Nipo tayari kwa kazi yoyote iliyo halali jamani

EveningStar

JF-Expert Member
Nov 14, 2018
262
162
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Nimeangaika kutafuta kazi kwa muda mrefu sana pasipo kupata mafanikio yoyote yale na muda unazidi kwenda, yaani hapa nilipo sina mahali pakuishi nimehifadhiwa tu kwa ndugu na ninalala ukumbini, kula yangu imekuwa ya tabu sana. Nimepeleka nyaraka zangu sehemu mbalimbali hasa viwandani hapa DSM lakini hawajanibu chochote na muda unaenda.

Hapa kwa ndugu nilipo wameshanichoka japokuwa nalala ukumbini lakini wanataka kunifukuza yaani nina hali mbaya sana jamani. Kwahiyo naomba kwa yeyote yule mwenye kazi au mwenye kuweza kuniunganisha nq kazi usisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, mimi sichagui kazi na nipo tayari kufanya kazi yoyote ili mradi iwe halali tu mimi nitaifanya. Nisaidieni jamani maana niko kwenye hali mbaya sana jamani. Mimi nipo Dar es salaam.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom