Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Hayo matumizi mbona yapo juu sana mkuu, unataka ununue vitu vyote kama unaishi na demu babu.

Deile nunua visamaki vya buku vile au misumari (dagaa), nyanya. Monthly nunua kitunguu, mafuta na unga wa ugali tu. Hivyo ndio masela tunavyoishi!

Sasa we unataka ununue hadi hoho,binzari, letuce,gilgilani magetoni!? Utakwama tu!!!
Watoto wa kishua hao. Hawajuhi hizo mambo venyewe sisi hufanya huku magetoni.
 
Weka utaratibu huu natumaini unalo fridge

Mchele kg 10 (16,000 - 22,000) - humalizi kwa mwezi

Samaki sato kg 2 (20,000)-utagawa kwa siku 4 (funga separate)

Nyama kg 2 (12,000) - siku 8 (1/4
Kg kwa siku)

Kuku 2 (15,000) - siku 4 (1/4 per day)
Nyanya sado 1 (4000-5000)

Vitunguu sado 1 (3000)

Bamia, hoho, karoti - (6,000)

Mafuta lita 3 - (17,000)

Tambi 2 (3000)

Unga kilo 5 - (10,000)

Maharage kilo 2 - 4000

Viazi ndoo ndogo - 7000

Na vingine vidogo vidogo - 15,000

Jaza fridge lako hapo unatoboa mwezi hayo mengineyo akili kumkichwa

Hapo bajeti yako ni laki 1 na 39, hujaweka sadaka, ndugu na mavazi kama alivyoyataja na hivyo ndio viko mkasi kweli.
Lakini pia hivyo vyakula ukivimaliza kwa wiki moja ndani ya miezi sita utaugua maana ni vingi sana.
 
mzee punguza vitu visivyo na msing kisha save money
hapo kwenye sadaka navojuaga ni utoe kile ulicho nacho. na inaonekana
wew ni muumin wa manabii wa zama hizi. sio mbaya
we cha kufanya uwe una beba pesa ya kukutoha usafiri mpaka church na kurudi na buku la sadaka pesa ingine iache home. kaza moyo ndugu .
ile chenji ya sadaka anzisha hata kamradi kadogo yani uwe unaingiza pesa sasa au vp
kamradi kanaweza kuwa ka buku teni au chini au juu kidogo ili mradi baada ya kutumia pesa nyingine ziwe zinaigia au vp jmaa
 
hivi tango sio tunda !???

Anyway, ongezea na maji ya kunywa 97,000 na juice 89,000 , pia kuweka bajeti ya nguo bila viatu sio poa, vuta hata sneaker moja ya 73,000
Safi braza.... Dawa ya mjinga ni kuumia tu.

Aliyepotea mpoteze zaid asirudi teena.

Unatoa sadaka 75 unakuja kuomba ushauri... Akamuombe askofu wa jimbo anayempa ulaji.
 
Ngoja na mimi nianze kuandika kuanzia tarehe 8 nione natumia kiasi gani kwa wiki
 
Back
Top Bottom