Nipo mbioni kuishtaki Jamhuri dhidi ya Jeshi (Tanpol), watu wasijulikana na kauli tata za viongozi wetu

Noel france

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
980
1,000
Wanajukwa habari zenu! Naomba niende moja Kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Kwa mujibu wa mambo yanavyo kwenda,hususani kwenye kesi ya msingi ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa upinzani. Kunavitu vimebainika na baadhi ya watu wameanza kusema na kuhoji mambo mengi sana. Kuhusiana na heshma na hadhi ya Jeshi letu la polisi kama kweli linatumika kisiasa ama la!

Kiukweli Jeshi letu la polisi linatumika vibaya kisiasa kwania la kudhofisha vyama vya upinzani nchini, haya ni maoni yangu kutokana na Mambo yanavyo endelea kule kwenye muhimili mwingine wa Dola. Nimebaini watuhumiwa wanateswa wakiwa chini ya polisi.

Watu wasio julikana. Kwa mujibu wa mambo yanavyo endelea Kule mwenye mhimili mwingine wa Dola watuhumiwa wanathibisha waliteswa Kwa staili moja kama tulivyokwisha kuwahoji wahanga wengine kama vile Dr. Ulimboka, Mdude Nyangari, Nay wa mitego, Roma Mkatoriki hadi amefika hatua ya kukimbia kwenda kuishi ughaibuni na wengine wengi siwaongelei waliopo mahakamani Kwa Sasa kutokana na kesi inayoendelea lakini na wao wanathibisha wametendwa kama watangulizi wao ambayo ni wahanga.

Kauli tata za viongozi, viongozi watia kauli tata zenye ukakasi ambazo zinasababisha tuhisi wanapanga wao matukio ya kuwadhulu wenzao Kisha kunawatu wanakuja kufanya yanayowezekana kuhalalisha hatia dhidi ya mpinzani wa kiongozi,Kwa kuwapatia kesi za kutunga, kuwalazimisha kukubali kubambikiziwa kesi za uongo ili takwa la kiongozi flani liweze kufanikiwa hata kama Kwa kupigwa.

Dhumuni la kufunguliwa kesi Jamhuli sina Imani na serikali yangu dhidi wananchi wake. Wananchi tunahifu hatuba Imani na Jeshi la polisi Kwa kujihusi na kutumika kisiasa na chama tawala. Usalama wa taifa umekaa kimya huku Amani,hofu na upendo pamoja na mshikamano wa kitaifa ukipotea Kwa wananchi.

Usalama wa taifa umefumba macho na masiko upo busy na usalama wa chama flani ambacho Kimeshika hatamu za uongozi nchini. Wananchi wanapotea na hakuna hatua zinazochukuliwa, Kwa mfano mzuri mwasiasa Ben saanane,pia mwandishi wa habari za uchunguzi Nzori na wengine wengi.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha na kuomba ushirikiano wa mawazo ili kutimiza lengo langu. Asanteni sana mungu awabariki.
 

Noel france

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
980
1,000
Angalia njia ya kutumia ili wale ambao wapo mahabusu wanaendelea na kipigo wasipotee moja kwa moja.
Kiukweli,kupitia kesi inayoendelea kwanza imenifanya nione serikali inawatesa wananchi wake pia serikali inawachukua wale wote wenye Muonekano wa kuwakosoa wako tayari kukupoteza Kwa kivuli cha watu wasiyojulikana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom