Nipo njia ya panda, Japan..............dah! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nipo njia ya panda, Japan..............dah!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by ggg, Nov 24, 2010.

 1. ggg

  ggg Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani nipo njia ya panda.Kuna full sponsoreship kwenda kusoma masters Japan, course: Nucleur Enginering, mmi nime graduate pale udsm, Electro-mechanical engineering, NILIMALIZA MWAKA JANA, nafanya kazi nalipwa 600,000/= kwa mwezi. nahisi kwenda huko ni kupoteza muda kulingana na hali harisi ya tanzania kwenye sector ya nucleur, naomba michango yenu. Program inaanza mwakani october.mchakato wa kuwa enrolled mwisho ni december 10, 2010.Wasiwasi wangu ni kwenye ajira. Nifungueni macho jamani kama yamefumba
   
 2. l

  len Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  hongera sana kwa kupata nafasi hiyo. mimi nakushauri usiangalie hali ya sasa ya hapa kwetu, jaribu kufocus miaka kadhaa ijayo. unaweza ukawa miongoni wa wataalamu wa mwanzo kabisa wa nuclear hapa tz. na pia unaweza ukapata opportunity kufanya kazi nje ya nchi. Lakini zaidi sana inategemea malengo yako, finally unataka kufanya nini.
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Kuna wengi sana wamesoma na hawapo nchini.................. NENDA KASOME Tshs. 600,000/= si kiasi cha kutaja, ni kdogo mno. Inaonekana unajilinganisha na WALIMU WA JK....!!!!

  SWALI KWAKO.................. kinachokufanya usite ni hizo Tshs. 600,000/= au hali harisi ya Tanzania kwenye sector ya nucleur..????
   
 4. R

  Renegade JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Nenda shule Kijana, Usawa huu ukipata full sponsorship unaanza Haraka, Ondoa Hofu Si unajua nini kinakuja baadaye? In the future kuna uwezekano wa kuwa na Nuclear Power plants katika nchi yetu, Opportunity ni nyingi, usiogope.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kama tayari unahisi ni kupoteza muda basi itakuwa ni kupoteza muda kweli, by the way Tshs 600,000 si ni kama $400? duh!!!!!!!!, kodi ya nyumba ya wiki. Mimi nakushauri usiende kwa sasa maana wenzio wanaotafuta nafasi kama hizi huwa hawajiulizi mara mbili mbili. Kusoma sio lazima uajirriwe na ajira si Tanzania tu mkuu!!!!! Fanya research na next time jaribu!
   
 6. ggg

  ggg Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hali harisi tanzania kwenye sector ya nucleur, ajira ni finyu.nioneshe mbele mkuu.
   
 7. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tanzania todate ina migodi zidi ya mitatu ya Uranium,Isitoshe ukimaliza shule unaweza ajiriwa South Africa na kwingineko.Nucleur is thing of the Future kaka wewe laza Damu utajijutia.
  Dr Bialali Prof Kandoro wa Dar es salaam Technical college wenzako wanapeta
   
 8. K

  KIBE JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ni mfatiliiaji wa mambo zamani safari ya kutoka dar kwenda lindi au mtwara ulikuwa unatumia siku 7 naa ndo ufike kusini lakini now days ni one day umetia timu. Maana yangu hapo ni kwamba dunia inabadilika siku hazi siku na tunako kwenda mbele huko vyanzo vikuu vya umeme hususani maji vinakwenda kufa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mvua zinakosekana ,kwa hiyo vyanzo ambavyo vitatumika miaka ijayo moja wapo ni nuclear ,na hata kama hutapata kazi tanzania hata ughaibuni utakula shavu tuuuuuu nenda kapige shule kijana achana na hako kamshahara kako laki 6.
  Upo hapo.
   
 9. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nenda kasome kijana huko unaweza kupata mitandfao mingine using'ang'anie ajira.
   
 10. mutisya mutambu

  mutisya mutambu Senior Member

  #10
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 165
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kasome bwana achana na hizo njuruku chache,unazijari kwani kwenye masters utatumia pesa ,si ni full
  scholarship,shida iko wapi? hata hivyo rafiki,usiuweke mtazamo wako kwenye mipaka ya kupata kazi ndani
  ya nchi hii,hapo naona umejifunga kwenye boksi,kasome kwa level za kupata kazi kimataifa,ikitokea tanzania
  ukitaka,utakuwa na uwanja mpana wa kupata,maana utakuwa level za juu zaidi,kama chance ipo fight kasome,pesa
  hiyo isikukwamishe lolote
   
 11. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  tafadhali sana usiachie hiyo nenda kasome. tanzania tuna uranium na kuna habari kuanzishwa mitambo ya umeme wa nuclear. vilevile utahitajiwa pia na nchi nyingine.
   
 12. S

  Sophia New Member

  #12
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very Simple Calculation: Mshahara wako ni 600,000. Full sponsorship inainclude pocket money/ stipend. How much per month? Am sure it will be more or almost equal to your Salary. Fanya kama unaenda kazini na Stipend utakayokua unapata iligard kama ndiyo your current Salary. Mwisho wa siku utapata na cheti/ kichwa kitakuwa safi na utakuwa umesafisha macho. How do you see this?

  Nenda shule ndugu. 600,000 ni nini ikuchanganye?

  Thanks,
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  I could say something about "products of UDSM" here, but that would just not be graceful.

  Usipoenda utaijutia sana hii nafasi baadaye.

  Tanzania hatujui baadaye kutakuwaje. Kwani ni lazima kufanya kazi Tanzania?

  By the way unajua Makamu wa Rais wako amesoma nini? Nuclear Physics, sasa angalia alichosoma na anachofanya.

  Kuna asasi nyingi zitakuja katika mambo ya nishati, na hata kama hufanyi kazi katika nuclear plant kwa sababu hatuna, unaweza kuwa mshauri au hata mwalimu katika ngazi yako.
   
 14. M

  Mnyalu wa Kweli JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kaka wajapan wakiku-sponsor course huwa si wababaishaji, nilikuwa huko kwa short course ( full sponsorship) na wanakupa na hela ya kujikimu. Japo Tokyo is the most expensive city in the world you will be able to save and also come back with something very important in your life -education. Go, Go, Go kijana, Go. Usiachie nafasu hiyo. Wengi wanazililia opportunities kama hizo.
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Kasome.......kazi si lazima ufanye TZ............ Huoni Dr. Bilali ni mtaalamu wa nyuklia..lakini ni makamu wa raisi........???
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu ulikuwa huna haja hata ya kuuliza mkuu nenda kasome, uranium ipo unaweza kuleta wazo jipya kwa maendeleo ya taifa hili. tunahitaji umeme tena sana tuu.
   
 17. I

  Iyankala Member

  #17
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3

  Kwa Upande wa taaluma hiyo, Japan ipo vizuri. Kuhusu application ya hiyo taaluma TZ ona mfano huu, hapa South Japan wapo wa- TZ wengi tu wanasoma mambo mbalimbali kuhusu Molecular Biology katika levels za Masters and PhD, nimehudhuria majumuiko mbalimbali ya kitaaluma juu ya aina ya tafiti na maendeleo ktk fani hiyo, ukilinganisha na nyumbani TZ application kwa sasa unawezakuona hakuna. Lakini kumbuka dunia yabadilika kwa kasi sana kiteknolojia na TZ sio kisiwa, hasa ukizingatia rasilimali zilizopo zinazoweza kuhusika na nuclear. Kusomea fani hiyo itakuwa ni investment nzuri kwa Human resourse ya TZ (kufikiri kizalendo). Tena iwapo ufadhili wako ni kupitia wizara ya elimu ya Japan (Mombukagusho) mara nyingi huwa ni toka Masters mpaka PhD japo mwaka huu masharti yamebadilika kidogo sana, japo yategemea iwapo wewe mwenyewe utakuwa tayari kuendelea na PhD.

