Nipashe Jumapili yaandika negative tupu kuhusu wabunge wa CHADEMA kutoka bungeni

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI HII LIMEANDIKA HABARI ZA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA BUNGE LIKIEGEMEA KWENYE UPANDE MMOJA TU WENYE KUPINGA. HABARI HIZO NIMEZIWEKA HAPO CHINI. KUNA HABARI KUU TATU TOFAUTI KWENYE GAZETI HILI. KUBWA ZAIDI NI MAONI YA MHARIRI NA NYINGINE MBILI NI HABARI ZA WAANDISHI WAO. HABARI ZOTE HIZI NI NEGATIVE VIEWS. HIVYO KAMA KUNA MTU AMBAYE HAJUI NI NINI KILITOKEA NA AKASOMA GAZETI HILI BASI ATAPATA VERY NEGATIVE SIDE YA HABARI HIZI KWA UPANDE WA CHADEMA KITU AMBACHO SI KWELI HATA KIDOGO.

KWA KIFUPI GAZETI HILI LINATAKA KUTUMA UJUMBE KWAMBA WABUNGE WA CHADEMA WALIKOSEA NA HAKUNA WATU WALIOWAUNGA MKONO KWA KITENDO CHAO CHA KUTOKA NJE YA BUNGE. LAKINI KINACHOSEMWA NA GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI SI KWELI. KITENDO CHA WABUNGE WA CHADEMA KIMEUNGWA MKONO NA WATU WENGI NA WENGI WAMEKITA NI CHA KISHUJAA.

KILA MTU MWENYE AKILI TIMAMU NA NIA NJEMA NA TAIFA LA TANZANIA ANAJUA KABISA MCHAKATO WA UCHAGUZI HASA KATIKA KUHESABU KURA ULIKUWA NA KASORO NYINGI TU KIASI KWAMBA KUNA WAGOMBEA WALISHINDA KWA KUTUMIA UJANJA WA KUGEUZA MATOKEO YA KURA ZA WANANCHI. NA HII SIO SIRI TENA. NEC YENYEWE ILIKIRI KUFANYA MAKOSA KATIKA JIMBO LA GEITA, PIA HIVI KARIBUNI BAADA YA NEC KURUDIA KUHESABU KURA ZA UBUNGE JIMBO LA VUNJO ILIONEKANA KUWA MGOMBEA WA UBUNGE WA CCM ALIKUWA AMEPATA KURA NYINGI ISIVYOSITAHILI KATIKA MATOKEO YA AWALI AMBAO YALITANGAZWA NA TUME HIYO HIYO. MGOMBEA WA TLP ALIKUWA AMEPATA 50% LAKINI BAADA YA KURUDIA KUHESABU ALIPATA 54%. HII NI KWA UBUNGE TU, SASA HATUJUI KWA UPANDE WA URAIS NA MADIWANI. HATA HIVYO KUTOKANA NA KUBADILIKA KWA MATOKEO TENA KWA 4% MHE MREMA WA TLP AMESEMA ANA WASIWASI MADIWANI WA CHAMA CHAKE WALISHINDA LAKINI WAKANYIMWA USHINDI KIUJANJA TU.

KWA KIFUPI KATIKA MIFANO HII MIWILI CCM IMEONEKANA KUPEWA KURA NYINGI ISIVYOSITAHILI.

OK TUACHANE NA MAELEZO MENGI.

KITU MUHIMU HAPA NAPENDA KUSHAURI GAZETI LA NIPESHA HASWA MHARIRI WAKE KUANDIKA HABARI ZAKE BILA KUEGEMEA UPANDE WOWOTE KWA MAANA KUSEMA UKWELI SIKU ZOTE. KINYUME NA HAPO HALITAKUWA TOFAUTI NA MAGAZETI YA VYAMA VYA SIASA AMBAYO YANAANDIKA HABARI ILI KUPIGIA DEBE CHAMA CHAO.

HABARI TATU ZA GAZETI HILI NI HIZI HAPA CHINI.

Chadema kumsusia JK bungeni siyo suluhisho, bali ni kujishushia hadhi
Na Editor
21st November 2010
Wiki hii wakati Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kutoa hutuba yake ya kulizindua Bunge la 10 mjini Dodoma, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) walitoa nje ya bunge kwa kile walichosema hawamtambui rais kwa kuwa ushindi aliopata eti siyo halali.
Haishangazi kwa kuwa kilichotokea Dodoma ni muendelezo wa chama hicho ambapo viongozi wake wa juu walisusia wakati wa kutangazwa matokeo ya mshindi wa urais Jakaya Kikwete, wakasusia alipoapishwa pale Uwanja wa Uhuru na wiki hii wabunge wa chama hicho wakasusa hotuba yake kulizindua Bunge. Hata wakati wa kuapishwa Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda imeelezwa hawakuhudhuria kwa sababu zile zile.
Chadema wanasahau kwamba Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za Bunge na pale bungeni hakosekani. Kama walimsusa Chamwino, pale Bungeni napo watamsusa?
Pale bungeni wabunge huuliza maswali ambayo hujibiwa na mawaziri kwa niaba ya serikali ambayo kimantiki ndiyo waheshimiwa hao wanamkataa Rais aliyeiunda.
Kituko cha pale bungeni siyo siri kiliwaacha Watanzania midomo wazi kutokana na kutoeleweka maudhui yake. Mara tu baada ya Rais kuanza kumshukuru Mungu kisha aanze hotuba yake, wabunge wote wa Chadema waliinuka na kuanza kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakiongozwa na kiongozi wao wa upinzani bungeni, Freeman Mbowe, wengine wakiinamisha vichwa chini. Wabunge wa CCM waliwazomea muda wote walipokuwa wakitoka nje.
Kitendo kile, japokuwa wenyewe walikiona cha kijasiri, lakini kimewatia dosari na kuonekana cha kitoto zaidi. Tulidhani kwamba kama ni malalamiko yanayohusiana na matokeo uchaguzi mkuu uliopita, basi suluhu ipatikane kwa mazungumzo na siyo kusababisha mgawanyiko kama ambao umeanza kujitokeza hivi sasa.
Chadema bila shaka wanaelewa fika kwamba sheria inaeleza wazi kuwa Rais akishatangazwa hakuna njia ya kumtoa kisheria. Isitoshe, tunajiuliza kama madai yao yamejikita kwenye mabadiliko ya Katiba, je, njia sahihi ilikuwa ni kumvunjia heshima Rais kwa kudharau hotuba yake ya kuzindua Bunge ambalo yeye(Rais) ni sehemu ya chombo hicho?
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha mpasuko wa wenyewe kwa wenyewe, baadhi ya wabunge hao wa Chadema waliongia bungeni na kutoka nje, wengine hawakuingia kabisa lakini walionekana wakivinjari nje. Yawezekana kabisa waliobaki nje hawakukubaliana na msimamo huo wa kususia hotuba ya Rais.
Tena kibaya zaidi, baadhi ya wapiga kura wa chama hicho na wadau wengine walioohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC) na Sauti ya America(VOA) walionyesha kukerwa na uamuzi huo. Wapo waliosema ni utovu wa nidhamu, wengine wakisema ni kitendo cha aibu huku wengine wakidai wamewaangusha wapiga kura ambao waliwatuma kuwakilisha na siyo kususia shughuli za bunge, ikiwemo uzinduzi wa Bunge.
Baadhi ya wabunge wa chama hicho ambao bila shaka walisononeka zaidi japokuwa walimezea, ni wale wapya ambao ndio kwanza wanajifunza shughuli, taratibu na kanuni za Bunge zinavyoendeshwa. Pengine ndiyo yale yaale ya bendera hufuata upepo kukidhi matakwa ya wakubwa zao.
Sisi tunadhani, kama kweli wabunge hawa wa Chadema wako ‘serious', wamepania, basi wakae nje ya Bunge wakisubiri maridhiano kama kilivyowahi kufanya Chama cha Wananchi(CUF) ambacho kilikataa matokeo ya Urais huko Zanzibar na walikaa nje ya bunge kwa miaka mitatu bila kuhudhuria vikao hadi mazungumzo yalipoanza. Hawakupokea posho, mishahara wala masurufu yoyote. Swali ni je, Chadema wataweza ungangari huo?
Ni vema siasa zenye mwelekeo huo zikaachwa na badala yake Chadema wakatafuta suluhu ya malalamiko yao kwa njia nyingine isiyoleta mgawanyiko ndani ya chama chenyewe na pia nchini mwetu.
Hakuna sababu ya kumvunjia heshima Rais aliyechaguliwa na wananchi kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na wagombea wengine. Na kusema ukweli, kitendo kile cha kususa kusikiliza hotuba ya JK bungeni hakikuwa ndio sululisho la madai yao bali kujishushia hadhi na kujizushia matatizo mengine yasiyostahili.
CHANZO: THE GUARDIAN

Chadema watupiana lawama
Na Mwandishi wetu
21st November 2010

Wadai lilikuwa shinikizo la mabosi

Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe, aliyevaa miwani akiwaongoza wabunge wa chama chake kutoka katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Siku chache baada ya Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kususia hotuba ya ufunguzi wa Bunge iliyotolewa na Rais, Jakaya Kikwete, baadhi ya wabunge wapya wa chama hicho walioshiriki kitendo hicho, wameibuka na kusema hatua ile haikuwa utashi wao, bali kwa shinikizo la baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Wabunge hao, wamesema iliwabidi kushiriki uamuzi ule kwa shingo upande, kwa kuhofia kuwa wasingeeleweka kwa viongozi wao na kuonekana wasaliti, lakini mioyoni mwao hawakuona mantiki yoyote ya kususia hotuba ya Rais ya ufunguzi wa Bunge, ikizingatiwa kuwa walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi waliowachagua.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini kwa sababu zinazoeleweka, wabunge hao ambao hii ni mara ya kwanza kuingia bungeni baada ya kushinda wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, walisema kitendo hicho ambacho kimepokewa kwa hisia tofauti na watu wengi, kimekidhalilisha chama chao badala ya kukisaidia.
Mmoja wa wabunge hao, alisema hapingani na chama chake kulalamikia matokeo yaliyompa ushindi Rais Kikwete, bali hakufurahishwa na uamuzi wa kuonyesha hisia hizo kwa kususia kikao muhimu cha ufunguzi wa bunge wakati Rais akihutubia.
Alisema kitendo hicho kimewachukiza wananchi wengi na kimejenga picha mbaya kwa wananchi kuwa chama hicho ni cha watu wenye visasi, wasio wavumilivu wa kisiasa na wanaopenda kutumia njia za mitafaruku kutatua matatizo badala ya njia za kidiplomasia.
Mbunge mwingine kijana wa chama hicho, alisema alitamani asishiriki kitendo cha kususia hutuba ya rais, lakini alishindwa kufanya hivyo, kwa kuwa baadhi ya viongozi wa juu walikuwa na msimamo mkali kuhusiana na suala hilo, hivyo asingeshiriki angejiweka katika mazingira magumu ndani ya chama.
"Unajua sisi bado ni wageni ndani ya chama na hili ndiyo bunge letu la kwanza, tusingeweza kwenda kinyume na matakwa ya viongozi wetu, japokuwa sisi wenyewe hatukufurahia jambo lile", alisema mbunge huyo.
Mbunge mwingine mpya wa Chadema, ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kile alichosema kuepuka msuguano na viongozi wake, alisema kuwa kitendo hicho kimewafanya wabunge wa Chadema kueleweka vibaya kwa wapiga kura wao waliowatuma kwenda bungeni kuwawakilisha.
"Lazima tukubaliane na ukweli kuwa baadhi ya wananchi waliotuchagua kwenye nafasi ya ubunge kwenye urais waliamua kumpa kura Kikwete, sasa tunapomsusia tunakuwa hatueleweki tunaonekana kama tumewasaliti wananchi".
"Hata ukiangalia wanaotuunga mkono kwenye jambo hili ni walewale walioonyesha kutuunga mkono tangu wakati wa kampeni, lakini kiukweli wananchi wengi hawajafurahia na hili si jambo jema. Lakini nadhani viongozi wetu watakuwa wamejifunza kitu, kwani binadamu tunajifunza kutokana na makosa", aliongeza kusema mbunge huyo.
Aliongeza kusema kuwa, kitendo hicho kinaweza kuwapa wasiwasi wananchi kuwa wabunge wa chama hicho watatumia muda mwingi kuvutana na serikali badala ya kushughulikia matatizo yao na kutekeleza ahadi walizoahidi wakati wa kampeni.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi waandamizi na wabunge maarufu wa Chadema ambao inaelezwa hawakuunga mkono msimamo wa wenzao kususia hotuba ya Rais Kikwete hawakushiriki katika kitendo hicho.
Inaelezwa kuwa wakati wa kikao cha kujadili kama ipo haja ya wabunge wa chama hicho kususia hotuba ya rais au la kulitokea mvutano mkali, baadhi wakipinga na wengine wakiunga mkono msimamo huo.
Baadhi ya wabunge ambao hawakuingia kabisa bungeni siku lilipotokea tukio hilo kwa sababu ambazo hazijajulikana na hivyo kutoshiriki katika kitendo hicho cha kutoka nje ya ukumbi wa bunge ni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Mpanda Said Arfi, Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya.
Wabunge wa Chadema walisusa na kutoka bungeni wakati Rais Jakaya Kikwete anaanza kulihutubia Bunge kulifungua rasmi Alhamisi iliyopita.
Hali hiyo isiyo ya kawaida ilisababisha kelele bungeni zikiwemo za wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwazomea wenzao waliosusa.
Mara baada ya wabunge wa Chadema kutoka ukumbini, wabunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) walikwenda kukaa kwenye viti vya waliosusa, Rais Kikwete akaendelea kuhutubia.
Katika hotuba yake, Rais Kikwete amesema, waliofanya hivyo wanapaswa kutambua kuwa hawana Rais, yeye ndiye Rais wao na kwamba hawana sehemu nyingine ya kupeleka mahitaji yao hivyo watakwenda, watarudi.
"Hata wale ambao hawakuichagua CCM bado hawana Rais, Serikali yao ni hii hii", amesema Kikwete kabla ya kumaliza kulihutubia Bunge mjini Dodoma wiki hii.
Mara baada ya Rais kumaliza kulihutubia Bunge, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaeleza wabunge kuwa, baadhi ya vyama vimeanza kuonyesha mwelekeo usio sahihi.
Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania wasiruhusu mtu yeyote kuwagawa hivyo waseme hapana.
Kwa mujibu wa Chadema, wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu, kura za mgombea wao, Dk. Willbrod Slaa ziliibwa ili kumpa ushindi Kikwete.
Chama hicho kimesema, licha ya kutomtambua Kikwete, wabunge na madiwani wake wataendelea na kazi kama kawaida katika vyombo hivyo vya uwakilishi.
Wabunge wa Chadema pia wamekataa uteuzi alioufanya Kikwete kumteua Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Kitendo hicho cha Chadema kimepokelewa kwa hisia mbalimbali na wananchi huku wengine wakisema kimetekeleza haki yao ya kidemokrasia, wengine wakilaani na kukieleza kuwa ni utovu wa nidhamu, kukosa busara na kutokamaa kidemokrasia.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

UDOM yaitaka Chadema kuomba radhi
Na Sharon Sauwa
21st November 2010
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Dodoma, wamewataka wabunge wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kufikiria upya msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ili kulinda maslahi ya wapigakura wao.
Kauli hiyo ilitolewa na wanafunzi wa vyuo vikuu mjini hapa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana wabunge hao kususia hotuba ya Rais.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa vyuo vya Mipango, St. John, CBE, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thobias Richard, alidai kuwa lengo la wabunge hao ni kutaka kuhamisha wananchi katika ajenda ya msingi ya maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa.
Richard ambaye ni mwanafunzi wa UDOM, alisema kitendo hicho ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua wabunge hao.
"Kama hawamtambui Rais maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimamia serikali sasa kama hawatambui serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo bungeni," alisema.
Aliwataka wabunge hao kutafakari upya kama kweli wanataka kuwawakilisha bungeni wananchi.
Aliwataka wawaombe radhi Watanzania kwa kuvuruga taswira safi ya Bunge lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa. Alisema kwa kutowaomba radhi wananchi ni kuwadharau Watanzania waliowachagua wakidhani kwamba ni waadilifu kwa taifa na sio chama chao.
Wabunge wa Chadema, walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, Ijumaa wiki iliyopita, lengo likiwa ni kuonyesha kuwa hawamtambui Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
CCM wako kazini ..lakini nafurahi sana kuona hiyo imewaingia na kuwauma haswa..yaani hiyo ni ngumi ya pua ndo maana mpaka leo wanaweweseka
 
Wewe humjui Mengi anavyojipendekeza? yeye huwa anawaambia Wahariri wake eti wamuunge mkono Kikwete lakini wapinge ufisadi. sasa katika hili ameisha ona upepo unakoelekea hataki aje kuvurumishwa kama alivyofanywa na mkapa!
 
Jamani kwani Chadema ni chama kinacho ongozwa na Malaika?Wana chama wake malaika?Mie huwa sipati picha hapa JF !washabiki na wanachama wa chadema hapa JF(ambao ndiye wengi)hawapendi kusikia chadema inakosolewa au inasema kama vile ni chama kinacho ongozwa na malaika !
 
CCM wamewalipa fedha nyingi IPP Media wakati wa kampeni, isingekuwa busara Mengi kuwatosa, ila tunashukuru matoleo yaliyopita waliwaunga mkono CHADEMA
 
GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI HII LIMEANDIKA HABARI ZA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA BUNGE LIKIEGEMEA KWENYE UPANDE MMOJA TU WENYE KUPINGA. HABARI HIZO NIMEZIWEKA HAPO CHINI. KUNA HABARI KUU TATU TOFAUTI KWENYE GAZETI HILI. KUBWA ZAIDI NI MAONI YA MHARIRI NA NYINGINE MBILI NI HABARI ZA WAANDISHI WAO. HABARI ZOTE HIZI NI NEGATIVE VIEWS. HIVYO KAMA KUNA MTU AMBAYE HAJUI NI NINI KILITOKEA NA AKASOMA GAZETI HILI BASI ATAPATA VERY NEGATIVE SIDE YA HABARI HIZI KWA UPANDE WA CHADEMA KITU AMBACHO SI KWELI HATA KIDOGO.

KWA KIFUPI GAZETI HILI LINATAKA KUTUMA UJUMBE KWAMBA WABUNGE WA CHADEMA WALIKOSEA NA HAKUNA WATU WALIOWAUNGA MKONO KWA KITENDO CHAO CHA KUTOKA NJE YA BUNGE. LAKINI KINACHOSEMWA NA GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI SI KWELI. KITENDO CHA WABUNGE WA CHADEMA KIMEUNGWA MKONO NA WATU WENGI NA WENGI WAMEKITA NI CHA KISHUJAA.

KILA MTU MWENYE AKILI TIMAMU NA NIA NJEMA NA TAIFA LA TANZANIA ANAJUA KABISA MCHAKATO WA UCHAGUZI HASA KATIKA KUHESABU KURA ULIKUWA NA KASORO NYINGI TU KIASI KWAMBA KUNA WAGOMBEA WALISHINDA KWA KUTUMIA UJANJA WA KUGEUZA MATOKEO YA KURA ZA WANANCHI. NA HII SIO SIRI TENA. NEC YENYEWE ILIKIRI KUFANYA MAKOSA KATIKA JIMBO LA GEITA, PIA HIVI KARIBUNI BAADA YA NEC KURUDIA KUHESABU KURA ZA UBUNGE JIMBO LA VUNJO ILIONEKANA KUWA MGOMBEA WA UBUNGE WA CCM ALIKUWA AMEPATA KURA NYINGI ISIVYOSITAHILI KATIKA MATOKEO YA AWALI AMBAO YALITANGAZWA NA TUME HIYO HIYO. MGOMBEA WA TLP ALIKUWA AMEPATA 50% LAKINI BAADA YA KURUDIA KUHESABU ALIPATA 54%. HII NI KWA UBUNGE TU, SASA HATUJUI KWA UPANDE WA URAIS NA MADIWANI. HATA HIVYO KUTOKANA NA KUBADILIKA KWA MATOKEO TENA KWA 4% MHE MREMA WA TLP AMESEMA ANA WASIWASI MADIWANI WA CHAMA CHAKE WALISHINDA LAKINI WAKANYIMWA USHINDI KIUJANJA TU.

KWA KIFUPI KATIKA MIFANO HII MIWILI CCM IMEONEKANA KUPEWA KURA NYINGI ISIVYOSITAHILI.

OK TUACHANE NA MAELEZO MENGI.

KITU MUHIMU HAPA NAPENDA KUSHAURI GAZETI LA NIPESHA HASWA MHARIRI WAKE KUANDIKA HABARI ZAKE BILA KUEGEMEA UPANDE WOWOTE KWA MAANA KUSEMA UKWELI SIKU ZOTE. KINYUME NA HAPO HALITAKUWA TOFAUTI NA MAGAZETI YA VYAMA VYA SIASA AMBAYO YANAANDIKA HABARI ILI KUPIGIA DEBE CHAMA CHAO.

HABARI TATU ZA GAZETI HILI NI HIZI HAPA CHINI.

Chadema kumsusia JK bungeni siyo suluhisho, bali ni kujishushia hadhi
Na Editor
21st November 2010
Wiki hii wakati Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kutoa hutuba yake ya kulizindua Bunge la 10 mjini Dodoma, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) walitoa nje ya bunge kwa kile walichosema hawamtambui rais kwa kuwa ushindi aliopata eti siyo halali.
Haishangazi kwa kuwa kilichotokea Dodoma ni muendelezo wa chama hicho ambapo viongozi wake wa juu walisusia wakati wa kutangazwa matokeo ya mshindi wa urais Jakaya Kikwete, wakasusia alipoapishwa pale Uwanja wa Uhuru na wiki hii wabunge wa chama hicho wakasusa hotuba yake kulizindua Bunge. Hata wakati wa kuapishwa Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda imeelezwa hawakuhudhuria kwa sababu zile zile.
Chadema wanasahau kwamba Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za Bunge na pale bungeni hakosekani. Kama walimsusa Chamwino, pale Bungeni napo watamsusa?
Pale bungeni wabunge huuliza maswali ambayo hujibiwa na mawaziri kwa niaba ya serikali ambayo kimantiki ndiyo waheshimiwa hao wanamkataa Rais aliyeiunda.
Kituko cha pale bungeni siyo siri kiliwaacha Watanzania midomo wazi kutokana na kutoeleweka maudhui yake. Mara tu baada ya Rais kuanza kumshukuru Mungu kisha aanze hotuba yake, wabunge wote wa Chadema waliinuka na kuanza kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakiongozwa na kiongozi wao wa upinzani bungeni, Freeman Mbowe, wengine wakiinamisha vichwa chini. Wabunge wa CCM waliwazomea muda wote walipokuwa wakitoka nje.
Kitendo kile, japokuwa wenyewe walikiona cha kijasiri, lakini kimewatia dosari na kuonekana cha kitoto zaidi. Tulidhani kwamba kama ni malalamiko yanayohusiana na matokeo uchaguzi mkuu uliopita, basi suluhu ipatikane kwa mazungumzo na siyo kusababisha mgawanyiko kama ambao umeanza kujitokeza hivi sasa.
Chadema bila shaka wanaelewa fika kwamba sheria inaeleza wazi kuwa Rais akishatangazwa hakuna njia ya kumtoa kisheria. Isitoshe, tunajiuliza kama madai yao yamejikita kwenye mabadiliko ya Katiba, je, njia sahihi ilikuwa ni kumvunjia heshima Rais kwa kudharau hotuba yake ya kuzindua Bunge ambalo yeye(Rais) ni sehemu ya chombo hicho?
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha mpasuko wa wenyewe kwa wenyewe, baadhi ya wabunge hao wa Chadema waliongia bungeni na kutoka nje, wengine hawakuingia kabisa lakini walionekana wakivinjari nje. Yawezekana kabisa waliobaki nje hawakukubaliana na msimamo huo wa kususia hotuba ya Rais.
Tena kibaya zaidi, baadhi ya wapiga kura wa chama hicho na wadau wengine walioohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC) na Sauti ya America(VOA) walionyesha kukerwa na uamuzi huo. Wapo waliosema ni utovu wa nidhamu, wengine wakisema ni kitendo cha aibu huku wengine wakidai wamewaangusha wapiga kura ambao waliwatuma kuwakilisha na siyo kususia shughuli za bunge, ikiwemo uzinduzi wa Bunge.
Baadhi ya wabunge wa chama hicho ambao bila shaka walisononeka zaidi japokuwa walimezea, ni wale wapya ambao ndio kwanza wanajifunza shughuli, taratibu na kanuni za Bunge zinavyoendeshwa. Pengine ndiyo yale yaale ya bendera hufuata upepo kukidhi matakwa ya wakubwa zao.
Sisi tunadhani, kama kweli wabunge hawa wa Chadema wako ‘serious’, wamepania, basi wakae nje ya Bunge wakisubiri maridhiano kama kilivyowahi kufanya Chama cha Wananchi(CUF) ambacho kilikataa matokeo ya Urais huko Zanzibar na walikaa nje ya bunge kwa miaka mitatu bila kuhudhuria vikao hadi mazungumzo yalipoanza. Hawakupokea posho, mishahara wala masurufu yoyote. Swali ni je, Chadema wataweza ungangari huo?
Ni vema siasa zenye mwelekeo huo zikaachwa na badala yake Chadema wakatafuta suluhu ya malalamiko yao kwa njia nyingine isiyoleta mgawanyiko ndani ya chama chenyewe na pia nchini mwetu.
Hakuna sababu ya kumvunjia heshima Rais aliyechaguliwa na wananchi kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na wagombea wengine. Na kusema ukweli, kitendo kile cha kususa kusikiliza hotuba ya JK bungeni hakikuwa ndio sululisho la madai yao bali kujishushia hadhi na kujizushia matatizo mengine yasiyostahili.
CHANZO: THE GUARDIAN

Chadema watupiana lawama
Na Mwandishi wetu
21st November 2010

Wadai lilikuwa shinikizo la mabosi

Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe, aliyevaa miwani akiwaongoza wabunge wa chama chake kutoka katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Siku chache baada ya Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kususia hotuba ya ufunguzi wa Bunge iliyotolewa na Rais, Jakaya Kikwete, baadhi ya wabunge wapya wa chama hicho walioshiriki kitendo hicho, wameibuka na kusema hatua ile haikuwa utashi wao, bali kwa shinikizo la baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Wabunge hao, wamesema iliwabidi kushiriki uamuzi ule kwa shingo upande, kwa kuhofia kuwa wasingeeleweka kwa viongozi wao na kuonekana wasaliti, lakini mioyoni mwao hawakuona mantiki yoyote ya kususia hotuba ya Rais ya ufunguzi wa Bunge, ikizingatiwa kuwa walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi waliowachagua.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini kwa sababu zinazoeleweka, wabunge hao ambao hii ni mara ya kwanza kuingia bungeni baada ya kushinda wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, walisema kitendo hicho ambacho kimepokewa kwa hisia tofauti na watu wengi, kimekidhalilisha chama chao badala ya kukisaidia.
Mmoja wa wabunge hao, alisema hapingani na chama chake kulalamikia matokeo yaliyompa ushindi Rais Kikwete, bali hakufurahishwa na uamuzi wa kuonyesha hisia hizo kwa kususia kikao muhimu cha ufunguzi wa bunge wakati Rais akihutubia.
Alisema kitendo hicho kimewachukiza wananchi wengi na kimejenga picha mbaya kwa wananchi kuwa chama hicho ni cha watu wenye visasi, wasio wavumilivu wa kisiasa na wanaopenda kutumia njia za mitafaruku kutatua matatizo badala ya njia za kidiplomasia.
Mbunge mwingine kijana wa chama hicho, alisema alitamani asishiriki kitendo cha kususia hutuba ya rais, lakini alishindwa kufanya hivyo, kwa kuwa baadhi ya viongozi wa juu walikuwa na msimamo mkali kuhusiana na suala hilo, hivyo asingeshiriki angejiweka katika mazingira magumu ndani ya chama.
"Unajua sisi bado ni wageni ndani ya chama na hili ndiyo bunge letu la kwanza, tusingeweza kwenda kinyume na matakwa ya viongozi wetu, japokuwa sisi wenyewe hatukufurahia jambo lile", alisema mbunge huyo.
Mbunge mwingine mpya wa Chadema, ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kile alichosema kuepuka msuguano na viongozi wake, alisema kuwa kitendo hicho kimewafanya wabunge wa Chadema kueleweka vibaya kwa wapiga kura wao waliowatuma kwenda bungeni kuwawakilisha.
"Lazima tukubaliane na ukweli kuwa baadhi ya wananchi waliotuchagua kwenye nafasi ya ubunge kwenye urais waliamua kumpa kura Kikwete, sasa tunapomsusia tunakuwa hatueleweki tunaonekana kama tumewasaliti wananchi".
"Hata ukiangalia wanaotuunga mkono kwenye jambo hili ni walewale walioonyesha kutuunga mkono tangu wakati wa kampeni, lakini kiukweli wananchi wengi hawajafurahia na hili si jambo jema. Lakini nadhani viongozi wetu watakuwa wamejifunza kitu, kwani binadamu tunajifunza kutokana na makosa", aliongeza kusema mbunge huyo.
Aliongeza kusema kuwa, kitendo hicho kinaweza kuwapa wasiwasi wananchi kuwa wabunge wa chama hicho watatumia muda mwingi kuvutana na serikali badala ya kushughulikia matatizo yao na kutekeleza ahadi walizoahidi wakati wa kampeni.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi waandamizi na wabunge maarufu wa Chadema ambao inaelezwa hawakuunga mkono msimamo wa wenzao kususia hotuba ya Rais Kikwete hawakushiriki katika kitendo hicho.
Inaelezwa kuwa wakati wa kikao cha kujadili kama ipo haja ya wabunge wa chama hicho kususia hotuba ya rais au la kulitokea mvutano mkali, baadhi wakipinga na wengine wakiunga mkono msimamo huo.
Baadhi ya wabunge ambao hawakuingia kabisa bungeni siku lilipotokea tukio hilo kwa sababu ambazo hazijajulikana na hivyo kutoshiriki katika kitendo hicho cha kutoka nje ya ukumbi wa bunge ni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Mpanda Said Arfi, Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya.
Wabunge wa Chadema walisusa na kutoka bungeni wakati Rais Jakaya Kikwete anaanza kulihutubia Bunge kulifungua rasmi Alhamisi iliyopita.
Hali hiyo isiyo ya kawaida ilisababisha kelele bungeni zikiwemo za wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwazomea wenzao waliosusa.
Mara baada ya wabunge wa Chadema kutoka ukumbini, wabunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) walikwenda kukaa kwenye viti vya waliosusa, Rais Kikwete akaendelea kuhutubia.
Katika hotuba yake, Rais Kikwete amesema, waliofanya hivyo wanapaswa kutambua kuwa hawana Rais, yeye ndiye Rais wao na kwamba hawana sehemu nyingine ya kupeleka mahitaji yao hivyo watakwenda, watarudi.
“Hata wale ambao hawakuichagua CCM bado hawana Rais, Serikali yao ni hii hii”, amesema Kikwete kabla ya kumaliza kulihutubia Bunge mjini Dodoma wiki hii.
Mara baada ya Rais kumaliza kulihutubia Bunge, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaeleza wabunge kuwa, baadhi ya vyama vimeanza kuonyesha mwelekeo usio sahihi.
Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania wasiruhusu mtu yeyote kuwagawa hivyo waseme hapana.
Kwa mujibu wa Chadema, wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu, kura za mgombea wao, Dk. Willbrod Slaa ziliibwa ili kumpa ushindi Kikwete.
Chama hicho kimesema, licha ya kutomtambua Kikwete, wabunge na madiwani wake wataendelea na kazi kama kawaida katika vyombo hivyo vya uwakilishi.
Wabunge wa Chadema pia wamekataa uteuzi alioufanya Kikwete kumteua Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Kitendo hicho cha Chadema kimepokelewa kwa hisia mbalimbali na wananchi huku wengine wakisema kimetekeleza haki yao ya kidemokrasia, wengine wakilaani na kukieleza kuwa ni utovu wa nidhamu, kukosa busara na kutokamaa kidemokrasia.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

UDOM yaitaka Chadema kuomba radhi
Na Sharon Sauwa
21st November 2010
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Dodoma, wamewataka wabunge wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kufikiria upya msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ili kulinda maslahi ya wapigakura wao.
Kauli hiyo ilitolewa na wanafunzi wa vyuo vikuu mjini hapa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana wabunge hao kususia hotuba ya Rais.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa vyuo vya Mipango, St. John, CBE, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thobias Richard, alidai kuwa lengo la wabunge hao ni kutaka kuhamisha wananchi katika ajenda ya msingi ya maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa.
Richard ambaye ni mwanafunzi wa UDOM, alisema kitendo hicho ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua wabunge hao.
“Kama hawamtambui Rais maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimamia serikali sasa kama hawatambui serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo bungeni,” alisema.
Aliwataka wabunge hao kutafakari upya kama kweli wanataka kuwawakilisha bungeni wananchi.
Aliwataka wawaombe radhi Watanzania kwa kuvuruga taswira safi ya Bunge lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa. Alisema kwa kutowaomba radhi wananchi ni kuwadharau Watanzania waliowachagua wakidhani kwamba ni waadilifu kwa taifa na sio chama chao.
Wabunge wa Chadema, walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, Ijumaa wiki iliyopita, lengo likiwa ni kuonyesha kuwa hawamtambui Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Ndugu yangu,

Tunafurahi wengi wetu wenye akili ya kutafiti mambo kwamba tunashukuru ujumbe umewafikia vema na ndiyo maana waandishi wenye akili finyu wanatumika.
 
upupu mtupu sijawahi poteza pesa kununua gazeti la nipashe. habari zao very shallow
 
Kilichobaki ni Kampeni ya Boycut Media Product za IPP. Vyombo Hivi Havina Manufaa kwa Wananchi na Kusoma Ipp na Vyombo vya Serikali na Television Yao Hakuna Credible News kwa Manufaa ya Umma. Wengi Hatupati News Kutoka Vyombo vya Serikali na Ipp. Tuna Uhakika Ipp Itakufa Tu. Mengi Hajui Yeye ni Mfanyabiashara na Anategemea Consumers Kununua Products Zake na Ukiangalia Mpaka Sasa Mengi Hapati Profits Hivyo Kulinganisha na Hapo Awali. Tueneze Kampeni ya Kutonunua Mengi Products na Wote Wasaliti wa Nchi Yetu.
 
kilichobaki ni kampeni ya boycut media product za ipp. Vyombo hivi havina manufaa kwa wananchi na kusoma ipp na vyombo vya serikali na television yao hakuna credible news kwa manufaa ya umma. Wengi hatupati news kutoka vyombo vya serikali na ipp. Tuna uhakika ipp itakufa tu. Mengi hajui yeye ni mfanyabiashara na anategemea consumers kununua products zake na ukiangalia mpaka sasa mengi hapati profits hivyo kulinganisha na hapo awali. Tueneze kampeni ya kutonunua mengi products na wote wasaliti wa nchi yetu.

mi nina muda mrefu sasa nimesitisha matumizi ya products zote za makampuni ya ipp, makampuni yanayoendeshwa na mafisadi.
 
Lazima wtanzania tufahamu kwamba nguvu ya KIKWETE na wapambe wake na wanawe ni kubwa sana sana katika nchi hii,na watanzania bila kusimamisha hii kasi kwa nguvu zetu zote si miaka mingi ijayo tutaingia kwenye machafuko makubwa sana
KIKWETE ni mtu hatari sana kwanza alianza kuendesha nchii hii mwaka mmoja kabla Mkapa hajaondoka mtandao wake ulikuwa umekita katika sehemu zote nyeti jeshi ,usalama wa taifa,serikalini na vyombo vya habari na mahakama

kutokana na visasi alivyokuwa amejilimbikizia na uhasama ulioibukka ndani ya CCM walitumia njia ya kura za maoni kuwamaliza mahasimu wao na kutumia pesa nyingi kuwanq,oa watendaji wazuri wa CCM waliokuwa mstari wa mbele kukosoa serikali yake kwa nia njema kabisa kama akina shelukindo,seleli, shibuda, sitta sita mwakyembe kukosa nguvu ya wanyakyusa alishatoswa zamani
kuhakikisha anatengeneza mtandao wa kuiba kura ili abaki madarakani kutumia familia na pesa za umma kuwanunua watu ili waweze kubambikiza kura za kujalizia
kinachonisikitisha sasa hii hali ya kuingia kwenye taasisi nyeti kama vyuo kuvitumia kwa propaganda hii ni hatari sana kama anavyojenga dhana ya udini kujineemesha kisiasa huyu mtu anatuangamiza n kubaliana na DR Slaa aliposema kumuacha KIKWETE na CCM madarakani ni maafa
naogopa alivyo mbaya anaweza hata akafanya operesheni za siri kukatisha uhai wa baadhi ya viongozi wa CHADEMA si muamini kabisa
ni mbinafsi mno na mroho sana wa madaraka kwa namna nyingine ni dikteta
 
Ukweli ni kwamba wananchi ndio tuliunga mkono suala la wabunge wa Chadema kumwacha Mkwere. Tunajua hatukumchagua anajilazimisha kuwa rais wetu kwa kutumia udhaifu wa katiba. IPP msitudanganye, kama mnataka kupima na kutaka kujua ukweli, CCM waitishe maandamano ya kupinga kitendo kile au Chadema waruhusiwe kuitisha maandamo ya kuunga mkono kitendo kile. hapo mtajua ukweli uko wapi.

Kumbukeni wakati wa Kampeni Jk alikuwa akiwasomba watu ili uwanja wa jangwani ujae watu wakati Chadema iliwapata watu hata zaidi ya wale waliokuwa wakifika kwenye kampeni ya CCM lakini bila kuwasomba. Nani atakana hilo? kura zetu mmechakachua msichakachue mawazo yetu.
 
Hii habari isiwatishe maana tunaosoma magazeti ni sisi wa mjini, huko village walikojaa sisiemu hawa habari na magazeti.

Sisi ndio tunajua ukweli uko wapi hata wakipotosha vipi. Pia wabunge wetu watazidi kuwaelimisha wananchi wapenda demokrasia ukweli uko wapi.

Demkorasia ya kweli itapatikana tu bado hatujakata tamaa.
 
Magazeti potofu yanajenga fikira potofu, intellectual people cant buy such shallow magazine........Dont expect company with cheap labour wakaproduce product nzuri...wanahongwa na mafisadi ili wapotoshe umma wakati ukweli wanaujua.Im saying this coz baadhi yao ni watu wangu wa karibu....i cant list them coz watakufa njaa
 
Cha ajabu ni kuwa wakati nipashe unawaponda wabunge wa ccm the guardian inaandika habari zinazozitaka vyama vyote waamue kwa busara. Hapo ndipo unapoweza kuanza kukuna kichwa kwamba hawa wanafanya mambo kwa kufikiri au ndo hivyo waandishi wanasahau ujumbe wao una madhara agin katika jamii:bump:
 
Uhuru wa vyombo vya habari uzingatiwe...msitegemee CHADEMA kusifiwa tu.....wakati mwingine lazima ipondwe!
 
Back
Top Bottom