Nipo katika kazi ya kubembeleza; Ni yule rafiki yangu msomi aliyemkataa mke asiyemsomi

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
3,030
3,324
Wakuu habari,

Wasomi wa kiume wa siku hizi wanajifanya wapo selective sana katika suala la wake wa kuoa. Wengi hutamani kuoa wake wasomi kama wao na kudhani kuwa, kufanya hivyo ndipo kutawapunguzia mzigo wa majukumu.

Ikumbukwe kwamba, nilishapandisha uzi hapa jamvini kuelezea jinsi rafiki yangu(msomi wa degree) wa karibu alivyokuwa akisita kumwoa binti mrembo (mwenye elimu ya form 4 asiye na kazi).
Mke asiye msomi na asiye na kazi ni mzigo?

Jamaa nilimshauri sana amuoe huyo mrembo hadi nikamwonyesha ule ushauri wenu humu jukwaani but akawa anasua sua. Mwanamke alimuuliza kila mara kama ana nia ya kumwoa kweli but jamaa akawa hajibu majibu yaliyonyooka.

Mwanamke akaona msela hana mwelekeo na last week kuna jamaa mfanyabiashara wa vipodozi vya jumla Kariakoo kaenda kumvisha yule dada pete ya uchumba.

Msela ndiyo anahuzunika balaa hadi kazi hawezi kufanya. Anabaki akimwapiza yule dada na kusema kuwa hamwombei mazuri kwenye ndoa atakayoifunga na huyo mfanyabiashara.

Imebidi nichukue time yangu nimbembeleze msela na nijifanye niko upande wake maana mwanzo nilianza kumcheka kanyang'anywa mrembo alikua very stressed nikaona asijefanya maamuzi mabaya bure.

Jamaa hapa anasema kila saa hatokaa apende tena
 
Kwa tafsiri yeyote ile nitasema jamaa yako "Hajui anataka nini" laiti kama angelikua anajua anachotaka "angeshatoa maamuz" either kumwoa au kutooa huyo mrembo, lengo lake ni kuoa "Msomi" mwenzie, kinacho mfanya achanganyikiwe n nini kama huyu mrembo hana hvyo vigezo vya hiyo "elimu" ?? mwambie aache kuweka vigezo vya kijinga, Wakati mwingine tunajikuta tunampangia Mungu hivi hivi, unaoa mtu ndoa inakua ndoano ni timbwili mtindo mmoja, Bible inasema "Mke Mwema ni nani awezae kumwona" Mungu hakuumba Adamu pekee, alimuumba Hawa pia, mwambie aache kulia lia arudi kwa Mungu wake amuulize Hawa wake yukwapi,


Picha: Situation aliyopo rafikiyo

5721b7596df726abe2274f9a17337fd5.jpg
 
Majuto ni mjukuu, unaemdharau kesho ndo heshima yako, hakuna namna jamaa asake tu mweny degree mwenzake japo najua atakuwa ameoa degree na sio mwanamke so siku yakibuma ajiandae kuyapoza kimtindo
 
Kila jambo hutokea kwa sababu, huenda kabinti ka watu kangenyanyasika vyakutosha kama kangeolewa na jamaa yako. Mwambie jamaa yako aache kulialia bali ajifunze kuwa na msimamo, alafu siku nyingine akitaka kuoa mwambie aombe MUNGU anaemtumikia apate MKE MWEMA na sio MKE MSOMI.
 
Its too late.
Maumivu ya kutojua thamani ya ulichonacho hadi kikaondoka.
Sasa mbona bado ..ngoja ainjoi ndoa na jamaa kama ni gentleman amhdumie vizur ndo siku amuone rasmi..atapiga yowe la kilio
Ni dada mzuri mno. Akipigwa makeup na kuvishwa vizuri,, atapendeza sana sana
 
Kumradhi mkuu lakini huyo msela wako ana akili za kibinti! Ni mabinti ndo huwa wako 'indecisive' mpk apoteze kile alichonacho ndo anagundua thamani yake.
 
Kumradhi mkuu lakini huyo msela wako ana akili za kibinti! Ni mabinti ndo huwa wako 'indecisive' mpk apoteze kile alichonacho ndo anagundua thamani yake.
Ni mwoga na mgeni kwenye hayo mambo maana huyo dem ndo alikua dem wake wa kwanza
 
Sasa ngoja binti akaoge apige vipodozi vya maana(coz yy ndo anaviuza), na joto la Daslam mtt ataivaje ..... Tatzo alitaka yy ndo atangulie kumpata msomi hlf amwache mwenzake anambwela, sasa bht mby kwake imekuwa kinyume..... arest in peace!
 
Haijalishi unaoa au kuolewa na msomi jambo jema ni kua na hekima na kutambua wajibu na majukum yako ktk familia.. Uspojua hvyo hata uwe na degree 10 ni sawa na bure tu
 
Inasikitisha sana baada ya demu kuvalishwa pete ndio anaona thamani yake..ningekuwa karibu ningemzaba kofi moja kumuweka sawa... Kipindi kile yuko nae anasitasita alikuwa haoni thamani yake? Na hata akimuombea mabaya yule Dada sijui kama yatampata
 
Back
Top Bottom