Nipo kwenye ndoa, mume wangu hataki watoto hivyo nikipata mimba natoa kulinda ndoa yangu

User2020

Member
Jun 17, 2020
7
17
Mimi nimeolewa nina karibia miaka miwli, sasa mume wangu hataki watoto. Nimebeba mimba tatu na zote amesema hataki na ikabidi nitoe kwa sababu ya upendo na upuuzi wangu.

Sababu anazotoa ni kwamba bado hajajipanga kimaisha, na tuna maisha ya kawaida ambayo tunaweza kabisa kumudu gharama zote za mtoto.

Je, ni sawa?
 
Umebakiza nafasi moja tu, Ikitokea umebeba mimba nyingine halafu ukatoa kuna uwezekano usipate mimba tena maishani mwako

Huyo Mumeo ni upumbavu sana, (Samahani kwa neno hili, sina Neno naloona anastahili) Kitendo cha kuoa tu basi hapo unakuwa tayari umejipanga kwa ajili ya familia,

Kaa nae au jaribu kushirikisha ndugu zake anao heshimiana nao muone kama mnaweza ki solve
 
Pole sana lakini inashangaza

1. Kama alikuwa hataki watoto kwa nini alioa?

2. Kama alikuwa hataki watoto kwa nini msifunge vizazi au kutumia njia za uzazi wa mpango kuliko "kutoa mimba" kitendo ambacho ni "uuaji".

3. Mnaamini katika Mungu ama dini gani mpaka kufikia kukubaliana katika mashauri ya namna hiyo?

Uzuri ni kwamba umetambua kuwa mume wako ana matatizo. Epuka kushiriki hayo mambo, ni vyema uvunje ndoa kuliko kuendelea kushiriki dhambi hiyo mbaya.
 
Sasa mmeoana ili Muwe mnapiganaa mitii tu??? Sasa kama ndo hivyoo fungaa kizazii sio huo upuuzi mnaofanyaaa utakuja kutaka mtoto siku ukoseee.. Alafu huyo mumeo itakuwa na uchawii anaoo yani ndoa mmefunga alafu hamna hata mtoto ukipata mimba anakwambia Utoee. Kama kuna kifungo kinachowatesa wanawake duniani ni NDOAA
 
Pole sana lakini inashangaza

1. Kama alikuwa hataki watoto kwa nini alioa?

2. Kama alikuwa hataki watoto kwa nini msifunge vizazi au kutumia njia za uzazi wa mpango kuliko "kutoa mimba" kitendo ambacho ni "uuaji".

3. Mnaamini katika Mungu ama dini gani mpaka kufikia kukubaliana katika mashauri ya namna hiyo?

Uzuri ni kwamba umetambua kuwa mume wako ana matatizo. Epuka kushiriki hayo mambo, ni vyema uvunje ndoa kuliko kuendelea kushiriki dhambi hiyo mbaya.
Umemaliza mkuu..
 
Huyo ni mume wako wa ndoa?

Kama jibu ni ndio, basi tambua wazi kwamba tayari mna watoto, ingawa wewe na mumeo sasa ni wazazi wa marehemu watoto watatu.

And last but not least, nyote mnatakiea mshitakiwe kwa kosa la mauaji ya watoto watatu wasio na hatia.
 
Na ujiandae kua mgumba atakapo hitaji kuzaa na ww wakati huo kizazi kilisha legea atakuacha na kukusimanga huzai jiandae kwa hilo na atakufukuza huyo mumeo sio mtu mzuri
 
Back
Top Bottom