Nipo njia panda kuhusu kuendelea kuishi ghetto. Ushauri wenu unaitajika

nyasangaboy

Senior Member
Jul 14, 2020
127
58
Habari zenu wadau, nilikuwa naomba ushauri kutoka kwenu wadau ni hivi ninapoishi kodi yangu inakaribia kuisha nataka kurudi nyumbani kwa mzee. Na sababu ya kutaka kurudi nyumbani na kuacha kupanga kwa sababu ya kutokuwa na kazi kwa sasa so hela ya kodi sina.

Lakini girlfriend wangu amekataa nisirudi nyumbani niendelee kupanga yeye atanisaidia Kodi, so nilikuwa naomba ushauri niendelee kuisha kwa kulinga unga ghetto au nirudi tu nyumbani nikajipange upya.
 
Ukirudi tu home ndio imetoka hiyo,utarudi home mara ngapi? ina maana kila utakapokua unakwama solution ni kurudi home? Pambana na una bahati ya kumpata GF mwenye ushirikiano,ingekua mwingine angesha kukimbia,ila kama alivyoshauri mdau hapo juu,usije kumtupa huyo GF wako.
 
Shukuru Mungu umepata mwanamke anayejitambua. Unarudi nyumbani kufanya nini? Kumbuka hata baba yako na mama yako walipitia changamoto hizi lakini wakakaza na hawakutaka kurudi nyumbani, walikopa na kufanya kazi zozote ili wapate ridhiki kipindi hicho cha hali ngumu na kilipita.
Baki kwenye gheto lako na fanya kazi yoyote ile inayokuja mbele yako. Hakuna pesa inayopatikana kirahisi kwahiyo ni kupambana tu.
 
Hongera sana kwa huyo GF wako kwanza anakupenda sana
Jitahidi ukomae mjini jishulishe kwa lolote kodi ikishalipwa mengine yatapatikana.

once again mpende sana GF wako kwani anakupenda kitendo cha kumwambia unarudi nyumbani kilitosha kukukimbia. Maana unajiuliza changamoto kidogo unataka kurudi nyumbani what if wazazi wako hawapo hapa mjini? Komaa ushakuwa mkubwa
 
Ukirudi tu, umeisha. Endelea kuwa mario tu, manzi akulipie kodi. Ila usije ukamtupa ikiwezekana oa huyo huyo. An future plans na mipango mema na wewe
Sio kwamba naishi Naye hapana nipo mwenyewe na kazi sina kwa sasa so naona mwanzo wa stress
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom