Nipe neno juu ya Chifu wa Wahehe Adam Abdul Sapi Mkwawa

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
fatmahmkwawa_81108661_2444090689053611_5119334721995677462_n.jpg
fatmahmkwawa_56558720_837784636596763_8410242943342968605_n.jpg
fatmahmkwawa_81799675_2522777391299036_1755069366689124003_n.jpg
fatmahmkwawa_66764994_2406982666203921_4602186506338236657_n.jpg
fatmahmkwawa_74456604_154987532544000_2259377773723778468_n(1).jpg

Chifu wa Wahehe Adam Abdu Sapi Mkwawa

MAZURI NAYOYASIKIA: Anajiheshimu, ni msafi, kaelimika kasoma shule ya matajiri (Iringa international school) ada ni milioni 20 kwa mwaka,

MABAYA NAYOYASIKIA: Ni chotara jambo linalopelekea baadhi ya wahehe kummpiga vita sana lakini naona kasimama kidete, Pia inasemekana hajui kihehe, hili jambo lilipelekea hata Magufuli alipofanya ziara iringa huyu chifu alipoitwa aliishia tu kusema "sina mengi ya kusema namkaribisha Raisi" kiukweli kuna watu tulienda pale kusikia mawili matatu hii ilitukwaza.
 

Attachments

  • fatmahmkwawa_81108661_2444090689053611_5119334721995677462_n.jpg
    fatmahmkwawa_81108661_2444090689053611_5119334721995677462_n.jpg
    68.9 KB · Views: 2
  • 1581938643064.jpeg
    1581938643064.jpeg
    112.7 KB · Views: 2
Huyu alitakiwa asome kuondoa ujinga tuu then arudi kijijini kulea na kuitukuza mizimu, anasoma shule ya 40M ili iweje wakati maisha yake yote analishwa na kulelewa na wana Iringa?

Unforgetable
 
cHIEF MKWAWA

View attachment 1360604

CHIFU MPYA
View attachment 1360605

View attachment 1360607

MAZURI NAYOYASIKIA: Anajiheshimu, ni msafi, kaelimika kasoma shule ya wazungu hapo itinga ada ni milioni 40 kwa mwaka,

MABAYA NAYOYASIKIA:Hajui kihehe hili jambo lilipelekea hata magufuli alipofanya ziara iringa huyu chifu alipoitwa aliishia tu kusema "sina mengi ya kusema namkaribisha raisi" kiukweli kuna watu tulienda pale kusikia mawili matatu hii ilitukwaza
Wahehe tumekamatika. Chief wetu Mburushi
 
safuher,
Inaelekea we ni kuku wa kisasa (umezaliwa mjini, umekulia mjini na wala hujawahi kwenda vijijini)

Nilienda mgogololo huko ndani kumsalimia rafiki yangu ni mwalimu, kihehe ni lugha rasmi huko kiswahili kinatumika kwa wageni ama kufundishia tu, Huko hadi leowanafunzi wanaenda shuleni peku na kupatwa na funza ni jambo la kawaida,

Case ya pili nilienda kijiji cha nyamongo huko Tarime, aisee kule sokoni ni mwendo wa kikurya tu unaweza ukapata wakat mgumu kununua hata togwa kama hukijui kikuria

Mkuu uwe unaenda kusalimia kwenu huko vijijini ndio ujue kuwa lugha zetu za asili zina uzito sana huko vijijini.
 
Huyu dogo wahehe wamempiga vita sanaa lakini naona kasimama aisee, na kinachomponza ni huo uchotara wake 😂😂.

Naona dogo amekua siku hizi.
 
Kujua kihehe sio ishu kwa sababu hakitampa faida yeyote kwa kuwa hata hao hapo anaoishi nao ambao yeye ni chifu wao hawaongei kihehe kama lugha ya kila siku ya mawasiliano.

Na dunia inaenda kasi sana sasa hivi,mimi kabila langu ni mmwera ila nikienda lindi kwetu sisikii watu wakiongea kimwera badala yake wanaongea maneno ya kisasa tu mara kudamshi n.k

Kimwera kinabaki kuwa historia tu,hata kihehe pia ni lugha ambayo haina faida zaidi ya kutumia kama kumbukumbu tu ikiwemo kwenye mambo kama hayo.

Sasa hivi mimi siwezi kukaa na mwanangu nikamfunza lugha ya kabila langu na kimwera najua haina faida itakayoleta mapinduzi na msaada kwa watu.

Chief yuko sahihi kwa sababu kama ni uhehe angefuata mpaka mila za mavazi,asitumie simu kabisa kwa sababu wahehe wa wakati huo hawakuwahi kutumia simu,so ilikuwa aishi kama zamani tu ila kwa kuwa zama zinabadilika lazima na yeye abadilike.

Saasa hivi makabila yanabaki kama chanzo cha kujuana tu sehemu uliyotoka na hilo ndo lengo kuu.
mkuu kwa huyo Chief kwake kujua Kihehe ni muhimu sana,
kuna muda litatokea jambo ambalo litahitaji aende kuonana na kuongea na wazee kijijini ndani-ndani na wengi hawajui kiswahili, kwa kweli hawatafurahi kuona chief wao anatafsiriwa Kihehe wakati yeye ni muhehe.
 
Back
Top Bottom