Nipeni urais, jengo la bunge mnadani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nipeni urais, jengo la bunge mnadani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NasDaz, Jul 2, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,311
  Likes Received: 1,593
  Trophy Points: 280
  Kwa hili sitanii kabisaa, mkinipa Urais Jengo la Bunge Dodoma niliweka mnadani otherwise nitalitafutia matumizi mengine!! Ni bahati mbaya sana kwamba sijui idadi kamili ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, lakini am sure hawapungui 250! Now let's take deep breath. Tuseme bunge litakaa miezi miwili, i.e. 56 days. Kwa wastani tuseme wamehudhuria wabunge 200 kwa kipindi kizima cha bunge!! Nasikia posho ya wakati wa vikao vya bunge ni Sh. 100,000. 00 kwa siku! Therefore kwa kipindi chote ni : 200x 100,000.00 = 1,120,000,000/. Hapa manake ni kwamba ikiwa watahudhuria wabunge 200 basi watatafuna kodi cha wananchi kiasi cha shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Moja Ishirini. However, ukiangalia sana labda kwa wastani Kila Mbunge atakuwa anauliza maswali matano kwa kipindi Kizima cha Bunge!! Anyway, tufanye Kila Mbunge ameuliza maswali KUMI kwa msimu mzima. This means that Ni siku Kumi Tu ndizo alilazimika kuwa bungeni ili kuwasilisha swali lake! Out of 56 days, 46 days anaenda bungeni kupiga soga na kupiga makofi!! Mkinipa urais, hakutakuwa na muda wa kupiga soga bungeni!! Naamini wastani wa maswali 10 unatosha kabisa kwavile kuna wengine hata hilo moja hawaulizi!! Hivyo basi, kila mbunge atakuja Bungeni siku zile tu ambazo ana maswali anayotaka kujibiwa ikiwa na kuuliza maswali ya nyongeza. Kwahiyo, kutoka kila mbunge tutaokoa siku angalau 40, ambazo monetary value yake ni:
  200 x 100,000.00x 40 = 800,000,000/. Siku zizizobaki atabaki nyumbani na kusikiliza kupitia redioni/runingani na akitaka kuja bungeni aje kwa gharama zake!! In addition, kwa wastani ni wabunge 25 tu ndio huchangia hoja au kuuliza maswali kwa kila session! Kumbe jengo la watu wasiozidi mia moja linatosha kabisa ku-accomodate hawa wabunge na wageni! Kwavile watoa hoja hawazidi 50 kwa siku, basi jengo langu la bunge litajengwa kwa kuzingatia idadi ya wabunge wanaotakiwa kuwepo bungeni kwa siku. Lililopo ni kubwa mno, hivyo nitalitia mnadani!!
  POSSITIVE IMPACT: Naamini jambo hili litasaidia mambo yafuatayo:
  1. Maprofesa na Madaktari waliojazana bungeni watapungua na kwenda kuzitumikia taaluma zao.
  2. Kwavile kwa siku kutakuwa na idadi ndogo tu ya wabunge basi hatuna haja ya kuwa na mjengo mkubwa. Uliopo tutauingiza sokoni na pesa zitakazopatika tutazipeleka Loan Board
  3.Tutakuwa tumeokowa kiasi kikubwa sana cha pesa.

  Najuwa kuna mapungufu lakini nitakaa na wataalamu wangu ili jambo hili tulifanikishe vizuri!
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,487
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Du ni sh 100,000 kwa siku kwa mbunge ina maana kwa siku 56 ni sawa na

  wabunge 200 X 100,000 X 56 = 1,120,000,000

  Kweli Tanzania ni nchi tajiri sana
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,017
  Likes Received: 1,217
  Trophy Points: 280
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,311
  Likes Received: 1,593
  Trophy Points: 280
  Tena ni super millionaire
   
 5. M

  Mwambashi Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa,
  Tunatumia resources zetu vibaya, badala ya Professors wetu kukaa kwenye accademic institutions wakatumia taaluma zao kwa kuelimisha jamii, wanakaa bungeni halafu hawachangii chochote!!!!!!!!!
   
Loading...