Nipeni tofauti ya Nchi, Serikali, Jamhuri, Taifa, Dola na Tanzania?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
781
500
Siku za hivi karibuni zimeibuka kauli tofauti tofauti na kila moja zinajinasibu kwa upande wake, wapo wanaosema siwezi kuichafua Nchi yangu, na wengine wanaosema hakuna Serikali isiyokuwa na Nchi, na wengine wanasema tuoneshe Bendera ya Nchi ilivyo na Bendera ya Serikali?
 

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
781
500
Mkuu gusia basi Nchi!

Kwanini unahangaika nalo?

Vitabu vipo chungu nzima

Kwa sasa nadhani tuangalie Dolla ile iliyoshuka siyo Dola Tanzania

Tuangalie Wanachi wa Tanzania watapata msukosuko gani wakiwemo wa zanzibar ndo maana ya jamuhuri,

Alafu Rais wa Nchi iitwayo Tanzania ishu ya Dollar kupanda anasemaje?
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,962
2,000
Siku za hivi karibuni zimeibuka kauli tofauti tofauti na kila moja zinajinasibu kwa upande wake, wapo wanaosema siwezi kuichafua Nchi yangu, na wengine wanaosema hakuna Serikali isiyokuwa na Nchi, na wengine wanasema tuoneshe Bendera ya Nchi ilivyo na Bendera ya Serikali?
Mkuu Nyumba mungu,
Nchi ni eneo, ardhi na mipaka yake- A country
Dola ni mamlaka ya nchi hiyo yenye nguvu za kimamlaka- sovereignty
Mfano Zanzibar ni inchi lakini sio dola.
Serikali ni mfumo wa utawala wa nchi.
Jamhuri ni nchi yenye mamlaka yake kamili ya kujitawala, mfano Tanganyika ilipata Uhuru Desemba 9, 1961 kuwa nchi huru, na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru,
Terehe 9 Desemba Mwaka 1962, ndipo tukawa Jamhuri, Mwalimu Nyerere akajiuzulu u PM, na kuwa the 1st President wa Republic of Tanganyika.
Taifa ni Nation, utaifa, nationality na nationalism.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya taifa, hivyo Mtanzania yoyote Mzalendo wa kweli, hawezi kulichafua taifa lake. Lakini mataifa yanaongozwa na serikali zinazoongozwa na watu.

Hawa watu wanaoongoza serikali wakichafua, wanapaswa kuambiwa. Kama wewe ni mchafu, kuambiwa ukweli kuwa wewe ni mchafu, sio kuchafuliwa bali ni kuambiwa ukweli. Kuchafuliwa ni kama wewe ni msafi, halafu mtu anakupaka matope uonekane mchafu wakati in reality wewe ni msafi.

Swali linabaki, wanaolalamikia watu kuchafua watu, serikali, viongozi, jee wachafuliwa hao ni wasafi?.
P
 

mvaa viatu

JF-Expert Member
Nov 6, 2017
282
500
Dola inatokana na neno la kiarabu daula , yaani uongozi.75% ya kiswahili imechukua maneno ya kiarabu Kama Kadri,aghalabu, mahali, kila, kitabu,kalamu,waziri, binti, binadamu, n.k
Sasa hili neno daula ktk kiarabu pia ninaonyesha ni msamiati mpya,maana nilishaliulizia kwa wasomi wa hiyo lugha lakini sikupata jibu sahihi ni kweli wanalitumia kuita nchi nyingine yaani kama daulatu tanzaania wakiwa na maana ya nchi ya tanzania,ila bado hakuna ushahidi kabra ya uwepo wa dolla yamarekani walikuwa wanalitumia neno hilo.ili ionekane jibu lako nisahihi thibitisha kwa kuleta maneno ya mtume au aya yanayoelezea kwa kuyaita mataifa mengine kwakutumia neno hilo la daulatu.dhana yangu mimi tunaposema vyombo vya dola au dala fulani nadhani tunaita hivyo sababu ya dola fedha ya marekani,kwamaana ndio fedha inayotumika kibiashara duniani,kwahiyo tunaita vyombo vya dola tunamaanisha vinaendeshwa kwa kutumia fedha.na sio kwamaana ya vyombo vya nchi.kama wapo watu wabalaza lakiswahili watusaidie maana ya hili ni nini? Na chimbuko lake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

zigii

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
516
250
Doĺa ni moja ya mihimili 3 ya serekali
1 DOLA
2 BUNGE
3 MAHAKAMA
DOLA ni majeshi yaani vyombo vyote vya ulinzi
BUNGE ni wawakilishi wa wananchi serekalini
MAHAKAMA ni mfumo mzima wa sheria na watendaji wake
Ktk uchaguzi chama chochote kikishinda na kumpata rais huunda serekali lakini haundi dola maana bunge likiahirishwa serekali hufa ndio maana rais huteuwa watendaji watakao msaidia kazi (executives) vyombo vya ulinzi huwepo muda wote kwa kuwa ameshika vyombo vya ulinzi huitwa amir jeshi mkuu huwezi kuwa amir jeshi bila kuwepo vyombo hivyo na ndio maana rais wa zanzibar sio amir jeshi kwa kuwa hana vyombo vya ulinzi
Raisi baada ya kushika dola anateuwa watu watakao kuwa juu ya vyombo hivyo ili kupunguza makali
BUNGE ni wawakilishi wa wananchi kazi yao kubwa ni kuwasimamia watendaji (executives) kuwakosoa kuelekeza na kutunga sheria ambazo hazitawakandamiza wananchi
MAHAKAMA wao wanashughulika sana na sheria kuitafsiri na kutoa haki katika mihimili miwili yaani bunge na dola watakapovunja sheria mahakama hutoa adhabu au haki
Sasa ukiunganisha hiyo mihimili 3 huitwa serekali na yeyote atakae kuwa na hamu ya kushika dola maana ya anavitaka vyombo vya usalama ambavyo ni jeshi, polisi, magereza, uhamiaji, tiss, zima moto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom