"Nipo juu ya mawe", nimeelewa maana halisi ya usemi huo kwani nimejikuta ghafla maisha yamekuwa magumu kiasi cha kuiona dunia mbaya sana

KB THE DON

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
243
108
Daah kama usemi wasemavyo wajuvi wa maisha NIPO JUU YA MAWE

Wiki hizi 2 ndo nimeelewa maana halisi ya usemi huo kwani nimejikuta ghafla maisha yamekuwa magumu kiasi cha kuiona Dunia kama mbaya sana.

Nimekuwa nikitegemea mshahara nao baada ya kuupata umepitiliza kwenye masuala ambayo ni must solve nikajikuta nabaki mwenyewe mtupu a.k.a JUU YA MAWE

Hata ninapoandika hapa sioni utamu au furaha ya aina yoyote ile duniani maana sina kitu nimebaki mwenyewe tena mtupu bila chochote
Hivyo nahitaji huruma na mawazo kutoka kwenu Great Thinkers.
 
Kama umeweza kulog in JF kisima cha maarifa naamini itakutoa stress za hapa na pale, hali unayoi feel ni yaa muda tu na si ya kudumu.
 
Punguza matumizi yako mkuu una mshahara halafu unalalamika hivyo Mungu hapendi

Kuna watu hata mshahara hawana je hao tuwaweke kundi gani mkuu
The issue ni kwamba mambo ambayo n ya lazima kuyasolve yalikuwa mengi kuzidi kipato ndo changamoto yangu tatizo si matumizi mabaya wala nn
 
Acha kufuruu mzee baba,
Kuishiwa mwezi mmoja tuu unalalamika?

Asemeje alieko kitandani miezi?
Asemeje hata asie na hicho kimshahara?
Asemeje hata asiepata ya kula?
Asemeje anayeteseka na madeni?..
Haya mawazo yananipa mori sana stress zimeanza kushuka sasa kwan kumbe kuna wakati tunajiangalia wenyewe nakuona kama tunayo matatizo makubwa sana
 
Mkuu, kavute "advance salary" kisha uanze kubana matumizi kwa siku zilizobakia. Leo ni tarehe 29, January najaribu kufikiria utakavyojibana mpaka ifikapo siku ya mshahara kwa mwezi February.

Omba Mola wako azidi kukushushia rehema na neema zake, ili zisitokee changamoto nyingine ambazo zitakufanya uwe na uhitaji wa matumizi makubwa ya fedha, usije ukajikuta unaanza kuweka vitu vyako vya maana rehani ama hata kuviuza kwa bei ya hasara.
 
Back
Top Bottom