Nipo chuo mwaka wa pili,nasomea ualimu wa sanaa,nataka kuacha chuo

Kwa mitazamo hyo yaaan nyie waalimu wetu mtaendelea kukandamizwa hvyohvyo mpaka mwisho wa hii dunia... Hakuna nnachowaza zaid ya kuajiriwa mbona wanaosoma masomo ya biashara hawawaz kuacha vyuo na serikali haijatangaza ajira zao???? Lengo kuu la kusoma sio kuajiriwa pekee na hata kama ni kuajiriwa sio lazima serikali ndio ikuajir
 
Acha upuuzi wewe maliza chuo then ukishapata vyeti vyako ingia mtaani tafuta mwenzako fungueni tution center.......ndio kujiajiri kwenyewe
Mkuu kwa jinsi Mama Ndalichako anavyotaka watoto wawe ma engeneer na madaktari I mean kutaka watoto wasome masomo ya sayansi peke yake then kutakuwa na demand ya walimu wa sayansi, tuition wenye kufundisha masomo ya science ndio watapata wanafunzi.

Mie sikushauri uache, soma,baadae huyu mama zikimjia kuwa anatakiwa kuweka mambo balanced, then demand ya walimu wa Sanaa itakua juu tena.
 
Acha tu vyeti vya degree havina maana ukisha vipata vinakuongezea presha ya kutafta kazi elimu uliyopata iyo miaka miwili inatosha kujiari kabisaas
Never, kwani hii serikali ni ya milele, itakuja ingine wataajiliwa. Usimpotoshe. Ndio maana Bukoba elimu inarudi nyuma. Kwenu wapi? Kanyigo? Kiziba? Nshamba?
 
Hellow wana jamvi mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja hivi hapa nchini,Nipo mwaka wa pili sasa semester yangu ya tatu.Nasomea ualimu wa masomo ya Arts yaani HIstory na Geography.
Kiukweli niliamua kusomea ualimu kwa lengo la kupata ajira,kwani ukiangalia mimi ni mtoto wa maskini nimesoma shule ya kata, kimbilio langu lilikuwa ni ualimu ili niweze kuajiriwa nikomboe familia yangu.

Hivi juzi waziri wa elimu amesema srikali haitaajiri walimu wa masomoya sanaa, na nikiangalia mbele yangu kuna Batch kama tatu hivi ambazo zitasota mtaani, Sasa mimisitaki shida na kujipa presha ,hii ndo semester yangu ya mwisho ,nikifanya UE mazima sirudi tena chuo maana lengo langu limevurugika hata kama nikiendelea kusoma najipotezea muda tuu.
Nilisomea ualimu ili niajiriwe sio kujiajiri, sikujiandaa kujiajiri kupitia ualimu,

Sitaki shida na ndalichako, sitaki shida na magufuli, Narudi zangu kijini waridhike wao, maana furaha yao ni kuona vijana tunaangaika mtaani.
NB:jueni kwamba asilia kubwa ya vijana wanaokimbilia kusomea ualimu ni watoto wa maskini

Mkuu ulichosema ni ukweli mtupu. Uko sahihi.

Isipokuwa ata ungekuwa ni wewe ungefanya ivyo. Na kama usingefanya ivyo basi kuna mashaka ungekuwa ni mmoja kati ya wale 4.

Sina nia ya kukutusi ila ni kutokana na sababu hii;

Waalimu wa masomo ya arts ni wengi sana kwa sasa. Unakuta mwl anafundisha kipindi kimoja tu kwa wiki, wakati minimum ni vipindi 25.

Ni shule chache tu zina upungufu wa masomo ya arts tena sio masomo yote ya arts.

Kwa kuwa hii ni awamu ya kutenda haki, itakuwa sio uerevu, itakuwa ni jambo la ajabu kuendelea kuwaajiri, maana wataenda kufanya kazi gani Mkuu!!?

Lakini bado wewe ni kijana kama kuna uwezekano unaonaje ungebadilisha hayo masomo,

au kama wanafundisha lugha za kimataifa unaonaje nazo ungeziwekea mikakati ili ujiongezee CV
 
Mambo yanabadilika sana yaan kipind cha nyuma ukisoma ualimu mkopo ni ni lazima pia huna presha na Gpa kal na ukimaliza ajira serikalin ni lazima wala co ombi. KWEL MAISHA YANAENDA KAS SANA.
 
Sasa unachosubir nini mpaka sasa, acha tu wala usijisumbue kufanya mitihani
 
Kijana fursa za ualimu ni nyingi cha msing soma upate cheti chako. Unaweza anzisha kituo cha masomo ya ziada,siku hizi ni dili. Hela ipo kazi ni kutumia akili kuivumbua ilipo.
 
Acha fikra kama hizo....maliza hio shahada..hiwez jua nn kitatokea mbele [HASHTAG]#sio[/HASHTAG] lazima uajiliwe na serikal..kuna ngo pia
 
Acha uje mjini machinga wameruhusiwa kufanya biashara hadi katikati ya barabara hivyo utapata nafasi kama uli save chenji za buku amua sasa..
 
Endelea kusoma ,ukiacha miaka michache ijayo utajuta.
Weka mawazo yako kwenye kujiajiri pia shule binafsi si zipo wao wataajiri tu,Unaweza kupata nafasi ya kwenda Polisi,Magereza,Uhamiaji,JWTZ kwa kutumia cheti chako cha digrii hivi mfano taasisi hizo za serikali zikitangaza zinataka kuajiri wahitimu wenye digrii wewe huna digrii na ulipata nafasi ya kusoma ukaacha utajisikiaje?, Pia fungua hata chekechea utaanza na watoto wachache mwisho wa siku utajikuta unatamani kuanziaha shule kabisa.
Maisha ni mapambano,ubunifu na uvumilivu.
Mlango mmoja ukifungwa mingine mingi itafunguka.
 
Poleni sana wadogo zangu. Ila chuo usiache... Kama ndege hawalimi ila wanakula nafaka na wanaishi naamini hata ww Mungu amekuandalia kitu... Sio wote unaowaona barabarani ni walimu aysee,,, maisha bado yapo sana
 
Itafika kipindi hata hao walimu wa sayansi watatosha na hawataajiriwa.
Mbona serikali haiajiri au inaajiri kwa kiasi kidogo sana mainjinia,wahasibu,waandishi wa habari,wataalamu wa Sanaa lakini bado watu wanasoma hizo fani.
 
Muhimu uwe na cheti chako hata ukiingia mtaani na kufanya vibarua si mbaya, opportunity are there Huwezi jua mbele itakuwaje
 
Mtihani mkubwa ni kuchagua usome kitu ili upate ajira kirahisi iwe kwa kuajiriiwa au kujiajiri....vyuo vingi vinatoa kozi nyingi zenye nafasi finyu ya ajira...
 
Back
Top Bottom