Nipende Kuungana na Watanzania Wenzangu Wapenda haki Kudai Katiba Mpya.

ProMagufuli

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
219
235
Poleni na Majukumu ya kikazi. Katika kuijenga nchi yetu nzuri Tanzania.

Moja kwa moja kwenye.
Haya ni maoni yangu binafsi. Kama mwananchi wa Tanzania niliye na Uhuru wa kutoa maoni.
Kama mjuavyo wengi tunaofutilia mambo nchini Tanzania. Kumeibuka vuguvugu la kudai katiba mpya Tanzania. Mimi nipende kuungana nao nikiwa na akili timamu. Hoja zangu ni..
1. Katiba mpya itatusaidia kuiondoa CCM madarakani pamoja na mifumo yake mibovu iliojiwekea pia na kuweza kuwawajibisha wote waliohusika kutufikisha hapa. Kwa sababu most ya viongozi wa CCM wako ni wabinafsi wako tayari kufanya upuuzi na kusifia ilimradi wapate vyeo. Wakati nchi inapotea, nchi inakuwa haina consistence ipo ipo tu.
2. Itasaidia nchi Tanzania kuwa na mifumo imara. Hivyo kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja pia na haki za watu kuzingatiwa.
3. Kupunguza mamlaka ya raisi aliemadarakani. Hapa napendekeza raisi awe anaweza kushitakiwa mahakamani pale akifanya upuuzi. Na hili liweze kufanywa na mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania.
4. Katiba mpya itapeleka wale wote waliodhulumiwa haki zao kuipata. Pia waliotumika kudhulumu pia nao kupata haki zao.
5. Itachochea maendeleo
6. Itatuonesha dira kitu watanzania wanataka.
7. Itafungua macho watanzania juu ya yale yolopita.
8. Na mengine kama kupunguza mtanziko uliopo wa Muungano. Pia kurejesha heshima za kiuongozi.

Mapendekezo yangu juu ya katiba mpya.
1. Kuwe na usawa kati ya wananchi. Mtu akikosa apatiwe haki yake bila kuangalia kile alichonacho.
2. Ubunge uwe na kikomo at most 15 years.
3. Serikali tatu, au moja.
4. Serikali za majimbo.
5. Kuwekwa kwa misingi ya kuboresha maisha ya watanzania wote.

Niwatakie Jumapili njema. Katika ujenzi wa Taifa imara.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom