The Angel
Member
- Mar 23, 2012
- 6
- 0
Wana JF
Mimi ni member mpya wa hili jukwaa but am interested with advice na michango mbalimbali ya kimawazo inayotolewa kwenye hili jukwaa.
In short kuna binti mmoja nilimpenda na nilimjua kwa kumuona pale nyumbani kwao.Kilichonivutia zaidi kwake ni kua huyu binti anaonekana ni binti anayejiheshimu na mtulivu.Elimu yake ni form 4. Hata siku moja tangu nimjue mwaka juzi sijawahi kumkuta njiani akizurura bila mpango.Muda mwingi anautumia akiwa nyumbani na anaonekana at least kufuata malezi ya kidini. Nilivutiwa na huyu binti na nikamweka kwenye mipango yangu ya kumuoa.Nilipopata nafasi ndogo ya kuongea naye nilijaribu kumshawishi juu ya hilo kwa muda mrefu lakini alikua hanipi jibu la kueleweka mpaka ikabidi nimtumie mama yake mdogo wanayeishi naye.Mama yake mdogo aliongea naye na binti akanikubalia ombi langu.Na mimi sikufanya ajizi haraka nikapeleka washenga, nikatoa mahari na sasa hivi niko kwenye mpango wa maandalizi ya harusi.
Tatizo langu ni kua huyu binti anamsikiliza sana huyo mama yake mdogo. Alimkataza asimiliki simu na anamkataza asifanye mawasiliano yoyote na mimi mpaka niombe ruhusa kutoka kwake. Nilikua natamani kua na mawasiliano na yeye ili at least niweze kujua ni aina gani ya mwanamke ninayetarajia kumuoa lakini imekua ngumu.
Issue hapa ni je itakuwaje nikimuoa huyu mwanamke then nikagundua kua hana zile tabia nilizokua nazifikiria? Na je nisahihi kwa mzazi kuendelea kumbana sana msichana ambaye tayari umeshamtolea mahari?
Naombeni ushauri kabla sijaamua navyofikiria mimi.