Nisababu zipi zilizo sababisha kufungwa kwa kiwanda cha GENERAL TYRE??

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Hivi nini kilisababisha kiwanda cha General Tyre kufungwa wakati kilikuwa kiwanda bora East Africa??au Wakenya walituhujumu??na lebo yao ya YANNA??
 
Hivi nini kilisababisha kiwanda cha General Tyre kufungwa wakati kilikuwa kiwanda bora East Africa??au Wakenya walituhujumu??na lebo yao ya YANNA??

Nnachosikitika ni kwamba mada hii hatakuwa na mvuto kwa wengi...lakini maswala kama haya ni ya msingi sana kujadiliwa humu jamvini.
Ndugu yangu viwanda vyetu vingi sana vimefungwa na hili lina madhara makubwa kwa uchumi wetu. Jiulize ya DOWICO, Tanganyika packers, NMC.....yaani sijui tunaelekea wapi..Ikumbukwe kwamba mwaka 1976 sekta ya viwanda ilichangia asilimia 13 ya pato ghafi la taifa(GDP) na miaka 30 baadae 2007 ilikuwa 8.7 asilimia.

Ni namna gani tunaweza kuifufua hii sekta inayotegemewa sana na kilimo na sekta nyingine? wadau leteni mawazo tujenge nchi yetu.
 
Nimepita hapo leo nikauliza swali hili hili....kuna viwanda vingi tu...Kuna Tanzania Litho, Kiltex, Kile kiwanda cha biskuti na kile cha Kiko....hivi vyote vipo sehemu moja lakini ni magofu sasa. kile cha biskuti kimekuwa kanisa ...sijui huu ndio uwekezaji mpya wa kisasa?....hebu wachumi tufungueni macho
 
Kuna kundi la mafisadi wanataka wajiuzie kwa bei poa.

hata mimi nimesikia hivyo hasa hicho cha General Tyre....nikajiuliza....watamiliki nchi nzima coz kuna mmoja nasikia ndio kinara, sasa huyu atakuwa anamiliki hii nchi......?
 
Halafu cha ajabu kimedumu kipindi soko ni dogo yaani magari Machache na kufa kipindi ambacho wamiliki a magari ni wengi mno hivyo soko ni la uhakika.
 
Back
Top Bottom