Nipashe Jumapili yaandika negative tupu kuhusu wabunge wa CHADEMA kutoka bungeni

GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI HII LIMEANDIKA HABARI ZA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA BUNGE LIKIEGEMEA KWENYE UPANDE MMOJA TU WENYE KUPINGA. HABARI HIZO NIMEZIWEKA HAPO CHINI. KUNA HABARI KUU TATU TOFAUTI KWENYE GAZETI HILI. KUBWA ZAIDI NI MAONI YA MHARIRI NA NYINGINE MBILI NI HABARI ZA WAANDISHI WAO. HABARI ZOTE HIZI NI NEGATIVE VIEWS. HIVYO KAMA KUNA MTU AMBAYE HAJUI NI NINI KILITOKEA NA AKASOMA GAZETI HILI BASI ATAPATA VERY NEGATIVE SIDE YA HABARI HIZI KWA UPANDE WA CHADEMA KITU AMBACHO SI KWELI HATA KIDOGO.


KWA KIFUPI GAZETI HILI LINATAKA KUTUMA UJUMBE KWAMBA WABUNGE WA CHADEMA WALIKOSEA NA HAKUNA WATU WALIOWAUNGA MKONO KWA KITENDO CHAO CHA KUTOKA NJE YA BUNGE. LAKINI KINACHOSEMWA NA GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI SI KWELI. KITENDO CHA WABUNGE WA CHADEMA KIMEUNGWA MKONO NA WATU WENGI NA WENGI WAMEKITA NI CHA KISHUJAA.


KILA MTU MWENYE AKILI TIMAMU NA NIA NJEMA NA TAIFA LA TANZANIA ANAJUA KABISA MCHAKATO WA UCHAGUZI HASA KATIKA KUHESABU KURA ULIKUWA NA KASORO NYINGI TU KIASI KWAMBA KUNA WAGOMBEA WALISHINDA KWA KUTUMIA UJANJA WA KUGEUZA MATOKEO YA KURA ZA WANANCHI. NA HII SIO SIRI TENA. NEC YENYEWE ILIKIRI KUFANYA MAKOSA KATIKA JIMBO LA GEITA, PIA HIVI KARIBUNI BAADA YA NEC KURUDIA KUHESABU KURA ZA UBUNGE JIMBO LA VUNJO ILIONEKANA KUWA MGOMBEA WA UBUNGE WA CCM ALIKUWA AMEPATA KURA NYINGI ISIVYOSITAHILI KATIKA MATOKEO YA AWALI AMBAO YALITANGAZWA NA TUME HIYO HIYO. MGOMBEA WA TLP ALIKUWA AMEPATA 50% LAKINI BAADA YA KURUDIA KUHESABU ALIPATA 54%. HII NI KWA UBUNGE TU, SASA HATUJUI KWA UPANDE WA URAIS NA MADIWANI. HATA HIVYO KUTOKANA NA KUBADILIKA KWA MATOKEO TENA KWA 4% MHE MREMA WA TLP AMESEMA ANA WASIWASI MADIWANI WA CHAMA CHAKE WALISHINDA LAKINI WAKANYIMWA USHINDI KIUJANJA TU.


KWA KIFUPI KATIKA MIFANO HII MIWILI CCM IMEONEKANA KUPEWA KURA NYINGI ISIVYOSITAHILI.



OK TUACHANE NA MAELEZO MENGI.

KITU MUHIMU HAPA NAPENDA KUSHAURI GAZETI LA NIPESHA HASWA MHARIRI WAKE KUANDIKA HABARI ZAKE BILA KUEGEMEA UPANDE WOWOTE KWA MAANA KUSEMA UKWELI SIKU ZOTE. KINYUME NA HAPO HALITAKUWA TOFAUTI NA MAGAZETI YA VYAMA VYA SIASA AMBAYO YANAANDIKA HABARI ILI KUPIGIA DEBE CHAMA CHAO.

HABARI TATU ZA GAZETI HILI NI HIZI HAPA CHINI.




Chadema kumsusia JK bungeni siyo suluhisho, bali ni kujishushia hadhi
Na Editor
21st November 2010
Wiki hii wakati Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kutoa hutuba yake ya kulizindua Bunge la 10 mjini Dodoma, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) walitoa nje ya bunge kwa kile walichosema hawamtambui rais kwa kuwa ushindi aliopata eti siyo halali.
Haishangazi kwa kuwa kilichotokea Dodoma ni muendelezo wa chama hicho ambapo viongozi wake wa juu walisusia wakati wa kutangazwa matokeo ya mshindi wa urais Jakaya Kikwete, wakasusia alipoapishwa pale Uwanja wa Uhuru na wiki hii wabunge wa chama hicho wakasusa hotuba yake kulizindua Bunge. Hata wakati wa kuapishwa Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda imeelezwa hawakuhudhuria kwa sababu zile zile.
Chadema wanasahau kwamba Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za Bunge na pale bungeni hakosekani. Kama walimsusa Chamwino, pale Bungeni napo watamsusa?
Pale bungeni wabunge huuliza maswali ambayo hujibiwa na mawaziri kwa niaba ya serikali ambayo kimantiki ndiyo waheshimiwa hao wanamkataa Rais aliyeiunda.
Kituko cha pale bungeni siyo siri kiliwaacha Watanzania midomo wazi kutokana na kutoeleweka maudhui yake. Mara tu baada ya Rais kuanza kumshukuru Mungu kisha aanze hotuba yake, wabunge wote wa Chadema waliinuka na kuanza kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakiongozwa na kiongozi wao wa upinzani bungeni, Freeman Mbowe, wengine wakiinamisha vichwa chini. Wabunge wa CCM waliwazomea muda wote walipokuwa wakitoka nje.
Kitendo kile, japokuwa wenyewe walikiona cha kijasiri, lakini kimewatia dosari na kuonekana cha kitoto zaidi. Tulidhani kwamba kama ni malalamiko yanayohusiana na matokeo uchaguzi mkuu uliopita, basi suluhu ipatikane kwa mazungumzo na siyo kusababisha mgawanyiko kama ambao umeanza kujitokeza hivi sasa.
Chadema bila shaka wanaelewa fika kwamba sheria inaeleza wazi kuwa Rais akishatangazwa hakuna njia ya kumtoa kisheria. Isitoshe, tunajiuliza kama madai yao yamejikita kwenye mabadiliko ya Katiba, je, njia sahihi ilikuwa ni kumvunjia heshima Rais kwa kudharau hotuba yake ya kuzindua Bunge ambalo yeye(Rais) ni sehemu ya chombo hicho?
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha mpasuko wa wenyewe kwa wenyewe, baadhi ya wabunge hao wa Chadema waliongia bungeni na kutoka nje, wengine hawakuingia kabisa lakini walionekana wakivinjari nje. Yawezekana kabisa waliobaki nje hawakukubaliana na msimamo huo wa kususia hotuba ya Rais.
Tena kibaya zaidi, baadhi ya wapiga kura wa chama hicho na wadau wengine walioohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC) na Sauti ya America(VOA) walionyesha kukerwa na uamuzi huo. Wapo waliosema ni utovu wa nidhamu, wengine wakisema ni kitendo cha aibu huku wengine wakidai wamewaangusha wapiga kura ambao waliwatuma kuwakilisha na siyo kususia shughuli za bunge, ikiwemo uzinduzi wa Bunge.
Baadhi ya wabunge wa chama hicho ambao bila shaka walisononeka zaidi japokuwa walimezea, ni wale wapya ambao ndio kwanza wanajifunza shughuli, taratibu na kanuni za Bunge zinavyoendeshwa. Pengine ndiyo yale yaale ya bendera hufuata upepo kukidhi matakwa ya wakubwa zao.
Sisi tunadhani, kama kweli wabunge hawa wa Chadema wako serious, wamepania, basi wakae nje ya Bunge wakisubiri maridhiano kama kilivyowahi kufanya Chama cha Wananchi(CUF) ambacho kilikataa matokeo ya Urais huko Zanzibar na walikaa nje ya bunge kwa miaka mitatu bila kuhudhuria vikao hadi mazungumzo yalipoanza. Hawakupokea posho, mishahara wala masurufu yoyote. Swali ni je, Chadema wataweza ungangari huo?
Ni vema siasa zenye mwelekeo huo zikaachwa na badala yake Chadema wakatafuta suluhu ya malalamiko yao kwa njia nyingine isiyoleta mgawanyiko ndani ya chama chenyewe na pia nchini mwetu.
Hakuna sababu ya kumvunjia heshima Rais aliyechaguliwa na wananchi kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na wagombea wengine. Na kusema ukweli, kitendo kile cha kususa kusikiliza hotuba ya JK bungeni hakikuwa ndio sululisho la madai yao bali kujishushia hadhi na kujizushia matatizo mengine yasiyostahili.
CHANZO: THE GUARDIAN


