ABEDNEGO CHARLES
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 567
- 104
Kwa maoni yangu Lema amefanya kile ambacho wana CCM wengi wameshindwa kukifanya kwa kwa miaka yote ya uhai wa chama chao ambacho ni kuishi kwenye mioyo ya anaowaongoza. Ndicho alichomudu mwana CCM mwenye kadi namba moja ya CCM Julius K Nyerere. Nyerere amekufa lakini hajafa kwenye mioyo ya watu. Bado wengi wanamwona kuwa ni alama yao ya maisha. Lema, kalimudu hilo ndani ya kipindi kifupi alichoshika jimbo hilo. Kukaa kwenye mioyo ya watu no matter how good or bad you are ni mafanikio makubwa sana. Ukitaka kujua hilo, mwulize JK. Alikuwa kwenye mioyo ya watu 2005 na leo hii kabakia kuwa kwenye mioyo ya mafisadi pekee.