninaweza kukuthibitishia hivi, ukutanapo na mtumizi wa kiingereza akakwambia 'oh! Meet my Aunt' je? Unaweza kutambua huyo ni Shangaziye au Mama yake Mdogo? Hapo ni kazi ''it needs more clarification'' kwa hapa nafkiri tumeelewana kidogo na huo ni mfano wa maneno ya kawaida tu, je tungeingia katika maneno tata/yenye maana zaidi ya moja nafikiri hapo kusingekucha leo.

Nadhani kwa hapo kiasi tunaelewana wandugu au mnasemaje? Penye makosa nisahihisheni.

Eid- Mubarak.

Mpwa = Niece (KE) Nephew (ME)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom