binam0
Member
- Dec 31, 2017
- 7
- 4
Hodi wadau wa JF. Nami nimekuja hapa kwa mara ya kwanza nikiomba ushauri.
Nimepata mpenzi mwaka jana mwishoni mwa mwaka (penzi letu bado changa kama miezi 3). Tumebaatika kupendana sana kwa dhati japo changamoto ni kila kukicha. Tatizo kubwa ni umbali (long distance relationship) kati yetu kitu ambacho kina challenge sana uaminifu wetu.
Tuna malengo ya maisha ya ndoa hapo baadae na tunaheshimiana sana. Yupo kwenye himaya yangu na familia yake na baadhi ya ndugu wakaribi wanajua yupo katika matunzo yangu japokua bado sijajitambulisha kwao rasmi. Namgharamikia matunzo yake yote na hakosi kitu kutoka kwangu.
Hivi karibuni amepata mashosti na tabia zao sijazipenda kwani naogopa watampotosha na tayari wameshaanza kumshawishi vibaya. Wasiwasi wangu ni kwamba nisipolishughulikia hili jambo tunaweza pishana na penzi likafa.
Tumeshapitia mambo mengi sana katika muda huu mfupi na kinachotusaidia ni kwamba tunaupendo wa dhati na tayari tunamalengo. Changamoto bado ni nyingi lakini ukweli utabaki palepale kuwa nipo mbali naye na naogopa hao marafiki watampotosha. Natarajia kuitwa baba (bado ni siri yetu) kwa hiyo nisingependa tugombane ukizingatia mtoto yupo njiani atahitaji matunzo yetu sote.
tumepishana kwenye:-
Dini ( Dini zetu tofauti)
Age (5yrs+ age difference, nimemzidi kiumri)
Elimu (mimi ni Graduate na yeye kaishia secondary school)
Nataka kurudi nyumbani ili tuwe wote lakini kwa sasa ni ngumu kwa sababu bado nachuma chuma kwa ajili yetu hapo baadae. Na tulishaongea kuwa ndani ya mwaka nitarudi lakini kasi ya hao mashosti inanipa wakati mgumu sana.
Nimeelezea juu juu tu ili mpate picha kamili lakini napitia wakati mgumu sana kwa kipindi hichi maishani mwangu. Ningeshukuru sana mawazo yenu manake kwa sasa nipo kivyangu vyangu hata wakumshirikisha nipate ushauri simuoni. Naogopa kufanya maamuzi yakaja niponza baade nifeli kote.