Nipitishie bank gani mshahara wangu ili nipate mkopo?

Mgengeli

Senior Member
Sep 23, 2011
193
13
Wana JF,Natafuta bank ya kupitishia mshahara wangu ili niweze kupata mkopo kwa bank zetu hapa tanzania ni bank gani inafaaa?
 
Wana JF,Natafuta bank ya kupitishia mshahara wangu ili niweze kupata mkopo kwa bank zetu hapa tanzania ni bank gani inafaaa?

Kama umewahi kuchukuwa mkopo Standard chartered Bank miaka ya nyuma na ukamaliza vizuri mkopo wako basi ukiwaomba sasa watakupa mara moja baada ya kupitisha mshahara wako.

Riba zao ni kuanzia 15 na kuendelea. Kama hujawahi kukopa sidhani kama kwa mwaka huu utapata ila unaweza ku search simu yao kwenye mtandao na ukaongea na mtu wa mikopo atakuambia kila kitu
Nakutakia kila heri
 
Wana JF,Natafuta bank ya kupitishia mshahara wangu ili niweze kupata mkopo kwa bank zetu hapa tanzania ni bank gani inafaaa?

Mkuu kwa uzoefu wangu mdogo nilionao benki ya Posta ni rahisi mno mno mno mno kupata mkopo ukipitishia mshahara wako huko. Mwajiri wako tu a-endorse na haina hasara kwake maana pia utatakiwa kulipia pesa kidogo kama bima ambapo ikitokea umeshindwa kulipa mkopo basi bima inawalipa benki.
 
je kwa mshahara wangu wa 1,370,000 baada ya makato nitapata mkopo kuanzia shilingi ngapi
 
je kwa mshahara wangu wa 1,370,000 baada ya makato nitapata mkopo kuanzia shilingi ngapi
Mh!mshahara wako hauendani na maswali unayouliza,ama kama upo serikalini au private organisation nashawishika kwamba upo kwenye seniority level,nashindwa kuelewa ni kwa nini hufahamu kitu kidogo kama hiki!!!!!I am dubious about your thinking capacity!!!
 
I am dubious about..........?
 
Inabidi mshahara upite mara ngapi benki ya posta kabla ya kuqualify kupata? Maana niliuliza Stanbi wakaniambia atleast 3 months of salary.
 
Sikushauri kukopa benki yenye interest rate ya juu zaidi ya 17%, bora ukajiunge na SACCOS zenye mwelekeo mzuri, kwa ajili ya maisha ya mbele.
 
Inabidi mshahara upite mara ngapi benki ya posta kabla ya kuqualify kupata? Maana niliuliza Stanbi wakaniambia atleast 3 months of salary.

Stanbic 21% interest rate, utalia na kusaga meno baadaye.
 
achana na mawazo ya kukopa. jifunze kuweka akiba. mkopo unaumiza sana ukisha upata na kuutumia. mia
 
Inategemea unakopa kwa ajili ya nini. Kama ni matumizi binafsi basi lazima utaumia baada, lakini kama utaweza kufanya kitu kuleta kipato kitachorejesha makato ya mkopo na kuleta kipato endelevu basi ni wazo zuri. Cha msingi ni kujua unakopa kwa ajili ya nini? Sio ilimradi upate hela tu!
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom