Nipeni mwanga nahitaji kujua huduma za Cable tv

mr man city

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
467
319
Kwema wakuu! Mwenye uzoefu au anayetumia Cable tv anipe mwanga kidogo nahitaji kujua huduma zao kabla ya kuunganishiwa
 
Sifa ya kwanza Channel zina mchele mchele.

Sifa ya pili malipo kwa mwezi ni nafuu sana.

Sifa ya tatu unaweza kaa miezi mitatu hujalipia na bado hukatiwi huduma.
 
Je chanel unabadilisha mwenyewe au inakuwaje.
Chanel za mpira mfano epl na uefa si zipo?
Au chanel za aina gani ndio zipo
 
Mkuu remote inakaa nyumbani kwako, au unamaanisha nini kubadilisha channel?

Kwa huku nilipo mimi channel za mpira zipo ila ni chache sana BeinSports (kuna mechi hutaweza kuziona).

Zipo channel nyingi, movies, music, documentary, religious n.k
 
Sijui huwa wanafanyaje ila unakuwa unabadili chamel kama unarusha nyimbo yani,na remote ya tv

Nimekumbuka mbali sana yalikuwa maisha.
 
Kwema wakuu! Mwenye uzoefu au anayetumia Cable tv anipe mwanga kidogo nahitaji kujua huduma zao kabla ya kuunganishiwa
Mkuu vuta tu DSTV ule raha na kifurushi cha premium . Cable shida mvua zikinyesha tu lazima wakate. Shida nyingine ni kuunguza TV kutokana na radi yaani Kila ukizima TV lazima uchomoe na waya wa cable hasa kipindi cha mvua kukwepa radi. Pia nyaya za cable zimepita sehemu nyingi ni rahisi kukatwa na watu wasiowahusika au kukatika
 
Mkuu remote inakaa nyumbani kwako, au unamaanisha nini kubadilisha channel?

Kwa huku nilipo mimi channel za mpira zipo ila ni chache sana BeinSports (kuna mechi hutaweza kuziona).

Zipo channel nyingi, movies, music, documentary, religious n.k
Sawa mkuu..mimi hizo chanel za mpira ndio nazitaka
 
Mkuu vuta tu DSTV ule raha na kifurushi cha premium . Cable shida mvua zikinyesha tu lazima wakate. Shida nyingine ni kuunguza TV kutokana na radi yaani Kila ukizima TV lazima uchomoe na waya wa cable hasa kipindi cha mvua kukwepa radi. Pia nyaya za cable zimepita sehemu nyingi ni rahisi kukatwa na watu wasiowahusika au kukatika
Kwa sasa usawa bado...dstv kifurushi ni sawa na mshahara wa mtu. Hicho cha elf 9 sitapata ninachotaka bora niangalie mpira kibanda umiza tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom