G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Rais Magufuli tangia akiwa waziri wa ardhi na nyumba, ujenzi na hatimaye uvuvi kabla ya kurudi tena ujenzi, hajawahi kamwe kufanya maamuzi magumu na hatimaye yakafanikiwa. Katika enzi hizo Kikwete ndiye alikuwa mhimili wake mkuu na chombo kikuu cha kumuongoza.
Rais Magufuli ndiye pekee waziri ambaye viongozi wake wakuu (waziri mkuu na baadaye rais mwenyewe enzi hizo akiwa waziri ) walitoka hadharani na kumkosoa mbele ya umati kwa matendo yake ya pupa, hasira na chuki. Hili kwangu lilikuwa jambo la kushtua.
Lakini nilishtuka zaidi pale nilipolala nikaota kuwa Magufuli ndiye rais wa Tanzania. Nilishtuka tena zaidi pale nilipoamka na kukuta ndoto yangu niliyoota kumbe lilikuwa ni jambo la "live" Magufuli sasa ndiye rais wa Tanzania.
Kwa dhati kabisa naunga mkono kuwa mikataba ya madini waliyoingia Chenge na Mkapa ilikuwa mibovu sana. Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, viwanda vya serikali waliofanya Chenge na Mkapa ulitia aibu taifa. Mwaka 1997-98 ulikuwa mwaka wa laana kwa Tanzania. Kiwanda kikubwa chenye eneo kubwa na mashine za kisasa kama TPI kuuzwa milioni kadhaa za kitanzania ni uwenda wazimu wa aina yake!
Tukio la jana: Hili ni tukio ambalo litaleta "total failure" kwa rais Magufuli na watanzania. Pengine litakuwa tukio tutakalokuja kukumbuka huko baaday kama tunavyokumbuka leo ya mwaka 1997-98.
Jambo linalofanywa na mtu mmoja (kama Magufuli) ama watu wawili (kama Chenge na Mkapa) nje ya mamilioni ya wataalamu ni la kuogopwa sana! Siyo jambo sahihi katika tu mwanzo wake.
Jana nilimsikia Profesa Mruma akisoma ripoti yake kwa hasira nikajiuliza, huyu si anasoma Alichofanyia utafiti? Hasira za nini? Nikamsikia Magufuli akitamka maneno "Upumbavu" na "Profesa Muhongo, profesa mwenzako ameku-prove wrong" Kisha nikamfananisha na Mruma nikajikuta nikisema mbona kama Magufuli amemteua mtu wa aina yake kwenye hili? Tutaupata ukweli na uhalisia?
Hatimaye haraka haraka Muhongo akaliwa kichwa na watendaji wengine. Hilo kwangu siyo shida.
Shida yangu ni je documents halali ambazo copies zake zipo kwa wanasheria na mahakama za kimataifa zinasemaje? Hawa wawekezaji wanafuata sheria zipi kwenye hayo mambo?
Kuna wakati nilimsikia rais Magufuli akisema kuwa hawa wawekezaji wakishachukua mchanga wanaenda kuwauzia wenye Smelters kisha wao biashara yao inaishia hapo? Kiongozi mkuu kuongea jambo ni lazima uwe na documents halali za kukupa support. Je Magufuli anazo?
Rais Magufuli ajue kuwa, na awe makini sana kuwa, sasa yeye ni kiongozi na atakaloongea ama kufanya anafanya kama kiongozi. Asije akadhani kuwa ataharibu kisha atokee Kikwete mwingine wa kumrekebisha. Akishaharibu yeye ni Tanzania imeharibu. Leo tunalia juu ya Bilionea Chenge na Mkapa. Tusije baadaye tukalia tena juu ya Magufuli na Masaju!
Zipo taarifa kuwa Muhongo alimuelekeza rais Magufuli ukweli wote kuhusu hili sakata la mchanga na madini. Akampa paka sheria zinazotubana pia akamtahadharisha tutakapokwamia endapo kama tutaamua kama tulivyokuwa jana. Lakini baadaye Mruma akaipindua akili ya Magufuli na ndipo ikawa vile.
Mimi huwa naamini kuwa jambo lolote lile linalofanya na mtu mmoja nje ya wataalamu mamilioni kwa mamilioni kama alichofanya Magufuli siyo jambo sahihi. Jambo lolote lile linalofanywa na watu wawili kama alivyofanya Mkapa na Chenge siyo jambo sahihi. Ndio maana kukawepo na bunge. Hilo ndilo hasa linaloweza kuja na jambo sahihi kwakuwa linahusisha mijadala huru. Bunge ndiyo mwanzo wa kila kitu.
Huko kwingine hata sikuamini. Naisubiri kwa hamu ripoti ya bunge juu ya hili. Ninaunga mkono kuwa Mkapa na Chenge walituletea janga na hata jana nilisema hilo kuwa kwa Magufuli ninachounga mkono ni kuwajibishwa kwa Mkapa na Chenge watueleze ni kwa nini aliamua hivyo. La jana bado nalitafakari ila nikitambua kuwa Magufuli huyu tuliye naye leo ndiye yule waziri wa jana.
Umakini mkubwa juu ya maamuzi yake ni lazima uhitajike na hasa tukiielewa vyema historia yake ya pupa na hasira. Kazi ni yetu sisi wa Tanzania kwakuwa Magufuli atapita kama alivyopita Mkapa aliyesifiwa kipindi hicho na sasa analaumiwa kweli kweli. Chanzo ni maamuzi ya akili moja! Bunge likiwekwa kando ni lazima ukwame tu.