  Kuhusu kazi: Ni kweli ni vema kuwa na mahali pa kujishikiza, lakini kumbuka kuwa muda mfupi tu uliopita kwa mfano katika serikali watu wenye taaluma ndogo waliweza kufanya kazi serikalini. Sera utumishi zabadilika na sasa qualifications sio za kuajiriwa tu bali hata za kupanda cheo zinategemea hasa kiwango cha elimu/taaluma pamoja na mambo mengine. Kwa uzoefu nilionao, first degree haina nafasi kwa miaka michache ijayo, unless unakubali kubaki kada ya chini ya utumishi. Naomba unielewe vema hapa, bado nchi nahitaji wataalamu wengi kujitosheleza hata at diploma level, but their performance will be limited kutegemeana na viwango vya elimu na taaluma. Soon with a first degree you can not compete with others, in addition to that, if you are interested to become a good performer, you need tools;taaluma. Kwa uzoefu wangu wa miaka 19 kazini, jambo hili limesababisha vijana wengi walio katika ajira kuwahi masomoni kungali mapema, Thank God you have full Scholarship (very rare for majorities).
  Mimi nakushauri ukasome, but mwamuzi wa mwiso ni wewe. Pima mambo vizuri, anagalia malengo yako, Some questions: unaelekea wapi, utafikaje unakoenda, Kuna faida gani na hasara gani kwa uamuzi utakaofanya leo, fanya Cost/benefit analysis ya choices zote mbili while taking into consideration the Total Opportunity Cost of the foregone choice, nikimaanisha kwa sasa na kwa future, then angalia amani ya moyo wako.
  Ukipenda naweza kukueleza roughly the basic living costs kwa mwanafunzi foreigner hapa Japan, ambazo estimates zake ni zinaendana sana na viwango vya scholarships za Mombukagusho kwa Masters na kwa PhD. You can comapre and may be it may add to your inputs to make decisions. If U` R` interested unaweza kunitumia PM.
   
 18. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  uhhh, nenda, najua kuna wkati mwingine mtu kwelu unachanganyikiwa na kitu kidogo sana, mpaka ucikie kutoka kwa mtu mwingine anacemaje. Huu ni uamuzi mzuri uliochukuwa wa kujiachia hapa jukwaani. Okay brother, watu wengi wametia maoni yako mazuri sana hapa, haku aubishi kuwa umeshachukuwa uamuzi sasa.
  La kwangu ni kuwa walichosema wengi hapa mm pia nawapa sapot kubwa, nenda shule bana...... hela hela kitu gani 600,000/-? naisi ndo kazi yako ya kwanza na uliipata kwa tabu, najua ilivyo tuwa tabu kuipata.... have 5yrs focus then diside who would u like to become? Kapige shule kama unataka kuwa mtaalam wa manyuklia mtusaidie watanzania
  Unajua ndo maana migodi mingi ilivyoanzishwa kulikuwa na hakuna watallam wa kutosha, na wengi walitoka nje ya TZ, sasa wewe baba tunakuhitaji kwanye migodi yetu mipya

  Kila la heri bana
   
 19. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kwani kazi lazima ufanye hapa Bongo?
  Ulaya na kwenyewe kunaweza kuwa kazini kwako pia
   
 20. R

  RUSESABAGINA Member

  #20
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa sasa usifikirie swala la ajira,kabla ya kumaliza hiyo degree ya kwanza ulijua utafanya wapi kazi? sidhani kama ulijua
  Au kuna watu wangapi hawana kazi na wanaproffesions ambazo ni marketable kwa sasa hivi...wanazunguka tu mtaani
  Kapige shule na ukiweza kuwashangaza wajapan kwa perfomance nzuri you may get a PHD scolarship too...
  All the best
   
Loading...