Chadema watupiana lawama
Na Mwandishi wetu
21st November 2010

Wadai lilikuwa shinikizo la mabosi

Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe, aliyevaa miwani akiwaongoza wabunge wa chama chake kutoka katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Siku chache baada ya Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kususia hotuba ya ufunguzi wa Bunge iliyotolewa na Rais, Jakaya Kikwete, baadhi ya wabunge wapya wa chama hicho walioshiriki kitendo hicho, wameibuka na kusema hatua ile haikuwa utashi wao, bali kwa shinikizo la baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Wabunge hao, wamesema iliwabidi kushiriki uamuzi ule kwa shingo upande, kwa kuhofia kuwa wasingeeleweka kwa viongozi wao na kuonekana wasaliti, lakini mioyoni mwao hawakuona mantiki yoyote ya kususia hotuba ya Rais ya ufunguzi wa Bunge, ikizingatiwa kuwa walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi waliowachagua.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini kwa sababu zinazoeleweka, wabunge hao ambao hii ni mara ya kwanza kuingia bungeni baada ya kushinda wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, walisema kitendo hicho ambacho kimepokewa kwa hisia tofauti na watu wengi, kimekidhalilisha chama chao badala ya kukisaidia.
Mmoja wa wabunge hao, alisema hapingani na chama chake kulalamikia matokeo yaliyompa ushindi Rais Kikwete, bali hakufurahishwa na uamuzi wa kuonyesha hisia hizo kwa kususia kikao muhimu cha ufunguzi wa bunge wakati Rais akihutubia.
Alisema kitendo hicho kimewachukiza wananchi wengi na kimejenga picha mbaya kwa wananchi kuwa chama hicho ni cha watu wenye visasi, wasio wavumilivu wa kisiasa na wanaopenda kutumia njia za mitafaruku kutatua matatizo badala ya njia za kidiplomasia.
Mbunge mwingine kijana wa chama hicho, alisema alitamani asishiriki kitendo cha kususia hutuba ya rais, lakini alishindwa kufanya hivyo, kwa kuwa baadhi ya viongozi wa juu walikuwa na msimamo mkali kuhusiana na suala hilo, hivyo asingeshiriki angejiweka katika mazingira magumu ndani ya chama.
"Unajua sisi bado ni wageni ndani ya chama na hili ndiyo bunge letu la kwanza, tusingeweza kwenda kinyume na matakwa ya viongozi wetu, japokuwa sisi wenyewe hatukufurahia jambo lile", alisema mbunge huyo.
Mbunge mwingine mpya wa Chadema, ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kile alichosema kuepuka msuguano na viongozi wake, alisema kuwa kitendo hicho kimewafanya wabunge wa Chadema kueleweka vibaya kwa wapiga kura wao waliowatuma kwenda bungeni kuwawakilisha.
"Lazima tukubaliane na ukweli kuwa baadhi ya wananchi waliotuchagua kwenye nafasi ya ubunge kwenye urais waliamua kumpa kura Kikwete, sasa tunapomsusia tunakuwa hatueleweki tunaonekana kama tumewasaliti wananchi".
"Hata ukiangalia wanaotuunga mkono kwenye jambo hili ni walewale walioonyesha kutuunga mkono tangu wakati wa kampeni, lakini kiukweli wananchi wengi hawajafurahia na hili si jambo jema. Lakini nadhani viongozi wetu watakuwa wamejifunza kitu, kwani binadamu tunajifunza kutokana na makosa", aliongeza kusema mbunge huyo.
Aliongeza kusema kuwa, kitendo hicho kinaweza kuwapa wasiwasi wananchi kuwa wabunge wa chama hicho watatumia muda mwingi kuvutana na serikali badala ya kushughulikia matatizo yao na kutekeleza ahadi walizoahidi wakati wa kampeni.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi waandamizi na wabunge maarufu wa Chadema ambao inaelezwa hawakuunga mkono msimamo wa wenzao kususia hotuba ya Rais Kikwete hawakushiriki katika kitendo hicho.
Inaelezwa kuwa wakati wa kikao cha kujadili kama ipo haja ya wabunge wa chama hicho kususia hotuba ya rais au la kulitokea mvutano mkali, baadhi wakipinga na wengine wakiunga mkono msimamo huo.
Baadhi ya wabunge ambao hawakuingia kabisa bungeni siku lilipotokea tukio hilo kwa sababu ambazo hazijajulikana na hivyo kutoshiriki katika kitendo hicho cha kutoka nje ya ukumbi wa bunge ni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Mpanda Said Arfi, Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya.
Wabunge wa Chadema walisusa na kutoka bungeni wakati Rais Jakaya Kikwete anaanza kulihutubia Bunge kulifungua rasmi Alhamisi iliyopita.
Hali hiyo isiyo ya kawaida ilisababisha kelele bungeni zikiwemo za wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwazomea wenzao waliosusa.
Mara baada ya wabunge wa Chadema kutoka ukumbini, wabunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) walikwenda kukaa kwenye viti vya waliosusa, Rais Kikwete akaendelea kuhutubia.
Katika hotuba yake, Rais Kikwete amesema, waliofanya hivyo wanapaswa kutambua kuwa hawana Rais, yeye ndiye Rais wao na kwamba hawana sehemu nyingine ya kupeleka mahitaji yao hivyo watakwenda, watarudi.
Hata wale ambao hawakuichagua CCM bado hawana Rais, Serikali yao ni hii hii, amesema Kikwete kabla ya kumaliza kulihutubia Bunge mjini Dodoma wiki hii.
Mara baada ya Rais kumaliza kulihutubia Bunge, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaeleza wabunge kuwa, baadhi ya vyama vimeanza kuonyesha mwelekeo usio sahihi.
Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania wasiruhusu mtu yeyote kuwagawa hivyo waseme hapana.
Kwa mujibu wa Chadema, wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu, kura za mgombea wao, Dk. Willbrod Slaa ziliibwa ili kumpa ushindi Kikwete.
Chama hicho kimesema, licha ya kutomtambua Kikwete, wabunge na madiwani wake wataendelea na kazi kama kawaida katika vyombo hivyo vya uwakilishi.
Wabunge wa Chadema pia wamekataa uteuzi alioufanya Kikwete kumteua Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Kitendo hicho cha Chadema kimepokelewa kwa hisia mbalimbali na wananchi huku wengine wakisema kimetekeleza haki yao ya kidemokrasia, wengine wakilaani na kukieleza kuwa ni utovu wa nidhamu, kukosa busara na kutokamaa kidemokrasia.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

UDOM yaitaka Chadema kuomba radhi
Na Sharon Sauwa
21st November 2010
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Dodoma, wamewataka wabunge wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kufikiria upya msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ili kulinda maslahi ya wapigakura wao.
Kauli hiyo ilitolewa na wanafunzi wa vyuo vikuu mjini hapa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana wabunge hao kususia hotuba ya Rais.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa vyuo vya Mipango, St. John, CBE, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thobias Richard, alidai kuwa lengo la wabunge hao ni kutaka kuhamisha wananchi katika ajenda ya msingi ya maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa.
Richard ambaye ni mwanafunzi wa UDOM, alisema kitendo hicho ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua wabunge hao.
Kama hawamtambui Rais maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimamia serikali sasa kama hawatambui serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo bungeni, alisema.
Aliwataka wabunge hao kutafakari upya kama kweli wanataka kuwawakilisha bungeni wananchi.
Aliwataka wawaombe radhi Watanzania kwa kuvuruga taswira safi ya Bunge lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa. Alisema kwa kutowaomba radhi wananchi ni kuwadharau Watanzania waliowachagua wakidhani kwamba ni waadilifu kwa taifa na sio chama chao.
Wabunge wa Chadema, walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, Ijumaa wiki iliyopita, lengo likiwa ni kuonyesha kuwa hawamtambui Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Kama sijakosea sana, mhariri wake ametokea magazeti ya CCM na ana itikadi zile zilee...tuwahurumie, wanaojikomba..
 
Nadhani huu ni uthibitisho wa habari zilizoandkwa na gazeti moja jana au mwanajamvi kuwa CCM ina mkakati wa kuwanunua wahariri na kuhakikisha wanaandika habari nzuri juu ya CCM na kuiponda Chadema. Hivyo Chadema ni lazima wawe na kampeni kali ya kujibu mapigo ikiwa ni pamoja na kuwa na redio na kituo cha runinga cha kujibu uvumi na uzushi wa CCM na vituo habari-manunuzi kama Nipashe.
 
Jamani kwani Chadema ni chama kinacho ongozwa na Malaika?Wana chama wake malaika?Mie huwa sipati picha hapa JF !washabiki na wanachama wa chadema hapa JF(ambao ndiye wengi)hawapendi kusikia chadema inakosolewa au inasema kama vile ni chama kinacho ongozwa na malaika !

sasa watu wakisema ukweli ndio kosa. Nani hajui nipashe walifanya kazi kwa maelekezo ya CCM? Kwa sasa wanahaha maana kama ni ngumi walisema haiumi wametulia sasa wakagundua imauma saaaana, but messege sent and delivered
 
Itashangaza kama hununui "Nipashe" lakini unanunua "Tanzania Daima" ni sawa na kuruka mkojo na..........!
duh huwezi fananisha njiwa na mbuni pia kuna watu wanajipendekeza kweli kama hapa UDOM watu wanasifia kitendo cha CHADEMA kutoka bungeni lakini kibaraka mmoja anasema eti CHADEMA iombe radhi, huyu ni kada wa CCM tunaomba aache kulamba miguu ya mafisadi
 
CCM wako kazini ..lakini nafurahi sana kuona hiyo imewaingia na kuwauma haswa..yaani hiyo ni ngumi ya pua ndo maana mpaka leo wanaweweseka (QUOTE).

Inashangaza kuona mtu anakuwa na mawazo ya aina hii. CHADEMA wamefanya kosa halafu mtu anasema kuwa eti CHADEMA wamepiga 'ngumi ya pua'. Sasa je , huyo aliyechokozwa akiamua kupiga ngumi kwenye chembe ya moyo (solar plexus) si tutashuhudia kifo?

Tatizo la wafuasi wa CHADEMA ni kuwa hawajui watendalo kama ilivyo kwa viongozi wenyewe, baadhi yao, wa CHADEMA ambao ni wahuni. CHADEMA kwa kuwa na wabunge wengi bungeni wanaleta siasa za ujivuni, za majivuno, za kujisikia, za dharau, za ugomvi, za vitisho.

Ukimsikiliza Mbowe ndio utagundua ajenda ya CHADEMA ambayo eti ni kuishinikiza serikali iwe na mazungumzo mezani. MBOWE anasema kuwa wanjiandaa kuchukua serikali katika uchaguzi ujao. Sijui ni serikali gani hiyo wanataka kuchukua. Kilicho dhahiri ni kuwa CHADEMA will never never never win presidential elections in this country. Watanzania sio wa jana na hawezi kufanya makosa ya kumpa mgombea wa CHADEMA awe ndiye rais. Huwezi.

Imani ya CHADEMA siku zote ukisikiliza kauli za viongozi wao mbalimbali ni kuwa watanzania wa sasa sio wale wa jana. Thisi is true. lakini kwa upande mwingine haina maana kuwa eti watanzania hawa ndio waipe CHADEMA. Ni kweli CHADEMA wamepata kura nyingi mwaka huu. lakini ni wazi kuwa tayari wameanza kupotea katika mwelekeo wao. Wasidhani kuwa watanzania ni wajinga kiasi hicho. Wapiga kura wameipa CHADEMA kura nyingi kutokana na hasira kwa lengo la kuimasha CCM. Uchaguzi unaokuja CHADEMA hawawezi kupata kura walizopata katika uchaguzi huu ikiwa wataendeleza sera za ujivuni.

NI wazi sasa CHADEMA wameanza kutetemeka kwa kitendo walichofanya cha kishenzi na ujinga cha kususia hotuba ya JK. Kwani kweli kuwa upo uwezekano wa wao kuenguliwa bungeni kwa kuvunja katiba ibara ya 62 kwa kutotambua sehemu moja ya Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hoja kuwa eti walisusia hotuba hiyo kwa lengo la kupeleka ujumbe ni ya kihuni kwani mtu huwezi ukavua nguo hadharani halfu uje utambe kwa watu kuwa eti 'message sent'. Aidha eti kwa kuwa unas bifu na Jiji kwa kuendekeza uchafu huwezi mtu mwenye akili zako ukaamua kuweka kinyesi barabarani ukishuhudiwa na watu na uje utamke kuwa 'nilikuwa nawasilisha ujumbe'.

Sasa hao CHADEMA wameanza kujichanganya. Eti walichofanya siyo kutomtambua Rais bali hawayatambui matokeo yualiyomweka JK madarakani. Yaani hapa wanacheza na lugha. Huu ni ujinga mtupu. Sasa kama wanamtambua JK isipokuwa matokeo yaliyomweka sasa kwanini wmsusie JK? Kama kweli hoja yao ina nguvu si wangeisusia NEC?

Tusubiri tuone lakini wazi kuwa CHADEMA watakuja ujutia uamuzi huo wa kitoto wa kususia hotuba ya JK.
 
Wala siwashangai IPP MEDIA kama pia mlifuatilia vipindi nyao kwenye ITV wakati wa uchaguzi utaona walikua wanaegemea upande mmoja japokua walikua wanaingizaingiza hotuba za Julius Kambarage Nyerere kuwazuga watazamaji!
 
Ukweli unajulikana na kamwe hawataweza kutudanganya,ila inaonyesha ni namna gani walivyo na mawazo finyu.Watu wameshaamka na hawatalala tena.
 
Chadema wanasahau kwamba Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za Bunge na pale bungeni hakosekani
Naomba nisaidiwe elimu hapa, Hivi Waziri Mkuu ndie kiongozi wa shughuli za Bunge pale bungeni au ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. That Author needs to get his shit back to school. Mengi fukuza kazi na ajiri mhariri mwingine atakaeendeleza propaganda zako kitaalamu zaidi.

Kitendo kile, japokuwa wenyewe walikiona cha kijasiri, lakini kimewatia dosari na kuonekana cha kitoto zaidi. Tulidhani kwamba kama ni malalamiko yanayohusiana na matokeo uchaguzi mkuu uliopita, basi suluhu ipatikane kwa mazungumzo na siyo kusababisha mgawanyiko kama ambao umeanza kujitokeza hivi sasa.

Suluhu ipatikane kwa mazungumzo, kwani kinacholalamikiwa kilipatikana kwa mazumgumzo? Kuna aina mbali mbali za kufikisha malalamiko, na njia waliyotumia CHADEMA ni moja wapo ya njia hizo. Wasi wasi wangu huyu mwandishi/mhariri akiendelea hivi 2015 atasema asimamishwe yeye kugombea uraisi kwa ticket ya CHADEMA.
 
Jamani kwani Chadema ni chama kinacho ongozwa na Malaika?Wana chama wake malaika?Mie huwa sipati picha hapa JF !washabiki na wanachama wa chadema hapa JF(ambao ndiye wengi)hawapendi kusikia chadema inakosolewa au inasema kama vile ni chama kinacho ongozwa na malaika !
Acha ushabiki na uzembe wa kufikiri mkuu, kuna mambo yakukubali kukosolewa lakini siyo hili.
 
Wahariri uchwara wenye njaa kali na wasiopenda ustawi wa Taifa hili la Tanzania kamwe hawataacha KUNUNULIWA NA CCM NA MAFISADI ILI WAENDELEE KUANDIKA HABARI ZA UONGO KUWA NI ZA UKWELI NA KINYUME CHAKE.

NI WATU WANAFIKI TU KAMA CCM WANAWEZA KUFURAHIA HABARI HIZI ZA KIZUSHI, LAKINI KWA THINK TANKS NA GREAT THINKERS HAKUNA WA KUDANGANYIKA.

I BELIEVE BY THE GRACE OF GOD WITHIN 1-2 YEARS, TANZANIA IS GOING TO HAVE A NEW CONSTITUTION. THEREAFTER WE GONNA MEET IN THE GENERAL ELECTION 2015! TUONE KAMA HAMTANG'OKA HAPO IKULU! BRAVO CHADEMA!

CCM MPO??? SAFARI HII HADANGANYIKI MTU.
 
Huyo jamaa/BOSS wa IPPMEDIA au humjui siku hizi ni mmoja wao. Angalia hata wakati wa uchaguzi alieegemea wapi:embarrassed:
 
Hallo hapo.

Wabunge sasa hivi wanarudi kwenye majimbo yao kuwashukuru wananchi na kufahamu matatizo ya wananchi. Kwa hiyo wabunge wa Chadema wachukue nafasi hiyo kuwaelimisha wananchi kuhusu hatua ile.

Ni kweli wananchi wa kawaida hawakuelewa, ila sasa wanaanza kupata mwanga. Kwa hiyo tuendelee kuwaelimisha wananchi kuhusu wabunge wa Chadema kutola bungeni.
 
Mimi concern yangu ni hao watoto wa UDOM. Udom is nothing but another honeypot of CCM. Huyo dogo anayezungumzia fate ya wapigakura wa Chadema, yeye mwenyewe ni wa chama gani. Anafahamu kuwa watu wa kutuomba radhi watanzania wote ni CCM na si mwingine?
Ajichukulie degree yake ya kisiasa hapo alipo aende akaungane na wenzie kupora raslimali zetu wakati tunajipanga kwa ujio wa mwisho wa kuiondoa CCM.
 
1954 what the hell is JK. Fisadi!!, mchakachuaji!! I WILL NEVER RESPECT LOW PEOPLE LIKE THAT MKWERE. To Hell!!!
 
Kuna tetesi kuwa mhariri wa gazeti la Nipashe Jumapili, Bi. Flora Wingia, ameahidiwa na mafisadi walio karibu na watawala kuwa akiendelea kukitukana CHADEMA na Dk. WILLIBROD SLAA na kumpamba Kikwete na CCM yake basi atapewa ukuu wa wilaya (DC) kwenye uteuzi unaotarajiwa kufanywa na Kikwete muda si mrefu sana baada ya kutangaza baraza la mawaziri wiki hii.

Hawa ndiyo wahariri wetu, na haya ndiyo magazeti yetu ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom