Nipeni mbinu za uandishi bora wenye kuvutia

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
315
740
Habari zenu ndugu na jamaa katika mtandao pendwa wa jamiiforums.com Bila Shaka muwema kabisa.

Hongereni kwa kazi na ibada kwa wale ambao walikwenda leo, na ambao hawajafanikiwa Basi MUNGU AWAKUMBUSHE.


BAADA YA KUWASALIMU.

Nimekuja mbele yenu leo kuomba msaada juu ya uandishi wa makala na stori za kuvutia.

Binafsi huwa napenda sana kuandika, na napenda sana kusoma. Lakini sina elimu sana juu ya Jambo hili.

Hivyo naomba mbinu mbali mbali za uandishi wenye kuvutia.

Kwani napenda kuandika Sana

- Stori mbali mbali za matukio ya kusisimua.

- Riwaya n.k

LAKINI

Kwakuwa sina ujuzi Sana, ndio maana hata huu Uzi wangu hapa haujakuvutia saaaaaana.

Hivyo Basi, NAPOKEA TOKA KWAKO -

Msaada
Ushauri
Maoni
Matusi
Lawama
Kashfa
Kukatishwa tamaa
Kupewa moyo

Na mengine mengi.

Nawasilisha.
 
Jaribu kusoma novels mbalimbali za Kiswahili na Kiingereza ucheki muundo wake,mtindo,aina ya lugha iliyotumika kumvutia msomaji n.k.Mimi sio mwandishi ila kutokana na kupitia hivi vitabu vya hadithi na simulizi kwa sana naweza sema ukinipa kazi ya kuandika novel sahivi, sitaandika vizuri sana au vibaya sana.Yaani ntakuwa mtu kati,tofauti na huko nyuma ningeandika vibaya tu.
Mengine wataongeza wazoefu.
 
Jaribu kusoma novels mbalimbali za Kiswahili na Kiingereza ucheki muundo wake,mtindo,aina ya lugha iliyotumika kumvutia msomaji n.k.Mimi sio mwandishi ila kutokana na kupitia hivi vitabu vya hadithi na simulizi kwa sana naweza sema ukinipa kazi ya kuandika novel sahivi, sitaandika vizuri sana au vibaya sana.Yaani ntakuwa mtu kati,tofauti na huko nyuma nisingeweza kuandika chochote.
Mengine wataongeza wazoefu.

L7 Zero brain
 
Jifunze kupitia stori/simulizi za wengine....hata humu jukwaani zipo nyingi tu ukitembelea ukurasa wa ENTERTAINMENT.

Jaribu pia kupita kwenye Mtandao wa You Tube nadhani waweza kutana na mafundisho mawili matatu, ingawa nadhani mengi yapo kwenye lugha ngeni ya kiingereza.
 
Back
Top Bottom