Nipeni mbinu za kumtoa bosi asiye na elimu aende kucheza taarabu..

kwakweli endelea kufundisha tu n
dg una masifa mno na hako kaelimu kako siku ukiwa mhasibu utalaza njaa familia za wakufunzi kwa urasimu usio walazima simply unataka waacknowledge umesoma, usipende kuvua samaki kwenye kapu la mwenzio badala yake nenda nawe baharini. Kuliko kulalamikia mtu ambaye pengine hajapata audit querry bora ungeanza CPA ndo ujue machozi na jasho ulilopata huko nyuma ni chamtoto.
Tuna walimu wachache wa hesabu plz endelea kusaidia taifa
 
habari wakuu,
nafanya kazi chuo cha ualimu. hapa nna dip. ya education na digrii ya accounting and finance.......... nafanya kaxi za kufndisha tu.....


muhasibu wa hapa hana elimu kabsaaaaaa, form four, mweupeeee!!!!!! nahsi aliajiriwa kama mfagizi.

nipen mbinu za kumtoa, nichukue nafas.......

toa maoni ya kujenga sio matusi..
Mkuu hujatueleza kama mliajiriwa pamoja au vipi? nani alianza kuajiriwa? Wewe kwani uliomba kazi gani? ni hiyo ya kufundisha au ya uhasibu. Siamini kama mtu una degree ya Account na Finance halafu ufundishe tu, kuna tatizo ambalo unalo na kila mahali ukienda baada ya kufanya kazi uliyoajiririwa unafanya kazi za research ya kujua nani ana sifa gani. Nadhani kitu muhimu ni kuzingatia ajira iliyokuleta hapo. Kama hailipi tafuta kwa kutumia degree yako. Na si kumtoa mwenzio. Kwan anaweza akatoka na hiyo nafasi usiipate wewe, kwa sababu wewe ni mwalim wa kufundisha na sio muhasibu kwa kumbukumbu alizo nazo mwajiri wako. Na watu kama nyinyi mko wengi maofisini ambao mnapoteza muda kwa kumfuatilia mtu mwingine. Hiyo ni kazi ya HR office kupima uwezo wa mtu.
 
Kama uliajiriwa kama Mwalimu rekodi yako itakuwa inasomeka kuwa wewe ni mwalimu, Je kwenda kwako kusoma hio degree uliidhinishwa na ofisi au ulisoma kinyemela? Kama ulisoma kinyemela anza na kurekebisha rekodi zako zisomeke kuwa umesoma hiyo degree, Na kama ni serikalini hiyo kitu ina mlolongo kidogo.
 
Muosha Huoshwa! Waijua hii Methali ?.
Fanya bidii sana kutafuta haki na si Kutenda Matendo ya Hila Ndugu yangu! Maana siku zote ukijua Kutoa wenzio nawe pia utatolewa! Na Pili sijaona sababu ya wewe kujisifu sana na Elimu uliyonayo maana wakati wa kujisifu umepita na Kinachoangaliwa angaliwa Maendeleo tu!
 
Back
Top Bottom