Nipeni sababu za kisayansi nimekuta chupa ya soda imepasuka na soda yake kwenye friji

Alphaking2023

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,093
2,121
Nisiongee sana maana Nina hasira na soda yangu niliiweka nikirudi toka mazoezi nije kunywa ila nimekuta imepasuka ndani ya friji tatizo nini,
Nipeni sababu za kisayansi na mniambie siku nyingne nifanye nini ili isipasuke kama Leo
 
Siku nyingine usiiweke chupa yako ya soda hapo ulipoiweka ikapasuka. Fizikia(Physics) inaeleza kwamba ubaridi mkali chini ya nyuzi 4 kizio cha centigrade huyafanya maji kuganda(Barafu) na maji yakiganda huongezeka ukubwa(Valume) i.e hutanuka. Hiyo chupa yako haikuwa na uwezo wa kuhimili kutanuka kwa maji(Soda) na hivyo ikapasuka. Pole sana bro. kanunue soda nyingine na hilo liwe fundisho kwako na wengineo
 
Hakuna chemical rxn kama hiyo hiyo ni sababu ya kufikirika sio ya kisayansi
Kutokana na baridi kuwa kali ile chupa ilibidi isinyae na hiki ni kitendo cha kila kitu kinapopata nyuzi joto la sifuri sasa chupa kutokana mfumo wake uliotengezewa imebidi ivunjike kutokana na ule mgandamizo. #chukuaHiyo
 
Siku nyingine usiiweke chupa yako ya soda hapo ulipoiweka ikapasuka. Fizikia(Physics) inaeleza kwamba ubaridi mkali chini ya nyuzi 4 kizio cha centigrade huyafanya maji kuganda(Barafu) na maji yakiganda huongezeka ukubwa(Valume) i.e hutanuka. Hiyo chupa yako haikuwa na uwezo wa kuhimili kutanuka kwa maji(Soda) na hivyo ikapasuka. Pole sana bro. kanunue soda nyingine na hilo liwe fundisho kwako na wengineo
Asante kwa jibu zuri nimeridhika ni la kisayansi ila hapo kwenye kujaa kwa volume means ningekuwa nimetoa kizibo isingeweza kupasuka.?
 
Kutokana na baridi kuwa kali ile chupa ilibidi isinyae na hiki ni kitendo cha kila kitu kinapopata nyuzi joto la sifuri sasa chupa kutokana mfumo wake uliotengezewa imebidi ivunjike kutokana na ule mgandamizo. #chukuaHiyo
Napata ugumu kukubaliana na wewe unaposema chupa ndo inayoathiriwa na ile baridi kwa sababu ukiiweka bila kitu haiwezi kupasuka
 
Ndiyo mkuu; Isingepasuka.
Maji yanaongezeka volume yanapoganda Sawa kwa maana hiyo nataka nifanye kitu hapa najaza Maji kwenye chupa naacha sehem ndogo sana kwa juu naweka kwenye freeze kesho asubuh niangalie kama yatakuwa yamejaa hadi juu baada ya kuwa yameongezeka volume au hukumaanisha hivyo?
 
Mh! Mkuu utaishia tena kuipoteza hata na hiyo chupa.Kumbuka kwamba hayo maji katika utanukaji wake ni kwa all directions. Hayatazingatia mdomo uko wapi ili yaelekee huko. Maji ni muunganiko wa kikemikali baina ya hewa ya Oxygen O2 na Hydrogen H2. Katika utanukaji unaozungumziwa hapa ni kwenye viunganishio (bonds) ambavyo huwezesha hewa hizo mbili kuwa kitu kimoja Compound iitwayo maji 2H2O. Samahani lakini Chemistry sio rahisi kueleza kwa kiswahili.
 
Dah form two hii nakumbuka kwenye pressure kna kiswali cha ivi ila apo difference in pressure inaleta io kwakua external pressure inakua transmitted undiminished through out io chupa.....
Ukiachana na mambo ya water expansion .
Hapa pressure haihusiki mkuu.
Ni hivi.
Tujikumbushe kwenye expansion of solid and liquid pia tusisahau na thermal expansivity zao.
Vyote viwili vinatabia za kushangaza. Ngoja tuanze na maji.
Maji hayana linear expansivity, yana anomolous expansivity.
Kwenye nyuzi za centigrade 4 maji hupungua ujazo. Yakisha zidi joto hilo huanza kuongezeka ujazo mpaka yanaganda na kuwa yabisi yanazidi kuongezeka ujazo

Sasa tuje kwenye chupa.
Asili ya chupa za soda ni glass in nature, na tabia yake ni insulator in nature hivyo wakati kuta za nje zikipata ibaridi inasinyaa haraka (contraction) kuliko kuta ya ndani.

Hivyo basi kipi huvunja chupa??
Maji ya ndani yanatanuka kwa kasi mno kadiri inavyopungua joto hasaa kwenye nyuzi sifuri, ukuta wa ndani unalazimishwa kutanuka kwa ndani ili barafu ipate nafasi zaidi ya kutanuka, huku nje nako chupa inalazimishwa kusinyaa kadiri joto linavyopungua sasa. Hapa inatokea kama ushindani kusinyaa na kutanuka na ikumbukwe chupa haina sifa ya elasticity mwisho hujikuta inashidwa kuhimili na kupasuka.

Mchango wangu huo
 
Back
Top Bottom